Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Mtoto aitwe jina lolote tu ambalo mzazi anapenda , hata Kama akiitwa ukwaju ni sawa tu...
 
Habari salamu sio ndefu nimechefukwa mtoto wa dada yangu kapewa jina Moana, jina la kikatuni cha Disney nikapata maswali sana, kwanini hadi leo tunaendelea kushikilia majina ya wageni? Majina mazuri ya Kiswahili, lugha za asili yameisha au ndio tunayaona ya kizamani na hayafai kitu?

Kuna uhusiano gani kati ya kuwa Muislamu na kumpa mtoto jina la kiarabu? Au mkristo kumpa mtoto jina la Kizungu kama Frank, Aboubakar, Sameer, Chris, Dorice, Khadija

Kwanini sio majina ya kichina au kihindi? Labda dini ni kitu chema lakini isiondoe u-Afrika wetu. Tujitafakari.
Mtoto unamuita pombe unatarajia nini 😃
 
Huu huitwa utumwa wa kujitakia wa kiakili usiokoma yaani perpetual mental slavery ambao dini zilipachika kwenye akili za watu wetu hadi wakajifunza kujichukia na kuchukiana huku wakitukuza na kupenda vya wenzao na kuponda vyao. Na hiki ndicho chanzo cha umaskini wetu hadi wanakuja wageni toka mbali wanatajirika miongoni mwetu kwa kututumia wakati tukipigana vita wenywe kw wenyewe wanangu. Nenda Dar uone wahindi wanavyowabagua waswahili lakini wao wakiendelea kuwaramba makalio na kuwatajirisha badala ya kuwasusa. Waarabu kadhalika. Ni aibu na hasara wanangu.
 
Mtoto unamuita pombe unatarajia nini 😃
Ila ukimuita livingstone, zephyr na upuuzi mwingine anakuwa bora kuliko Pombe kweli? Mkumbuke Pombe aka Walwa Magufuli alivyowaamsha toka usingizini wakati akina Ali, Julius na Ben wakiwalaza usingizi wa kupotea.
 
Kwanza mleta mada badili jina lako uitwe Mlima wa Msitu, au Eibanga Ly'eirungu halafu irudishe mada yako tuiweke sawa.
 
Pombe,
Ila ukimuita livingstone, zephyr na upuuzi mwingine anakuwa bora kuliko Pombe kweli? Mkumbuke Pombe aka Walwa Magufuli alivyowaamsha toka usingizini wakati akina Ali, Julius na Ben wakiwalaza usingizi wa kupotea.
Sasa Nani ametaja Magufuli hapo??? Mie nimetaja jina la Pombe tu nakuchagulia jina la mwanao, hayo mengine sijui akina walwa , utayapeleka kwa babu yako atakuchagulia.
 
Pia hajatuamsha nadhani amewaamsha watu wa huko Kanda ya ziwa sio hapa mjini watu tulibaki tunamuangalia tu alipojifanya yeye ni Simba wa nyika.

Hivi jiulize umewahi kukutana na nyoka pale askari monument posta Dar es salaam??? Kaja mjini hapa tunamcheki tu, akajifanya oooh kama wewe ni mwanaume kweli ndani ya miaka mitano lazima uhame mjini, funny enough akaanza kuhama yeye Mara Dodoma, akajikuta Chato na habari yake ikaishia huko.

Tuheshimiane bana, ukija sehemu ukawakuta wenyeji salimia kwanza. Sasa ukiona wenyewe wanamuangalia tu usijimwambafai ujue kuna balaa linakufuata na hakuna atakayekushika sikio.
 
Ongea kwa herufi kubwa na uwazi nikuelewe. Kaja mara chato mara si utaje jina unaogopa nini wakati mtu mwenyewe ashajiondokea zake? Hivi SGR imejengwa kanda ya ziwa au unajifanya kipofu tu? Je mwendokasi uko kanda ya ziwa? Upanuzi wa uwanja JKNIA nao ni Musoma? Acheni unazi wa kifikra bila sababu za kitaalamu mwanangu.
 
Pombe,

Sasa Nani ametaja Magufuli hapo??? Mie nimetaja jina la Pombe tu nakuchagulia jina la mwanao, hayo mengine sijui akina walwa , utayapeleka kwa babu yako atakuchagulia.
Samahani mwanangu. Sikujua kuwa kumbe nilijaribu kumpigia bata gitaa. Nisamehe. Mea culpa mea culpa.
 
Mitaa yangu hiyo homeboy nimecheza basketball uwanja wa kilakala sec mwaka 2008 Hadi na 2010
Mi nimetokea Kilakala Madizini

Mimi wa Kilakala Madizini mkuu, kizalendo zaidi
 
Acha zako wewe,kwani lazima uwaze kwenye negativity Tu

Lulu
Furaha
neema
Waridi

Haya siyo majina mazuri ya Kiswahili ya kuwapa watoto mkuu? Wenzetu wapo ulaya lkn Wana wanawaita watoto "Dele Ali " " wale" na rotimi

Tuondoe hii dhana ya kila jina la Kiswahili ni Baya na kina mikosi asee!!!

Kimsingi hakuna majina WATU ya KISWAHILI labda useme majina ya KIMILA (kikabila). Hayo uliyotaja Lulu sijui Furaha sijui Neema ni VIELEZI au majina ya VITU vingine.

Niendelee?
 
Naongezea:
Upendo
Imara
Utukufu
Maua
Faraja
Hekima
Kunegunda
Mashauri
Ambangile
Mboka
Mobali
Nk.

Mengi kati ya hayo umetaja si majina ya WATU, bali ni VIELEZI tu au VIVUMISHI sijui [faraja, hekima, mashauri/mashauzi, upendo, utukufu, imara] na majina ya vitu [maua].

Ukisema majina ya kimila (kilugha) hapo sawa, Ambangile, Mboka, Mobali.

Hivyo, hakuna majina ya WATU ya KISWAHILI.
 
Yapo! Labda hujawahi kuyasikia. Furaha, Neema, Amani, nk.; wapo wengi na ni Kiswahili, lugha yetu adhimu. Si kizungu!
Mengi kati ya hayo umetaja si majina ya WATU, bali ni VIELEZI tu au VIVUMISHI sijui [faraja, hekima, mashauri/mashauzi, upendo, utukufu, imara] na majina ya vitu [maua].

Ukisema majina ya kimila (kilugha) hapo sawa, Ambangile, Mboka, Mobali.

Hivyo, hakuna majina ya WATU ya KISWAHILI.
 
Sahizi mtoto ukimuita majina kama Masanja, Mabula, Misoji, Minza, Rhobi na mengineyo mengi unaitwa mchawi pia unaabudu mizimu. Wengine huenda mbali na kudai mizimu ya mababu huwafuata watoto, acha tusonge hivi hivi.
No ujinga,kutokujitambua,na utumwa wa fikra,
 
Kimsingi hakuna majina WATU ya KISWAHILI labda useme majina ya KIMILA (kikabila). Hayo uliyotaja Lulu sijui Furaha sijui Neema ni VIELEZI au majina ya VITU vingine.

Niendelee?
Nimekuelewa Kaka,but the point ni kwamba; siyo lazima jina la Kiswahili liwe Baya km inavyodhaniwa,yaani siyo lazima umwite masumbuko au mateso kusha tuleteane mrejesho kwamba majina ya Kiswahili mabaya

Kuwa kielezi sijui kivumishi Mimi sipo huko,maana unaweza kumpa mtt jina kutokana na Hali mfano "upendo"
Au mtu alichelewa kupata mtt but alipomzaa kutokana na Hali ya furaha anayoifeel akaamua kumwita Lulu au furaha
 
Mengi kati ya hayo umetaja si majina ya WATU, bali ni VIELEZI tu au VIVUMISHI sijui [faraja, hekima, mashauri/mashauzi, upendo, utukufu, imara] na majina ya vitu [maua].

Ukisema majina ya kimila (kilugha) hapo sawa, Ambangile, Mboka, Mobali.

Hivyo, hakuna majina ya WATU ya KISWAHILI.
Labda nikuulize swali mkuu..nini maana ya jina ambangile
 
Back
Top Bottom