Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

Kukimbiza mwenge si utamaduni wa asili wa Mtanganyika. Tumeiga, licha ya kukimbizwa miaka yote hiyo (Kwa Imani ya kwamba unaleta maendeleo na faraja) lakini bado changamoto lukuki ziko ndani ya nchi yetu. Kwa mfano:
  1. Umaskini bado mkubwa.
  2. Mauaji ya watu ni makubwa
  3. Ufisadi ndiyo balaa
  4. Ujinga unazidi kutamalaki. Mfano, kuuziwa maji ya upako(au kitambaa) Kwa Imani ya kumpatia ahueni ya maisha mnunuaji.
Zama ambazo sayansi na technology imekuwa ndiyo msingi wa maendeleo, lakini Tanzania bado watu wanauabudu mwenge (eti unaleta maendeleo 😂😂😂). Lol
Utamaduni wa asili wa Mtanganyika ni upi? Unaujua?
 
Soma Biblia ndugu yangu acha uzembe:
Kutoka 3:2
“Malaika wa Bwana akamtokea katika mwali wa moto kutoka katikati ya kijiti. Akaangalia, na tazama, lile kijiti lilikuwa linawaka moto, lakini halikuteketea.
Nipe andiko linalosema tuwashe Mwenge/ mienge
 
Mpaka utakaponionesha kwenye Amri kumi za Mungu imeandikwa tusiwashe mwenge nitakuja kukuletea maandiko mengi sana. Je, amri ya ngapi imesema tusiwashe Mwenge?
Kuna amri na makatazo ni vitu viwili tofauti
 
Sipati picha kila mwaka Serikali inatenga bajeti ya kukimbizana na moto nchi nzima wakati nchi ni masikini.
 
acha imani za kishirikina mkuu
Nani alikuwambia hiyo ni Imani ya kishirikina? Na kitabu kipi kimesema hiyo ni imani ya kishirikina? Au upo too emotional? 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Sipati picha kila mwaka Serikali inatenga bajeti ya kukimbizana na moto nchi nzima wakati nchi ni masikini.
Kawaida sana. Nchi zingine kama India, China na Ulaya zipo na siku za kuwasha mshumaa.
 
Japan - Mbio za Mwenge wa Olimpiki: Mwenge wa Olimpiki hukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya nchi mwenyeji kwa kipindi cha takriban miezi mitatu.
 
Duniani hakuna jipya kila kitu ni kilekile mambo ni ku recycle tu
We acha kujibu vitu usivyojua bwana..unadhani Marekani wana Muda wa ukimbizana na Moshi?hakuna cha recycle wala nini nilikuwa namzingua tu huyu much know ila alivyojibu tu nikajua hakuna anachoelewa
 
Kukimbiza mwenge si utamaduni wa asili wa Mtanganyika. Tumeiga, licha ya kukimbizwa miaka yote hiyo (Kwa Imani ya kwamba unaleta maendeleo na faraja) lakini bado changamoto lukuki ziko ndani ya nchi yetu. Kwa mfano:
  1. Umaskini bado mkubwa.
  2. Mauaji ya watu ni makubwa
  3. Ufisadi ndiyo balaa
  4. Ujinga unazidi kutamalaki. Mfano, kuuziwa maji ya upako(au kitambaa) Kwa Imani ya kumpatia ahueni ya maisha mnunuaji.
Zama ambazo sayansi na technology imekuwa ndiyo msingi wa maendeleo, lakini Tanzania bado watu wanauabudu mwenge (eti unaleta maendeleo 😂😂😂). Lol
Hapo kwenye kuleta maendeleo hata mimi pananiacha mdomo wazi sana😅😅
 
We acha kujibu vitu usivyojua bwana..unadhani Marekani wana Muda wa ukimbizana na Moshi?hakuna cha recycle wala nini nilikuwa namzingua tu huyu much know ila alivyojibu tu nikajua hakuna anachoelewa
Kwani sie wamarekani,,,unataka ya wamarekani nenda marekani.....kila mtawala na mipaka yake na taratibu zake,,,kama unaona hazikufai sepa tu
 
Ishara kumi na mbili za dunia zimeunganishwa katika makundi manne (Moto, Ardhi, Hewa na Maji)
Kwakuwa tunataka tuijue nchi yetu zaidi kwa leo sitaongelea kwa undani zaidi hizo ishara Kumi na Mbili na makundi yote hayo manne, bali leo nitaongelea pekee kuhusu Moto

Kuwasha mwenge kunaweza kuashiria mwanga, mwangaza wa kiroho, na uongozi

Kuleta Mwanga kwa Mambo ya Siri
: Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha kuangaza mambo ambayo hayajulikani au kuleta uwazi katika hali fulani. Inaweza kuashiria kipindi ambacho ukweli uliokuwa umefichika au siri zinafichuliwa.

Uongozi na Hekima: Mwenge mara nyingi huonekana kama ishara ya hekima au maarifa ya kiroho. Unaweza kumaanisha kuwa na mwongozo wakati wa kipindi cha giza au kuchanganyikiwa, kama vile jukumu la mwalimu au kiongozi wa kiroho.

Mabadiliko na Mwanzo Mpya: Mioto, kwa asili yake, inahusishwa na kipengele cha moto, ambacho ni kipengele cha mabadiliko katika unajimu. Kuwasha mwenge kunaweza kumaanisha mwanzo wa hatua mpya, hasa ile inayohitaji kuachilia mambo ya zamani ili kutoa nafasi kwa mapya.

Kuamka Kiroho: Katika muktadha wa kiroho, kuwasha mwenge kunaweza kuashiria kuamka au kupanuka kwa ufahamu wa mtu. Ni kuhusu kuwa na ufahamu zaidi wa tabaka za ndani za maisha na nafsi.

Taifa lisilokuwa na Utamaduni na Mila zake hilo ni Taifa mfu.

Nitaendelea kueleza zaidi.
 
Na yale makafara ya milimani yananeemesha Taifa??
 
Kafara inahusika na kuchinja wanyama. Kitu ambacho hakihusiani na kuchinja wanyama siyo kafara
Umechemka mzee 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom