Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Elimu yako kubwa ndiyo imekufanya uone siyo tusi? Hivi kama wewe siyo kilaza wahed, hapa sijui umlaumu mamako? Mkapiga risasi mnayesema anashirikiana na “siyo tusi”. Wewe akili yako inakutosha wewe peke yako tu. Hapa unaniwekea usiku tu.
Beberu ni mfumo wa kiuongozi sio tusi. Kuna wajamaa(socialist) na mabeberu(imperialist ). Beberu ubepari uliokomaa. Beberu sio tusi
 
muda gani beberu anakuwa beberu na muda gani anakuwa mfadhiri
Hatoweza kujibu hilo, kwasababu wanafahamu ni uongo wanaowalisha wananchi! Lakini wananchi walikataa, sema nguvu imetumika na wizi mkubwa wa kihistoria!

Hilo la mabeberu, wanalitumia ili waweze kutumia dola na nguvu ya jeshi pamoja na usalama wa Taifa! Njia pekee ya ccm kubakia madarakani!
 
Are you really serious jmushi 1? Hawa sio wafadhili wetu,ni wezi na watesi wetu,wake up guys.Halafu unawaremba,eti "wafadhili wetu" dah!Kweli wajinga ndio waliwao.Watch and listen to the following clip uone ukweli wa hao unaowaita "wafadhili wako."

Beberu ni mfumo wa kiuongozi sio tusi. Kuna wajamaa(socialist) na mabeberu(imperialist ). Beberu ubepari uliokomaa. Beberu sio tusi
Hilo ndilo jina linalotumika pale unapokuja ule uongo wa “vita ya kiuchumi” dhidi ya wafadhili wako? Hivi hufahamu sababu za watu kupotezwa hovyo hovyo kwa kutumia vyombo vya dola? Tangu lini jina lenye uadui huo lisiwe tusi na wakati huo huo linaleta ladha hiyo linapotumika kwa minajili ya kisiasa?
 
Beberu ni mfumo wa kiuongozi sio tusi. Kuna wajamaa(socialist) na mabeberu(imperialist ). Beberu ubepari uliokomaa. Beberu sio tusi
Sasa huo mfumo wa kiuogozi, ndiyo unahusianaje na wao kwenye uchaguzi wetu hadi kufanya kila jambo zuri liloongelewa na Upinzani lionekane kuwa ni baya kwa wananchi kwasababu ya “mabeberu” wanaotaka uchaguzi wa huru na haki, Pia demokrasia ya vyama vingi?
 
Kuna kitu nataka ku'post' lakini nimeshakifuta mara tatu. Ngoja nikiache tu.
 
Wengi ambao hawapendi, kwa Africa ni dictators. Ndiyo maana wao hupendelea China zaidi. Au unadhani wafadhili ndiyo kwamba hawako? Ni uchaguzi tu wa serikali.

Pia ni wazi hukunielewa vyema ninaposema “ushamba”, ni kumtukana mamba kabla hujavuka mto. Otherwise hakukuwepo kabisa na haja ya kuingiza Taifa kwenye figisu na wananchi wengi kwenye taabu zaidi.
 
Kama unakumbuka ...kuna kampun moja la ki British liliitwa "IBEACo. Means ....imperial.. British east Africa company ..... hapo umeona neno imperial kwa kiswahil ni BEBERU.....so hata wnyw wananajijua kuwa ni MABEBERU
 
Unajua maana ya BEBERU? why tusiwaite hivyo hali ya kuwa ni kwel Mabeberu? Nawasiwasi na Elimu yako.. huwenda huufahamu Ukoloni ni nini.. na wala hujui Ukoloni mambo leo ni kitu gani..

Inasikitisha
Nimekuwa nikiona watoa Mada wanaopiga vita Ubeberu ila sijabahatika kukuta anayetoa clear definition ya Beberu.Unaweza kutusaidia majina/utambulisho wa Mabeberu ili sisi sote tumtambue huyu adui tishio kwa maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania na Afrika kiujumla.
 
Mbona wao huwa wanatuita sisi masikini/fukara/dunia ya tatu?
 
wafadhili sijui jina gani bibi zenu,etc huo ujinga ni hukohuko cdm,sisi wazungu kina trump na wenzake wote mabeberu hutaki bwekaa tena 😂😊
 
Unajua maana ya BEBERU? why tusiwaite hivyo hali ya kuwa ni kwel Mabeberu? Nawasiwasi na Elimu yako.. huwenda huufahamu Ukoloni ni nini.. na wala hujui Ukoloni mambo leo ni kitu gani..

Inasikitisha
Mabeberu ni nani tupe maana ya mabeberu?
 
Unajua maana ya BEBERU? why tusiwaite hivyo hali ya kuwa ni kwel Mabeberu? Nawasiwasi na Elimu yako.. huwenda huufahamu Ukoloni ni nini.. na wala hujui Ukoloni mambo leo ni kitu gani..

Inasikitisha
Ukolon mambo leo unaongozwa na genge la wahuni ccm
 
wafadhili sijui jina gani bibi zenu,etc huo ujinga ni hukohuko cdm,sisi wazungu kina trump na wenzake wote mabeberu hutaki bwekaa tena 😂😊
Hivi unafahamu mwenyekiti wenu siyo tu ni “narcissist”, lakini pia ni mtu mwenye kubagua bagua tu. Ni mbaguzi wa kila namna. Yeye na Trumper ni sawa kabisa.
 
Mbona wao huwa wanatuita sisi masikini/fukara/dunia ya tatu?
Wana ubavu huo kwasasa! Hata mimi nilichukia sana Trumper aliposema sisi ni “shit hole” nations! Na kweli kwa siasa zetu unadhani siyo?
 
Beberu ni mfumo wa kiuongozi sio tusi. Kuna wajamaa(socialist) na mabeberu(imperialist ). Beberu ubepari uliokomaa. Beberu sio tusi
Mkuu..

Unasema ubeberu ni ubepari iliokomaa?!!

Na IMPERIALISM ni nini?!!!

Je si tusi kumuita mtu imperialist?!!

Sijui tunafurahishana tu hapa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…