Panzi Mbishi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2021
- 2,231
- 2,904
Hivi wakristo waliacha kubatiza kwa kubadili jina la asili na kumpa mtoto jina la kizungu?Habari salamu sio ndefu nimechefukwa mtoto wa dada yangu kapewa jina Moana, jina la kikatuni cha Disney nikapata maswali sana, kwanini hadi leo tunaendelea kushikilia majina ya wageni? Majina mazuri ya Kiswahili, lugha za asili yameisha au ndio tunayaona ya kizamani na hayafai kitu?
Kuna uhusiano gani kati ya kuwa Muislamu na kumpa mtoto jina la kiarabu? Au mkristo kumpa mtoto jina la Kizungu kama Frank, Aboubakar, Sameer, Chris, Dorice, Khadija
Kwanini sio majina ya kichina au kihindi? Labda dini ni kitu chema lakini isiondoe u-Afrika wetu. Tujitafakari.
Ni utaratibu wa kizumbukuku sana