Wanajamvi,
kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa ya binafsi na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!
Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenye huku ukicheSasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu?
Matokeo yoyote yake mabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!
Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi. Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao!
Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa ccm kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.
Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi ambapo ccm hawana njia ya kukwepa lawama. Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi. Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi. Kwasababu wananchi huwa wanajiskia na kunufaika na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku.
Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?