Kuwa na shule zinazofua hadi nguo za watoto, ni matokeo ya uzembe na kupenda kuiba mali za umma!

Kuwa na shule zinazofua hadi nguo za watoto, ni matokeo ya uzembe na kupenda kuiba mali za umma!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Mtoto anakuwa boarding maisha yake yote, huko hafanyi kazi yoyote, hafui wala kukimbia mchakamchaka, tumeiga mifumo ya wapi huko?

Na hapa ndipo chanzo cha kuharibu vijana wa nchi hii,

Mtoto ambaye hawezi kufanya kazi zaidi ya kukaa tu, atapata wapi uchungu wa nchi na maliasili zake?

Ataweza kufanya kazi gani zaidi ya kupiga pesa za wananchi

mtu asiyefanya kazi tangu utoto hulemaa kiakili na hawezi kuwa mbunifu popote zaidi ya kuwa mzigo kwenye taifa lake

Ndiyo hao watoto wanaouwa wazazi wao ili warithi baada ya kupigwa na ukali wa maisha

Na ndiyo hao wanaokuja kuwa viongozi wanaamini katika uganga badala ya uchapa kazi

Wizara ya Elimu, futeni huu utaratibu wa hovyo unaotamalaki sasa kwenye Taifa hili,

Wazazi wanaotaka watoto wao wasifanye kazi mashuleni, wapeleke watoto wao nje ya nchi!
 
Ili ccm iwe madarakani lazima nchi iwe na wajinga na wavivu wengi, kwahyo mimi kama chipukizi naunga mkono mfumo huo uwe mpaka shule za kata.
 
Ili ccm iwe madarakani lazima nchi iwe na wajinga na wavivu wengi, kwahyo mimi kama chipukizi naunga mkono mfumo huo uwe mpaka shule za kata.
Taja basi manufaa yake mkuu
 
Umenikumbusha mtoto wa dada yangu yupo darasa la sita hata soks hawez kufua.
 
Kwani umelazimishwa upeleke mtoto huko?
 
Umelazimishwa kumpeleka mwanao hiyo shule? Kwanini mnapenda kujidai mbumbumbu kila kitu serikali iwafanyie?
 
Back
Top Bottom