Ndiyo. Mzee Nyerere aliwaita mabeberu wakaiangusha bei ya zao la mkonge halina bei hadi leo. Alipokuja Mzee Mwinyi akabadilisha jina wakawa wahisani au wafadhali, Mzee Mkapa akawaita wawekezaji. Mzee Kikwete akawaita wadau wa maendeleo sasa awamu hii tunaanza kurudi kule kule kwa Nyerere ambaye walimtaiti mpaka akaukimbia urais
..hapana.
..Mwalimu Nyerere alikiri kwamba alikosea kutaifisha mashamba ya mkonge.
..alikiri kwamba alikuwa na uelewa mdogo kuhusu ugumu wa serikali kuendesha kwa ufanisi sekta ya mkonge.
..lakini zaidi Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, " you have to use Capitalists to build Socialism.."
..Mwalimu alishirikiana na mataifa ya kijamaa, na vilevile alishirikiana na mataifa ya kibepari.