Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Habari salamu sio ndefu nimechefukwa mtoto wa dada yangu kapewa jina Moana, jina la kikatuni cha Disney nikapata maswali sana, kwanini hadi leo tunaendelea kushikilia majina ya wageni? Majina mazuri ya Kiswahili, lugha za asili yameisha au ndio tunayaona ya kizamani na hayafai kitu?

Kuna uhusiano gani kati ya kuwa Muislamu na kumpa mtoto jina la kiarabu? Au mkristo kumpa mtoto jina la Kizungu kama Frank, Aboubakar, Sameer, Chris, Dorice, Khadija

Kwanini sio majina ya kichina au kihindi? Labda dini ni kitu chema lakini isiondoe u-Afrika wetu. Tujitafakari.
Kweli mkuu huku tunataka kiswahili kikuwe huku tunaita watoto majina ya kizungu kama ni vikatuni mbona viko Vingi vya kiswahili bora angemwita hata kirikuu, madenge,....ila kuna padri mmoja alikataa kubatiza watoto majina yakizungu hadi ujue maana ya jina halisi tena liwe la kiswahili au la kilugha kiukweli hata majina tumewazidi hadi wenye Nayo/wazungu
 
Tatizo forest hill wewe mchawi una majini mizimu nk kwaiyo nikizaa mtoto nimwite forest hill majini yako na mamizimu yako yataanza msumbua mtoto yakiamini pale ni sehemu salama kwaiyo itabidi tukwite tuanze matambiko nk mtoto akikataa ndio ile galfa anakuwa mwehu ,mara azai mara mlevi

Kuepusha shari ndio maana sasa watoto tunawaita JF yani jamii forum, Fb face book, twitter, instagram, whatsap tuone je ataiga hizo tabia maana katika ukoo wetu hatuna haya majina
Haha
 
Recently nimekutana na mtu anasajili namba ya simu kwa kitambulisho cha NIN kwa jina ka Bandika Bandua Balele
 
Kweli mkuu huku tunataka kiswahili kikuwe huku tunaita watoto majina yakizungu kama ni vikatuni mbona viko Vingi vya kiswahili bora angemwita hata kirikuu,madenge,....ila kuna padri mmoja alikataa kubatiza watoto majina yakizungu hadi ujue maana ya jina halisi tena liwe la kiswahili au la kilugha kiukweli hata majina tumewazidi hadi wenye Nayo/wazungu
Hata kama ningekuwa na mbuzi nisingemuita madenge/kirikuu.
 
Waafrika tulishavurugwa kitambo,ila hili sio jambo la kwanza, Hayati Dikteta Mobutu Sese Seko Kuku Ngwendu wa Zabanga alipiga marufuku majina ya kigeni ndani ya Nchi yake ya Zaire

Ndio tukawapata akina Kabasele ya Mpanya
 
Tatizo forest hill wewe mchawi una majini mizimu nk kwaiyo nikizaa mtoto nimwite forest hill majini yako na mamizimu yako yataanza msumbua mtoto yakiamini pale ni sehemu salama kwaiyo itabidi tukwite tuanze matambiko nk mtoto akikataa ndio ile galfa anakuwa mwehu ,mara azai mara mlevi

Kuepusha shari ndio maana sasa watoto tunawaita JF yani jamii forum, Fb face book, twitter, instagram, whatsap tuone je ataiga hizo tabia maana katika ukoo wetu hatuna haya majina
Majini yanajua jina ? Du kweli waafrika bado tupo gizani.
Majini yana macho na akili ya kibinadamu !!!!!
 
mi katika vitu nilivyokataa mapema ni hili la kuita watoto majina ya kizungu. nilipata uzoefu nilivyotengeneza viatu vyangu vikakamatwa kisa jina langu la kizungu pale hongkong wakasema ni kopi vikataifishwa.
 
Naunga mkono hoja... Maaana hata uislam umesema tuwape watoto wetu majina mazuri... Ila haujasema tuwape ya kiarabu pekee imesema majina mazur tuh.. Afu kingine kila mzazi apangiwi jina we ukiwa na wanao waite utakavyo c hatutokupinga.... Ila majina ya kizaramo mabaya aisee mara sikujua,chausiku,shida,mwakatobe .....kwa hio sometimes ya kizungu na kiarabu ni bora
 
Back
Top Bottom