Antetokounmpo
JF-Expert Member
- Feb 5, 2020
- 1,240
- 2,010
Majina yetu haya ya antentoukmpo hawayapendi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio uungwanaWaafrika tumepoteza dira , angalia mtu anaondoa ngozi yake ya asili ili aonekane Kama mzungu ! Ni uuuuungwana ?
Ndubwi🤣🤣🤣🤣🤣Mkuu ungekubali jina lako lingekuwa KISODA?
au NDUBWI?
Mkuu mbona Povu???Acha zako wewe,kwani lazima uwaze kwenye negativity Tu
Lulu
Furaha
neema
Waridi
Haya siyo majina mazuri ya Kiswahili ya kuwapa watoto mkuu? Wenzetu wapo ulaya lkn Wana wanawaita watoto "Dele Ali " " wale" na rotimi
Tuondoe hii dhana ya kila jina la Kiswahili ni Baya na kina mikosi asee!!!
Au...Wewe c uncle wake muite "Tabu, Shida, Masumbuko na Sikujua au watoto wako wape haya ili ufurahi na roho yako
Mimi nimeita wanangu majina ya kienyejiSiwezi kushangaa sana ukisema hivyo.
Kwa sababu Watanzania wengi wamezoea maisha ya kijima, ya kufuatiliana fuatiliana, maisha ambayo mtu haamui mambo yake mwenyee, mambo yanaamuliwa na jamii, maisha ya kuzongana, kuchunguzana, kufuatiliana.
Ni hivi, mtu ana haki ya kuamua anampa mtoto wake jina gani.
Ukianza kumuingilia kwenye hilo, unamuingilia kwenye mambo ya ndani ya familia yake.
Wewe kama hupendi jina fulani, tafuta mtoto wako umpe jina unalolipenda wewe.Na mtu akikuingilia katika hili, hata wewe nitaitetea haki yako hii ya msingi.
Kwa nini uanze kulazimisha mtu baki achague jina unalolipenda wewe na asilolipenda yeye?
Yani mtu katafuta mtoto kivyake, jina umpangie sheria wewe?
Wewe mtu akikupangia jina la kumpa mtoto wako usilolipenda wewe, analolipenda yeye, utaona sawa?
Acheni mambo ya zama za ujima kila kitu kinaamuliwa na kijiji.
Jina la mtoto lisipopitishwa na kikao cha kijiji huwezi kumpa mtptp hilo jina.
Huu ndiyo mwanzo wa kusema wote tupigie kura CCM, kwa sababu mwenyekiti wa kijiji kasema.
Groupthink.
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya groupthink ya aina hii na umasikini.
Wanyakyusa hatunaga shobo na uzunguKuna fahari na raha kubwa kufurahia asili yako. Hujisikiii mnyonge na huwezi kujidharau hata ukidharauliwa na yeyote. Mimi ni Mnyakyusa kamili na majina yangu yote ni ya Kinyakyusa, yaani Gwandumi Gwappo (Gwapponile) Atufwene Mwakatobe Mwakimenya. Asili yangu ni Mwakaleli, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya
Nawasikitikia ambao asili ya majina yao imepotea kabisa. Mathalani Abdul Salmin Amour Juma, Victor Robert Willy Henry au Longinus Lawrence Recocatus Deogratius.
Nasikia zamani wakoloni walikuwa wanakataa waafrika kubatizwa au kuandikishwa shuleni kwa majina yetu ya asili. Tumerithi hata visivyo riziki!
BoraSasa wameacha, labda upende mwenyewe au wazazi. Bahati mbaya majina mengi tunawapa watoto wasiokuwa na maamuzi au uwezo wa kuhoji chochote
Usifikiri matatizo yako wote tunayoMwita hapa kutoka mara
Mtu mrefu ajabu.
Jina la kiyahudi naitwa solomon.
Hakuna mwafrika mwenye jina moja katika zama hizi za kubatizana
Tushatishwa bila ubatizo na kuzaliwa upya huendi mbinguni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tatizo si jina tatizo ni kwamba tunapenda watu wafate mawazo yetu na si furaha zao.
Yeye akimuita moana,frank, charity na wa kwako ukamwita ndondocha, chungu, tabibu halafu wote mkakaa kimya bila kuzodoana itapendeza.
Hivi ile lodge ya mlimani cottage Bei gani ?Nimekulia mitaa Ile,,mtaa unaitwa mlimani cottage
Sijawahi kuuliza mkuu,Kama upo serious nitauliza kwa wadauHivi ile lodge ya mlimani cottage Bei gani ?
Wewe mfuasi wa shetani.majina yote ni ya dini kuu mbili.uislamu na ukristo.sasa uafrika wako upo wapi?wahindi wanaabudu ngombe,wachina wanaabudu jua.isitoshe kama unao watoto wape majina unayoyataka.mmoja mwite mavi,mwingine mkojo,Ngombe,Kondoo,pakan.k. Upo huru.Sasa nimeelewa kwa nini makampuni ya simu yalipandisha gharama za Internet.mijitu inaandika upuuzi tu.Habari salamu sio ndefu nimechefukwa mtoto wa dada yangu kapewa jina Moana, jina la kikatuni cha Disney nikapata maswali sana, kwanini hadi leo tunaendelea kushikilia majina ya wageni? Majina mazuri ya Kiswahili, lugha za asili yameisha au ndio tunayaona ya kizamani na hayafai kitu?
Kuna uhusiano gani kati ya kuwa Muislamu na kumpa mtoto jina la kiarabu? Au mkristo kumpa mtoto jina la Kizungu kama Frank, Aboubakar, Sameer, Chris, Dorice, Khadija
Kwanini sio majina ya kichina au kihindi? Labda dini ni kitu chema lakini isiondoe u-Afrika wetu. Tujitafakari.
Umeamua kuandika matusi na hukuelewa nilichoandika,nimekusameheWewe mfuasi wa shetani.majina yote ni ya dini kuu mbili.uislamu na ukristo.sasa uafrika wako upo wapi?wahindi wanaabudu ngombe,wachina wanaabudu jua.isitoshe kama unao watoto wape majina unayoyataka.mmoja mwite mavi,mwingine mkojo,Ngombe,Kondoo,pakan.k. Upo huru.Sasa nimeelewa kwa nini makampuni ya simu yalipandisha gharama za Internet.mijitu inaandika upuuzi tu.
Kwenye mizimu inaweza kuwa na ukweli mkubwa!Sahizi mtoto ukimuita majina kama masanja, mabula, misoji, minza, rhobi na mengineyo mengi unaitwa mchawi pia unaabudu mizimu. Wengine huenda mbali na kudai mizimu ya mababu huwafuata watoto, acha tusonge hivi hivi.