Kuwatumia "Mafundi" badala ya Wahandisi kwenye Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule ni dharau

Kuwatumia "Mafundi" badala ya Wahandisi kwenye Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule ni dharau

Hapo itakuwa kutowatendea haki. Kwa nini kuishia kwa wahandisi?

Wanasiasa waliotutawala kwa miaka 60 leo wameifanyia nini nchi hii?
Yaani unatoa elimu kwa watu ambao baadae huwaamini!
 
Hapo itakuwa kutowatendea haki. Kwa nini kuishia kwa wahandisi?

Wanasiasa waliotutawala kwa miaka 60 leo wameifanyia nini nchi hii?
Wahandisi wajitetee kivyao na sio kwa vigezo mfanano, hali kadhalika hao wanapopo nao pia kivyao
 
Hongera kwa kukusanya TOZO ya dhuluma, mnataka kujenga vituo vya Afya ambavyo "vilianza kujengwa" tangu enzi za JK....sina tatizo!

Tatizo langu ni lile sharti kwamba "Ujenzi" ufanywe na wale mafundi wetu a.k.a Fundi Maikoz kwa kisingizio cha kupunguza gharama...

Hii si bahati mbaya:

"Hawa Vijana wetu, Kaka na Dada zetu wana kampuni za Ujenzi, wana taaluma husika, wanalipa kodi, wameajiri.....Leo hutaki kuwatumia then at the same time unataka Makampuni yao yalipe Kodi na Wao waendelee kulipa mikopo ya Bodi ya Elimu...."

Kila kitu nchi hii ni siasa. CCM imekuwa ikiwekeza kwa wajinga ikiwabana vilivyo wenye uelewa au afueni yoyote katika maisha:

Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho

Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho

Hiyo ndiyo siri ya kudumu kwao madarakani.

"Hao kina Maiko na vibarua wao ndiyo wapiga kura wetu."
 
Tatizo ni kuwa Watanzania waaina ya Alu api, Makonde, Wabaya na Kherini Mstaafu wa uvvccm ndio wanaoongoza maprofesa na kupanga nani atoke jalalani na nani abaki kwenye jalala la pugu.

Ilipaswa iwe hivi labda nikusaidie kidogo .
Local fundi asipewe tenda yoyote bila kuwa na msimamizi mwenye Taaluma ya Ukandarasi wa majengo.
Yaani maombi yake yaambatanishwe na proposal ya mtaalamu wa majengo.

Hii iwe kila sekta.
Hata Duka lenye thamani ya zaidi ya milioni 50 liwe na mtaalam wa fani ya uhasibu kwa ajili ya ushauri kama ilivyo mawakili.
Hali kadhalika Magereji, yasisajiliwe bila kuwa na mshauri aliyesomea Fani hiyo.
Yaani wakiomba leseni lazima barua zao zipitishwe na wenye fani hizo kama ilivyo kwa mawakili.

Mbona kwa mawakili na maduka ya Dawa na hospitali imewezekana lakini kwa wale wa fani ya biashara na fedha na mainjinia inashindikana ?
 
Force account haimzuii engineer kuomba kazi,kuna tofauti ya engineer na mkandarasi,mkandarasi siyo engineer, force account inahitajika muombaji aoneshe veti vya chuo alicho Soma na uzoefu wa kujenga majengo ya serikali,fundi mangungo mfumo wa force account hauwezi ukampa kazi hana pesa kulipa vibarua kwa kuwa unafanya kazi Kama kutumia mkandarasi,yaani fundi anatakiwa atumie gharama zake kulipa vibarua kwa kila hatua ya ujenzi na anakaguliwa then ndio analipwa,ma engineer wanaweza kuomba kazi Ila watalipwa pesa ya ufundi tu,ambapo ni asilimia 25 ya gharama zote za ujenzi,
 
yaani kitu akifanya mama hata km kilikuwepo before Lazima muweke nongwa
 
mfumo wetu wa elimu ni wa hovyo ambao muasisi wake ni CCM.
Ninahisi hii ndio sababu kubwa ya kutowapa wahandisi kazi.

Serikali inajua ubovu wa elimu wanayotoa na udhaifu wa wahitimu(kiutendaji).
Ndio maana wameamua kuwapa hao wa kujifunza veta ambao ni wawajibikaji na wana nidhamu ya kazi.
 
Mbona mlikuwa kimya wakati jiwe yupo hai?
Mlinyamaza na kuacha mambo yaende holela basi tulieni watoto wetu watakuja kufukua makaburi kupima bongo zetu
 
Force Account ni kaa la moto for those who are so called Engineers

Kujenga majengo yote kwenye ngazi ya jamii nq has chini ya serikali za kienyeji (Local Government) kuanzia madarasa, zahanati, maabara, vituo vya afya nyumba za watumishi n.k Engeneer hawezi kutoboa kwa local fundi yaani yule alietoka veta mwenye walau maujuzi yake ya muda mrefu ya kujenga locally

Hawa MaEngeneer gharama zao utadhani wapo wanafanya miradi ya wafadhiri ndio maana hata serikali inawapotezea tu.

Wajitathimini!!!
 
Nafikir iko hivo kwenye ujenzi! Nitasahihishwa!

Kwenye miradi ya Force Account, lazima kuna mtaalam wa ujenzi! Ambaye ndo anakuwa Msimamizi wa Mradi (Project Supervisor). Pamoja na kuwepo Local Fundi lkn kunawepo na engineer ambaye anatoa technical konw how ya Mradi!

Aidha, miradi hii ina kamati mbili
1. Kamati ya ufundi (technical team)
2. Kamati ya mapokezi!

Kwenye kamati ya Technical ndo unakuta kuna engineer (msimamizi wa Mradi) na Technician wale wa Halmashauri/ au taasisi husika! Huyu engineer ndo mshauri Mkuu na local fundi watalazima kuzingatia ushauri wake. Hata mradi unapofungwa na kukabidhiwa maelezo ya msingi ya Mradi yanatolewa na Msimamizi wa Mradi ambaye ni engineer/Technician.

So shortly hao wakandarasi wapo, kosa ni kwamba tu wamenyimwa tenda! Kwa sababu hata kwenye ujenzi wa tender za kikandarasi, hao ma-engineer hawajengi hutumia hawa hawa Local Fundi. Afu wao hubaki kutoa tu ushauri wa kitaalam.
 
Point nzuri sana lakini hawa ni Wasimamizi sio Wajenzi. Pia sio sahihi kusema kuwa "pesa itarudi kwenye jamii" kwani Wakandarasi wao wanaishi jamii IPI?
Hapa brother kuna ramani, ukiwa mhandis basi unasimamia maswala ya msingi wa nyumba(foundation mafundi huita) ramani kila kitu ili usije pishana na(BOQ Bill of quantities), ukishamaliza hayo unajikuta mafundi wanashambua kuta balaa kona kwakona, shule za mzee lowasa za kata nchi zima tulijenga kwa njia hiyo mzee
 
Eti fundi Maiko ndio ajenge zahanati na vituo afya duuuu kisa save pesa...aibu
 
Ukijua Mazingira ambayo Force Account inatumika utaelewa kwanini waziri kasema watumie hiyo njia
 
Naamini hawajapewa hio nafasi ila kama wepewa nafasi na wakashindwa basi mfumo wetu wa elimu ni wa hovyo ambao muasisi wake ni CCM. Kwahio tuchague moja kati ya hayo mawili
hizo Ni excuses, elimu yetu imepitwa na wakati na haitufai hata kidogo.
 
Vijana ambao ni wahandisi wajitathmini. Pamoja na elimu zao lazima wawe wajasiriamali na ku-fit kwenye systems zetu. Hawa wasomi ndo kwa miaka mingi badala ya kujenga majengo yakaonekana wao ni kuleta siasa nyingi zisizo na maana. Mafundi wa kawaida diploma kushuka chini wanafanya vitu vinaonekana ndo maana hawakosi kazi.

Kama fundi ana uzoefu apewe tu kazi. Ma-injinia mkiendelea kuleta mambo ya shuleni huku field mtalia sana njaa.
 
Back
Top Bottom