Mleta mada ana hoja unalazimika kupinga sababu umeshachemka ila kimsingi huna sababu wala hoja ya msingi
Siwezi kushangaa sana ukisema hivyo.
Kwa sababu Watanzania wengi wamezoea maisha ya kijima, ya kufuatiliana fuatiliana, maisha ambayo mtu haamui mambo yake mwenyee, mambo yanaamuliwa na jamii, maisha ya kuzongana, kuchunguzana, kufuatiliana.
Ni hivi, mtu ana haki ya kuamua anampa mtoto wake jina gani.
Ukianza kumuingilia kwenye hilo, unamuingilia kwenye mambo ya ndani ya familia yake.
Wewe kama hupendi jina fulani, tafuta mtoto wako umpe jina unalolipenda wewe.Na mtu akikuingilia katika hili, hata wewe nitaitetea haki yako hii ya msingi.
Kwa nini uanze kulazimisha mtu baki achague jina unalolipenda wewe na asilolipenda yeye?
Yani mtu katafuta mtoto kivyake, jina umpangie sheria wewe?
Wewe mtu akikupangia jina la kumpa mtoto wako usilolipenda wewe, analolipenda yeye, utaona sawa?
Acheni mambo ya zama za ujima kila kitu kinaamuliwa na kijiji.
Jina la mtoto lisipopitishwa na kikao cha kijiji huwezi kumpa mtptp hilo jina.
Huu ndiyo mwanzo wa kusema wote tupigie kura CCM, kwa sababu mwenyekiti wa kijiji kasema.
Groupthink.
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya groupthink ya aina hii na umasikini.