Kuwatetea Watanzania inahitaji kidogo uwe na tatizo la Kisaikolojia

Kuwatetea Watanzania inahitaji kidogo uwe na tatizo la Kisaikolojia

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Moja ya mambo niliyojifunza kwa muda mfupi kuhusu utetezi wa Haki ni pamoja na uhusiano wa Haki na Saikolojia. Na hapo ndipo nikakuta mifano halisi katika jamii yetu.

Nitakupa mifano kadhaa;

1. Huwezi tetea haki za Waumini wa Manabii wa upako ambao unahisi au unajua wanatapeliwa pesa zao wakati wao wenyewe wanaona sawa. Na wameridhika na wanatoa ushirikiano.
Kisaikolojia wewe ndiye mwenye matatizo sio wale. Kuwaona wanatatizo ni jambo zuri na ni akili pia. Ila kuwapigania si ishara nzuri. Ni dalili kuwa unatatizo la kisaikolojia.

2. Huwezi tetea Haki za wanawake kwamba wasitembee uchi wakati wao huona wakitembea uchi na kukaa uchi ndio wamependeza na ndio wanafurahia hali hiyo. Hilo tunaita unatatizo la kisaikolojia.

3. Huwezi tetea Haki za watanzania wanyonge ambao kwaakili yako unaona wanaonewa, wanaumizwa, wanabagazwa lakini wao wenyewe hawana habari, wanafurahia maisha yao na wanaungana na Wale unaona wanawatesa. Tatizo halipo kwao tatizo lipo Kwako.
Usijesema watanzania ni waoga Nope! sio kweli! Nimefuatilia kwa umakini Mkubwa nimegundua kuwa watanzania sio waoga ila wanapenda Hali walizo nazo, wameridhika nazo.

Watanzania ukitaka kujua wanapenda hali zao. Jifanya unawatetea ndio utaelewa kile ninachokisema. Kwanza watakuona mjuaji, unakiherehere na unawakera.

Maisha ya Watanzania unayoyaona ni Culture yao. Ndio utamaduni wao waliouzoea na kuukubali.

Ndio maana ukiangalia kuanzia katika ngazi ya familia chini kabisa hakuna utofauti mkubwa na ngazi ya kitaifa.
Yaani ukifuatilia life style ya mtu mmojammoja katika familia yake. Vile unavyoiona serikali ndivyo familia nyingi za kitanzania zilivyo.

Kama ulikuwa hujui, kwa Watanzania ni Culture;

I) Dhulma na uonevu ni utamaduni
Mkubwa anaruhusa ya kumwonea au kumdhulumu mdogo. Hiyo ni culture. Sio ajabu mzazi kumdhulumu mtoto. Na jamii inaona ni sawa. Utaambiwa ni mzazi wako.

Au Mume kumdhulumu Mke. Kumwonea na kumfanyia ukatili. Hiyo kwa jamii yetu ni Culture. Mzazi kisa amekuzaa anaweza akakutandika nusu kukuua kwa kosa la kuulizia jambo la haki.

2) Mkubwa Hakosei.
Watu wanailaumu serikali kutotaka kukosolewa lakini yenyewe ukiyakuta nyumbani ndio yanafanya yaleyale.
Wewe kama hukosei kwa mtoto uliyemzaa na huna jeshi lolote. Serikali yenye jeshi ndio inakosea?
Mume hataki kuambiwa ukweli na mkewe.
Mama/ baba hataki ukweli kutoka kwa watoto.
So ni jambo la utamaduni.

Hao viongozi wenyewe wa Dini wanakuambia usimnyoshee mtumishi wa Mungu kidole. Kuna wakati niliwahi eleza hili. Kuwa mtumishi wa Mungu ni mtu yeyote anayefanya kazi yoyote halali kwa njia ya maadili na yenye ufanisi.

3. Mkubwa Anaheshimiwa kuliko Mdogo.
Huo ni utamaduni. Yaani ni utamaduni wa kijinga kwa sababu hauna qualifications za tija na matendo ya uadilifu.
Badala yake ungetakiwa uwe hivi; Heshima ya mtu ipo kwenye matendo yake. Hii ni culture ya watu wenye akili na hekima.
Kumaanisha kuwa mzazi sio kigezo cha heshima. Bali matendo yako mema ya uadilifu ndio iwe kipimo cha heshima alafu uzazi iwe sifa ya ziada. Kwa sababu kila mtu ni mzazi.
Viongozi wa nchi wanatakiwa kuheshimiwa na kuchaguliwa kulingana na matendo yao.
Lakini utamaduni wetu ni tofauti. Mkubwa yeyote hata liwe Jizi, liuaji, libakaji, au sifa mbaya sehemu kubwa ya jamii ikiwemo dini zitampa heshima

4. Kuthamini wageni Kuliko wenyeji.
Usiishangae serikali na kuipa lawama kwa baadhi ya watumishi na viongozi kuthamini wageni kuliko wenyeji wa nchi hizi.
Tembelea nyumba za watanzania ukiwa mgeni. Wengi wao watakukaribisha na kukuthamini kwa heshima kubwa kuliko hata walivyofanya kwa watoto wao au mke/mume wake kwa mwaka mzima.
Huo ni utamaduni mbaya.
Kutaka kuwafurahisha watu wengine kuliko watu wa familia yako

Kwamba mwaka mzima usipike chakula kizuri mpaka siku mgeni aje. Huo ni utamaduni wa kijinga ambao unatakiwa kukoma.

Kwa Watibeli, Mgeni hawezi kupewa heshima kuliko mwenyeji.
Hatuwezi kujiandaa kukufurahisha mgeni kwa gharama za jasho la wanafamilia ambao mwaka mzima wameteseka na hawajapata chakula kizuri. Never ever.

Kuwatetea Watanzania kwenye idara za haki kwa hali wanazozichukulia kama utamaduni ni kupoteza muda wako na kuonyesha unatatizo la Kisaikolojia.

Mimi acha nipumzike sasa!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umechukua akaunti namba? Fundraising ni leo, na wa Tanzania hawajakaa na mtu kukubalina awatetee, ni viherehere tu na kujipendekeza
 
Back
Top Bottom