Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

Ndiyo. Mzee Nyerere aliwaita mabeberu wakaiangusha bei ya zao la mkonge halina bei hadi leo. Alipokuja Mzee Mwinyi akabadilisha jina wakawa wahisani au wafadhali, Mzee Mkapa akawaita wawekezaji. Mzee Kikwete akawaita wadau wa maendeleo sasa awamu hii tunaanza kurudi kule kule kwa Nyerere ambaye walimtaiti mpaka akaukimbia urais
Hahahahaaaaaa akitoka huyu atakuja mwingine atawaita wahisani,kisha ajaye atawaita wawekezaji....Mzunguko utajirudia.
 
China imeendelea sana
Ilipewa misaada?
Badilisha mtazamo
Umatonya ni fikra mgando
Mikakati ya China kujikwamua inaendana na ya kwetu hapa?.Big vision goes together with big mission.China walifanya Technology transfer.Je,vipi kuhusu sisi?
 
China hawakufanya ujinga huu. Walimweka karibu zaidi mzungu na kumuibia teknolojia ndiyo maaana wakafikia hapo walipo. China hawakufuata “isolationism”

Sikubaliana na umatonya, lakini huu ni ushamba ambao utaligharimu Taifa.
Wewe ndio mshamba wewe kwa akiri yako unazani wazungu wote wanatutakia mema, umesahau hao wazungu ndio walifawanya watumwa babu zetu na kuwatesa tangu lini kupe akawa na mapenzi mema acha ujinga lazima tuwaseme wajue ili sindano iwaingie akiri yako umeiaminisha bila mzungu huwezi hata kama anakunyonya wewe una mkumbatia tuuuuuuu.
 
Wewe endelea kuota tu, eti maendeleo yatakuja na ufadhili. Tumefadhiliwa tangu tulipopata uhuru, lakini 2015 hapajakuwa na meandeleo yoyote. Nchi zilizokuwa nyuma ka,ma Korea Kusini, malaysia, Vietnam, etc zote zimeendelea kwa kutumia pesa za ndani tu. Wewe bado unatamani na kung'ang'ania kufadhili. Wewe ni sawea na baba wa familia anayeshindwa kulisha familia yake akitegemea misaada na kuhemea kutoka kwa ndugu na marafiki. ebu angalia kutegemea kwetu mapato ya ndani kumetufikisha wapi katika miaka mitano (UCHUMI WA KATI).Mtu mwenye aklili na kutaka kuendelea ataendelea tu kwa kutotegemea misaada peke yake. Kwanza hata hiyo misaada huwa ina masharti ya kuturudisha nyuma wakatyi mwingine. Jitegemee kwanza, mikopo iwe ni pla two.

hivi wewe ukitaka kuanzisha biashara (kujiendeleza) utategemea misaada tu. Kabla hata ya kupata mkopo inabidi waangalie uwezo wako wa kuwalipa, na una nini cha kuchukuwa ukishindwa kulipa.
Kujitegemea ni jambo muhimu tena la kulipigania kwa nguvu zote.Tatizo,mikakati.Huwezi kuwa tajiri kwa kujenga uadui na matajiri.Hizo mbinu za utajiri utajifunzia kwa masikini wenzako?
 
Wewe ndio mshamba wewe kwa akiri yako unazani wazungu wote wanatutakia mema, umesahau hao wazungu ndio walifawanya watumwa babu zetu na kuwatesa tangu lini kupe akawa na mapenzi mema acha ujinga lazima tuwaseme wajue ili sindano iwaingie akiri yako umeiaminisha bila mzungu huwezi hata kama anakunyonya wewe una mkumbatia tuuuuuuu.
Wewe ni mwingine ambaye akili yako inakutosha wewe tuu na siyo zaidi ya hapo.

Afadhali lakini wewe akili zako zinakutosha wewe mwenyewe. Kuna ambao akili zao haziwatoshi hata wao wenyewe.

Ni ushauri tu kwasababu sioni cha kuku jibu hapo.
 
Hapa umeandika kishabiki tu.
Kusema “suala la ugaidi Tanzania litaweza kuzuilika kwa serikali za majimbo”, ni ushabiki? Au hujaelewa? Sema Kwanini ni ushabiki kabla sijaichukulia kauli yako ya kimdhaha inavyostahili kuchukuliwa.
 
Inashangaza sana pale watu weusi tunapotaka tusaidiwe kiuchumi na hao watu weupe na huku eti hatutaki watuingilie kisiasa! Hauwezi kufanya maamuzi kupitia mfuko wa mwenzio!
 
Mkuu..

Unasema ubeberu ni ubepari iliokomaa?!!

Na IMPERIALISM ni nini?!!!

Je si tusi kumuita mtu imperialist?!!

Sijui tunafurahishana tu hapa....
Ubepari uliokomaa(Monopoly capitalism).ni sawa na IMperialist, imperialism limetoka na neno Empire( emperior or empress) mtawala anaetawala nje ya mipaka ya nchi zingine. British empire rule Tanganyika. Uingereza ndio mabeberu
 
Inashangaza sana pale watu weusi tunapotaka tusaidiwe kiuchumi na hao watu weupe na huku eti hatutaki watuingilie kisiasa! Hauwezi kufanya maamuzi kupitia mfuko wa mwenzio!
Hatutaki demokrasia ndo maana.
 
Unapoteza utu wako Kwa sababu ya fedha? Wakati unao uwezo wa kujenga uzalendo ukapata fedha tu Kama kila mtazania ataelewa umuhimu wa Uzalendo
 
Unapoteza utu wako Kwa sababu ya fedha? Wakati unao uwezo wa kujenga uzalendo ukapata fedha tu Kama kila mtazania ataelewa umuhimu wa Uzalendo
Kumbuka hii kauli neno uzalendo imeibuka sana hii miaka ya karibuni yaani kama hili taiga lina raia wa aina mbili tuseme waliowazalendo na wasiwazalendo.
Hizi zote ni kauli za kuwagawa watu kwa ujanja wa watu wenye malengo yao kwa faida yao kwa kipindi flani.
Kama taifa lina watu wa aina mbili ni kipimo kipi kinatumika kujua ni idadi ipi inayozidi kuongezeka kama kati ya kundi moja linazidi kuongezeka faida ni ipi kama halina faida tumejiandaje kuangalia wanachokitaka.
Inawezekana wengi wao wanahitaji kusogezewa huduma za kijamii kama ndio hivyo hatuwezi kuyakwepa haya kwani ni haki ya raia.Kujua tatizo la jambo litatusaidia sana sio kejeli wala vijembe maneno mazuri ni dawa juu raia mwenzako
 
Back
Top Bottom