Kuwatumia "Mafundi" badala ya Wahandisi kwenye Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule ni dharau

Unajua maana ya forced account?
 
Mkuu,
ukiona serikali inawadharau wasomi ujue........Mimi nimeshangaa sana....
 
Huko halmashauri watakuwa na wahandisi watawatumia hao......serikali iko sahihi kukamilisha hii miradi haraka iwezekanavyo kukwepa upigaji wa michakato na serikali kuishia kupata aibu......
 
Mafundi wa kawaida wanaonekana ni wa hivyo na hawafai kuwapa kazi bila ya msimamizi mkuu, lakini ukweli hao mafundi ndio wanatujengea nyumba zetu kila leo tunaoishi na hazijawahi kuharibika.

Ndugu mleta mada umewawakosea sana mafundi, sio kila fundi ni fundi maiko.
 
Huu ujinga aliuanzisha Magufuli na wanauendeleza. Ukweli ni kwamba force account ni ya hovyo na inayumbishwa uchumi wa nchi kwa kupunguza ajira za wahitimu wengi. Ukweli tumekosa viongozi tumebaki na wababaishaji
 
Hebu soma maandiko yangu yote
3. ujenzi utumie force account na sio mkandarasi...
hapa ndio mada yako ilipolalia. kumbe kutumia force account ina jumuisha pia kutumia fundi juma as one of the options. Sasa hiki ndicho upingacho. Lkn kumbuka force account ilikua inatumika before. Ndio nkasema kanya anye kuku.....
 
Napingana na wewe, nawapongeza kutoa kazi kwa fundi maiko kama ulivyosema, CRB wamekosea sana kuweka SHARTI kupata leseni lazima mwanahisa awe INJINIA.

Nilitaka kufungua kampuni ya ujenzi ila nilishindwa kufungua kwa kigezo mwanahisa awe INJINIA,kwanini wanalazimisha? Kwanini msiweke kigezo lazima kuajiri INJINIA tu na kazi iendelee?
 
Wewe kwanza hiyo force Account sio kwamba haitumii wahandisi, Halmashauri zina wahandisi na Techncians ndio wanasimamia masuala ya kitaalamu .

Hapo imani iliyopo ni kwamba wakandarasi wana gharama kubwa na usumbufu mwingi wa kwenye makaratasi kuliko kufanya Kazi.
 
Ni kwasababu hakuna watu wa health and safety at work, kufanya ukaguzi na kupitisha majengo.
Wapo na wanafanya hiyo Kazi na wanahakikisha usalama mahala pa Kazi,acha upotoshaji ..huu utaratibu umetumiwa miaka 5 iliyopita mbona hamkuwa mnaropoka kama saizi?
 
Hadi unaenda kufungua kampuni hukujua kwamba kuna kodi? Acheni ujinga.

Hata hivyo Serikali imeamua kuongeza fedha kwenye barabarani kwa hiyo wakandarasi waende huko Kazi ni nyingi sana na hao wahandisi hawatoshi.

Mkoani kwangu Tarura pekee kuna yenda 53 bado Tanroads na Ruwasa.

Pia kwenye ujenzi wa Makao Makuu pale Dom serikali imesema itatumia wote private sector na public kama Tba nk
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Force account inaokoa fedha nyingi kuliko kutumia Mkandarasi.

Lakini kitaalamu, mradi wowote wa Ujenzi unakuwa na muda wa matazamio ambapo ikitokea kuna dosali yeyote ndani ya kipindi cha ungalizi (Defect liability period) cha miezi 6 hadi Mwaka Mkandarasi atakuja site kufanya marekebisho hayo kwa gharama zake.

Huku kwenye force account inakuwa ni tofauti, hakuna defect liability period na ikitokea faults yeyote hakuna anayewajibika ndiyo tunapata hasara hapo kama Nchi pamoja na Kodi zetu kutumika.

Kuna haja Serikali ikawakumbuka Wakandarasi, wamepoteza mitaji sana kipindi cha 2016 - 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…