Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Mkuu..

Unasema ubeberu ni ubepari iliokomaa?!!

Na IMPERIALISM ni nini?!!!

Je si tusi kumuita mtu imperialist?!!

Sijui tunafurahishana tu hapa....
Wanajitoa ufahamu kwa mahaba niuwe!
 
Mnachanga maneno mabeberu ni hawa hapa[emoji116]

Akaulizwa beberu ni nani? Akajibu: "Beberu hana rangi wala utaifa, beberu ni mtu, taasisi au taifa lolote ambalo tukiwa hatuna hospitali, barabara, madaraja, ndege na vingine muhimu kwa maendeleo wanatubeza; tukianza kuvijenga na kuvifanyia kazi wananuna na kujaribu kuhujumu na kuvibeza bila hoja; mtu wa namna hii awe Mtanzania au si Mtanzania ni beberu tu," alisema.
 
Ni elimu yako ndogo tu ndio inakufanya uone neno beberu ni tusi ,malaumu babako kwa kushindwa kukupa elimu ya kutosha

Capitalism -ubapari
Capitalist -bepari
Imperialism -ubeberu
Imperialist -beberu
Socialism -ujamaa
Socialist -mjamaa

Kwa kuwa wao hutuita wajamaa nasi tunawaita mabeberu (imperialists -mabaeberu)

Imperialism is highest level of capitalism -ubeberu ni ubepari uliokomaa

USSR
Hivi we unaamini viongozi wetu wanafata Sera za ujamaa

Ova
 
USAID help us ARV(antiretrovirus drugs) for free of charge....

Kule kwao KICHUPA kimoja cha Vidonge 100 ni dola 300....imagine?!!!

Can we afford to produce it?!!
Can we afford to distribute to our CITIZENS for free?!!!!

How about drugs against Tuberculosis(TB)?!!!

Though am not supporting each and everything they do against third world countries but through globalization they are the most dearest FRIENDS than CHINESE...look at MKAPA FOUNDATION on health....

Look on what they help us fighting against Porchers in our game reserves?!!!
Can Chinese support us the same as US and our European counterpart does....?!!!!

1.DANIDA
2.SIDA
3.GTZ
4.USAID
5.NORPLAN
6.FINLAND
7.JICA
8.KOREA et al

Though we stand as NATIONALISTS but we should RESERVE our words against these DEVELOPMENT PARTNERS and not what honourable Gwajima SAID today....
 
Wanajamvi,

kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa ya binafsi na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!

Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenye huku ukichekelea! Sasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, na hili wahusika walilifahamu hata kabla ya kampeni kuanza, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu? Tena hata wakati wa kuwazungumzia wagombea wengine

Matokeo yoyote yamabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!

Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi. Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao!

Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa CCM kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.

Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi ambapo CCM hawana njia ya kukwepa lawama.

Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi.

Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi.

Kwasababu wananchi huwa wanajiskia hiruna kunufaika na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku.

Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?

Sasa ukizingatia kuwa tunaweza kuwekewa vikwazo, kwasababu ya yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na jitihada za kuminya demokrasia, watakaoendelea kuteseka bila sababu ni wananchi ambao wengi ni masikini.
Duniani huwezi kujitetea hata kama una uwezo wa kifedha bado kuna huduma au bidhaa utazipata kwa mtu ambaye ni masikini
 
Silika za ubaguzi toka juu. Changanya na ccm. Balaa kwa Taifa!
 
Ni elimu yako ndogo tu ndio inakufanya uone neno beberu ni tusi ,malaumu babako kwa kushindwa kukupa elimu ya kutosha

Capitalism -ubapari
Capitalist -bepari
Imperialism -ubeberu
Imperialist -beberu
Socialism -ujamaa
Socialist -mjamaa

Kwa kuwa wao hutuita wajamaa nasi tunawaita mabeberu (imperialists -mabaeberu)

Imperialism is highest level of capitalism -ubeberu ni ubepari uliokomaa

USSR
Umemaliza mkuu,
vijana wengi elimu ni shida, siasa zakiharakati zimeharibu ubongo, wanapaswa kuelimishwa kidogokidogo.
Wataelewa tu.
 
Duniani huwezi kujitetea hata kama una uwezo wa kifedha bado kuna huduma au bidhaa utazipata kwa mtu ambaye ni masikini
Yeah ndio maana hayo mataifa makubwa yana mahusiano NASI...

Hawawezi KUJITENGA...
Hatuwezi KUJITENGA....

Laa muhimu ni WIN WIN SITUATIONS tu...

Maendeleo hayana VYAMA
 
Umemaliza mkuu,
vijana wengi elimu ni shida, siasa zakiharakati zimeharibu ubongo, wanapaswa kuelimishwa kidogokidogo.
Wataelewa tu.
Wewe ndiyo utaelewa, subiri tu uone kama ushamba unalipa na matusi ya reja reja.
 
USAID help us ARV(antiretrovirus drugs) for free of charge....

Kule kwao KICHUPA kimoja cha Vidonge 100 ni dola 300....imagine?!!!

Can we afford to produce it?!!
Can we afford to distribute to our CITIZENS for free?!!!!

How about drugs against Tuberculosis(TB)?!!!

Though am not supporting each and everything they do against third world countries but through globalization they are the most dearest FRIENDS than CHINESE...look at MKAPA FOUNDATION on health....

Look on what they help us fighting against Porchers in our game reserves?!!!
Can Chinese support us the same as US and our European counterpart does....?!!!!

1.DANIDA
2.SIDA
3.GTZ
4.USAID
5.NORPLAN
6.FINLAND et al

Though we stand as NATIONALISTS but we should RESERVE our words against these DEVELOPMENT PARTNERS and not what honourable Gwajima SAID today....
Wameshindwa kuwahudumia wananchi. Wameshindwa kuwaondoa kwenye umasikini wa kutupwa. Wanawadanganya kuwa umasikini wao umesababishwa na mabeberu wanaoshirikiana na upinzani. Wako radhi kubakia madarakani na kuwatumia wananchi kwa manufaa yao binafsi huku wakitetea chama ambacho kipo madarakani tokea uhuru.
 
Ni elimu yako ndogo tu ndio inakufanya uone neno beberu ni tusi ,malaumu babako kwa kushindwa kukupa elimu ya kutosha

Capitalism -ubapari
Capitalist -bepari
Imperialism -ubeberu
Imperialist -beberu
Socialism -ujamaa
Socialist -mjamaa

Kwa kuwa wao hutuita wajamaa nasi tunawaita mabeberu (imperialists -mabaeberu)

Imperialism is highest level of capitalism -ubeberu ni ubepari uliokomaa

USSR
Kuna ubepari na ubapari ulio komaa..ebu fafanua vizuri umekomaa vipi..?

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kiufupi wakitoa misaada ni wahisaninwa maendeleo..ila wakihoji kuhusu demokrasia..utawala bora na haki za binadamu ndio wanaitwa mabeberu..[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119] kuwa mataga ni laana kwa nchi.

Trump kiboko ya mashoga ,mashoga wanamhaha
Hivi unafahamu mwenyekiti wenu siyo tu ni “narcissist”, lakini pia ni mtu mwenye kubagua bagua tu. Ni mbaguzi wa kila namna. Yeye na Trumper ni sawa kabisa.
 
Wanajamvi,

kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa ya binafsi na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!

Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenye huku ukichekelea! Sasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, na hili wahusika walilifahamu hata kabla ya kampeni kuanza, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu? Tena hata wakati wa kuwazungumzia wagombea wengine

Matokeo yoyote yamabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!

Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi. Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao!

Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa CCM kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.

Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi ambapo CCM hawana njia ya kukwepa lawama.

Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi.

Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi.

Kwasababu wananchi huwa wanajiskia hiruna kunufaika na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku.

Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?

Sasa ukizingatia kuwa tunaweza kuwekewa vikwazo, kwasababu ya yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na jitihada za kuminya demokrasia, watakaoendelea kuteseka bila sababu ni wananchi ambao wengi ni masikini.
Wewe endelea kuota tu, eti maendeleo yatakuja na ufadhili. Tumefadhiliwa tangu tulipopata uhuru, lakini 2015 hapajakuwa na meandeleo yoyote. Nchi zilizokuwa nyuma ka,ma Korea Kusini, malaysia, Vietnam, etc zote zimeendelea kwa kutumia pesa za ndani tu. Wewe bado unatamani na kung'ang'ania kufadhili. Wewe ni sawea na baba wa familia anayeshindwa kulisha familia yake akitegemea misaada na kuhemea kutoka kwa ndugu na marafiki. ebu angalia kutegemea kwetu mapato ya ndani kumetufikisha wapi katika miaka mitano (UCHUMI WA KATI).Mtu mwenye aklili na kutaka kuendelea ataendelea tu kwa kutotegemea misaada peke yake. Kwanza hata hiyo misaada huwa ina masharti ya kuturudisha nyuma wakatyi mwingine. Jitegemee kwanza, mikopo iwe ni pla two.

hivi wewe ukitaka kuanzisha biashara (kujiendeleza) utategemea misaada tu. Kabla hata ya kupata mkopo inabidi waangalie uwezo wako wa kuwalipa, na una nini cha kuchukuwa ukishindwa kulipa.
 
Bila CCM thabiti nchi itayumba.... hapa mwalimu alikuwa sahihi 100%..

Kwa sasa CCM dishi limeyumba..nchi inakwenda kwenye matatizo makubwa!!
 
Wanajamvi,

kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa ya binafsi na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!

Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenye huku ukichekelea! Sasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, na hili wahusika walilifahamu hata kabla ya kampeni kuanza, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu? Tena hata wakati wa kuwazungumzia wagombea wengine

Matokeo yoyote yamabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!

Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi. Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao!

Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa CCM kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.

Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi ambapo CCM hawana njia ya kukwepa lawama.

Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi.

Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi.

Kwasababu wananchi huwa wanajiskia hiruna kunufaika na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku.

Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?

Sasa ukizingatia kuwa tunaweza kuwekewa vikwazo, kwasababu ya yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na jitihada za kuminya demokrasia, watakaoendelea kuteseka bila sababu ni wananchi ambao wengi ni masikini.
Hata wanaotoa kauli hizo, wanajua wanazitoa kisiasa.

Njia rahisi ya kumtawala Muafrika ni kumtengenezea adui wa pamoja, yani hawa wakoloni weusi wa leo kina Magufuli wanaotutawala kwa kuiba kura wakishindwa kutatua matatizo ya wananchi, kimbilio lao ni kuzusha vita dhidi ya "mabeberu".

Hapo wanawachota wananchi.

Na utakuta watu masikini kabisa wanaokandamizwa na hii serikali, na wao wanaitetea, kwa sababu tu wamelishwa ujinga wa "kupigana dhidi ya mabeberu".

Kusema ukweli ubeberu kwa kiasi fulani upo. Dunia ina geopolitics, ina espionage, ina national interests. Kwa hiyo, dhana ya "mabeberu" si kweli kwamba ni ya uongo kabisa.

Ila, wanasiasa wanajua kuitumia kwa manufaa yao, si kwa manufaa ya taifa.

Wanajua kuutumia ukweli fulani mdogo (a kernel of truth) na kuukuza vibaya kwa manufaa yao ya kisiasa.

Maanay yake nini?

Chukulia Wamarekani kwa mfano. Nchi yenyewe imegawanyika. Kuna Democrats na Republicans.Kuna Conservatives na Liberals. Kuna watu wa mijini na wa vijijini. Hawa si wamoja, wenyewe wanapingana.

Kwa kuangalia "popular vote", mshindi, Joe Biden, mpaka sasa, hajafikisha hata 51% ya kura zote. Yuko kwenye 50.8%. Wakati Trump yuko 47.3%.

Katika serikali ya Trump, kuna watu wamejiuzulu kazi serikalini kwa kupingana na muelekeo wa serikali ya Trump.

Rais George W. Bush, a conservative and Republican, ndiye rais aliyeisaidia Africa kuliko marais wote, kuliko hata Obama. Hususan kwenye mambo ya kupigana na magonjwa kama Malaria na AIDS.

Sasa watu hawa very complex. Tuukiwashutumu, basi na shutuma zetu ziwe complex.

Siyo mtu unaiba kura, Wamarekani wakikusema umeiba kura, unajitetea kwa kuwaita mabeberu.

Wakati hata wananchi wako wengi tu wanalalamika umeiba kura na umezima mitandao ya kijamii.

Sasa hao wananchi wako nao ni mabeberu?

Kuiba kura na kuzima mitandao ya kijamii nako si ubeberu?

Beberu ni lazima awe mzungu au Mmarekani?
 
China imeendelea sana
Ilipewa misaada?
Badilisha mtazamo
Umatonya ni fikra mgando
Wewe utakuwa bwege kweli. China imeendelea sana! Nani kakuambia?

China ina pato kubwa la Taifa kutokana na uwingi wa watu na ukubwa wa nchi lakini maendeleo ya watu, bado ni duni sana. Ni nchi ya 89 kwa maendeleo ya watu. Inazidiwa na nchi kama Botswana.

China mpaka leo inahangaika kutafuta wawekezaji toka Ulaya na America. Na waliosaidia uchumi wa China kukua ni wawekezaji kutoka America na Ulaya.

Katika makampuni 10 makubwa kabisa China, kampuni ya China ni moja tu. Nyingine zote ni kampuni za America na Ulaya.

China ndiyo inayoongoza Duniani kwa kuvutia mitaji ya nje. Mitaji inayoingia China kwa mwaka toka Ulaya na America kwaajili ya uwekezaji ni wastani wa dola bilioni 80.

Watu wenye akili ndogo na uelewa mdogo wanadhani China imeendelea sana.

Mwakajana Rais Trump alipendekeza kwenye Baraza la Usalama la Umoj2a wa Mataifa, China iingizwe kwenye nchi zilizoendelea, Waziri Mkuu wa China alipinga sana, na kusema kuwa China bado ni maskini. Wasiangalie GDP pekee pale waangalie uhalisia wa maendelea ya wananchi wa China, ambayo bado ni chini sana.

Lakini kuna wendawazimu Tanzania wanasema eti China ina maendeleo makubwa. Ama kweli kosa vyote, usikose akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiufupi wakitoa misaada ni wahisaninwa maendeleo..ila wakihoji kuhusu demokrasia..utawala bora na haki za binadamu ndio wanaitwa mabeberu..[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119] kuwa mataga ni laana kwa nchi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hivi wewe utajisikia vipi, ukitaka msaada mtui anasema atakusadia lakini lazima ukubali ahoji jinsi wewe unavyoendesha mambo ya familia yako. Wakati ni kweli haki za binadamu ni tatizo kubwa duniani lakini kuna haki gani nchi matajiri kuhoji hayo wakati wao nchini mwao hakuna anayeweza kuwahoji! Hivi wewe unajuwa kuwa Marekani, Chinas, Ulaya yote, Canada, Australia, Neswzealand huwa hawahojiwi kuhusu haki za binadamu. Hivi wewe unajuwa kuwa Mmarekani yeyote hawawezi kushtakiwa kwenye korti ya dunia ya The Hague. Kama kuna nchi yenye kukiuka hgaki zaq binadamu, Marekani inaongoza. Hii ni pamoja na ndani (jinsi inavyowatendea watu weusi na wageni toka dunia ya tatu hasa Waislamu) na nje (majeshi ya Maarekani yanayopigana nje na kuhusika na vifo vya raia maelfu lakini wana kinga ya kushtakiwa kwenye korti ya dunia). Mambo kama haya ni dhahiri kuwa Maarekani inajuwa inakiuka haki za binadamu na ndiyo maana katika mikataba yake yote inajipa kinga ya watu wake kushtakiwa kwenye korti kama ile ya The Hague.
 
Wanajamvi,

kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa ya binafsi na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!

Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenye huku ukichekelea! Sasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, na hili wahusika walilifahamu hata kabla ya kampeni kuanza, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu? Tena hata wakati wa kuwazungumzia wagombea wengine

Matokeo yoyote yamabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!

Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi. Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao!

Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa CCM kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.

Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi ambapo CCM hawana njia ya kukwepa lawama.

Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi.

Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi.

Kwasababu wananchi huwa wanajiskia hiruna kunufaika na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku.

Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?

Sasa ukizingatia kuwa tunaweza kuwekewa vikwazo, kwasababu ya yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na jitihada za kuminya demokrasia, watakaoendelea kuteseka bila sababu ni wananchi ambao wengi ni masikini.
Baada ya kichapo cha mbwa mtu kwenye box la kura naona unaibuka na nyuzi za kitoto. Unajua nini maana ya Beberu? Unadhani kila mfadhili ni Beberu. Unafahamu dhana nzima ya Imperialism? Tumia akili zako unapofanya ukosoaji wa kiuchambuzi.
 
Back
Top Bottom