Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?


Bridal Mask?

Lee Kang-to aka Sato Hiroshi.
 
Mkuu kuleta migogoro ya majina i kujipunguzia muda wa kuishi!
Acha watu waitane na kuatizana majia wanayojisikia comfort!
Ukizaa wa kwako mwite unavyotaka, ukimwita kwa kilugha mfao: Nyoronyo, Nyakabibi, Pantalusasi, Neemwannchekwene, Mwakafyusisye, au ya kiswahili : Melesiana, Annalieta, Jailosi, Sindano, Sesilia, Benezeti, Lusiata, Deusdediti n.k.
Kwa ufupi tusiyashangae majina ya kizungu wakati hata serikali tu imeruhusu miji, vitogoji na mitaa yetu kupewa majina ya Kizungu au majina ya nchi za wenzetu. Mfano Dar kuna tunacho kitogoji kiaitwa Morroco, tunayo barabara ya New York n.k
 
Kuna kitu kimoja watu wanashindwa elewa...

Jina la mtu lipo kwenye maana na wala si lugha iliyotumika...

Majina mengi ya kibantu yamebeba maana za ajabu ajabu, kwa sababu wakati wa kale majina ya watu yalitolewa kulingana na majira, matukio, hali n.k. Haina maana kuwa hayapo yenye maana nzuri...
 
Imagine mtoto wako unamwita Masumbuko...

Simple tuu ita mtoto Brightness,Britter,Brighton yaan mpaka raha kabisa
 
Mkuu, Cha muhimu ni maana ya jina tu. Nadhani kila mzazi anampa mwanaye jina linaloakisi uzuri wa jina lenyewe.
 
Huku mtaan jina la Jayden limeshamiri...hawajui lilitoholewa kutoka kwa jina la mama.. jada..

Wabongo buana..ni ushamba tu
 
Mkuu katika maisha tunayoishi, tumetofautiana , mawazo, mitazamo na fikra.. sio dhambi mtu kuwaza tofauti na wewe, au wewe kuwaza tofauti na mwingine.

Sijaona sababu ya wewe kupanic na kumuattack mtu hadi kumuita mfuasi wa shetani..?
 
Forest Hill ndio nini sasa? Kwanini usijiite Gumbo, au Matotola au Vindili nk?
 
Rel
Dunia imeshakuwa kijiji, utamaduni umebadilika sana, kuanzia vyakula mavazi, miziki tunayosikiliza. Sasa kwanini unahoji majina, mbona hiyo ni ishu ndogo tu kwenye mabadiliko ya tamaduni zetu? Moana ni bonge la jina, haujaona kina Megan, Chloe wa hapa Bongo?
 
havinitishi,mwanaasha,mwanamvua,mwanajua,mwananjaa,mwanakimbunga,msiba,mzugwa,mwakijambile,sumbuka..etc
 
Yaani la Mwakatobe liwe baya kuliko la Abdillatif?acha utumwa wewe katika waislamu ni Ditopile mzuzuli tu ndio kakataa utumwa mashujaa ni akina Ambwene,Atupele,Ipyana,Lusajo nk hilo la mwakatobe ni la ukoo, weka akilini mwako usikurupuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…