Kuwatumia "Mafundi" badala ya Wahandisi kwenye Ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule ni dharau

Serikali inasomesha Wataalam, wanapata ujunzi na hata kuanzisha kampuni za ujenzi lakini Serikali inaona gharama kuwatumia au kuwapa kazi. Fani za Wataalam hao inaelekea si kwa mahitaji ya Fedha za Serikali labda Wanasomeshwa kwa mahitaji ya Sekta Binafsi na nje ya nchi. Inafika mahali fundi wa kawaida anamwajiri fundi msomi na kuanza kumsimamia kwa sababu yeye ndiye anayeingia Mkataba na Serikali.
 
M
Halmashauri zina wahandis hivyo watasimamia zoezi
Tuliwaona hao wahandisi wakitungua vilio wakionyeshwa jengo lililojengwa chini ya kiwango ohh Niko peke yangu majengo mengi siwezi kuwa site muda wote ohh nikiomba gari kunipeleka site nanyimwa nk jiandaeni kilio

Halafu Nani ataidhinisha kuwa Hilo jengo limejengwa viwango? Segregation of duties iko wapi? Kwa hiyo halmashauri ndio watakuwa architect,wahandisi na quantity surveyor wenyewe na waidhinisha malipo wenyewe Halmashauri? Kuna tatizo mwisho wa siku

Jengo la umma si Sawa na Nyumba yake binafsi Ummy Mwalimu ujenzi wake
 
Ulichokiandika ni sahihi kabisa.BUT ukumbuke serikali ni ya wote mkuu,kwa uelewa wangu wapo mafundi wazuri sana huko mitaani ambao wanafanya kazi kwa weledi mkubwa sana hata kama zipo changamoto na risks mbalimbali kama ulivyosema lakini utakubaliana na me kuwa hata hao wakandalasi unaowapigia debe kuwatumia nao ni risk pia.Hapa najifunza serikali ku-take risk katika kugawana keki ya Taifa
 
Shukrani Kaka, sina tatizo ila ni kuweka "ulazima" ingeachwa ikawa huru, unaonaje?
 
Mpwaaaa
 
Sawa sikatai,utakubaliana na me kuwa uhuru unapotolewa then mwenye nguvu atapewa fursa na mnyonge ndo atapotezwa mazima.Ninasema hivyo kwasababu nipo huku mikoani na kupitia mpango huo wa serikali wa kuwatumia mafundi then watu wamefauru hata kufungua vimigahawa na kuanzisha hata ufugaji wa kuku na nguruwe,hali ilikuwa ngumu sana kwa mnyonge huku chini kupata cash hivi.Hii issue isikie tu kwenye redio mbao but nikuthibitishie mkuu hii hela imeenda kugusa maisha ya mtu aliyejikatia tamaa
Shukrani Kaka, sina tatizo ila ni kuweka "ulazima" ingeachwa ikawa huru, unaonaje?
 
Ujinga ambayo serikali wanalijua na hawataki kulisemea ni kua; ujenzi kwa kutumia force account inaumiza sana wasimamizi kutoka halmashauri kwani tenda ya vifaa vyote vya ujenzi zinachukuliwa na mabosi wao.

Wanapoleta vifaa vya chini ya kiwango wanalazimisha zipokelewe na zitumike mwisho wa mchezo ni wale wasimamizi ndiyo wanasimamishwa kazi na kupewa adhabu pale tatizo inapotokea.

Yetu macho
 
Mbona simple tu, hao wenye kampuni nao waombe kama mafundi mchundo maana kinachobadilika hapo ni mfumo wa manunuzi tu.

Kutumika mkandarasi maana yake gharama za vifaa na ufundi ni juu yake, lakini force account maana yake vifaa vinanunuliwa yeye analipwa ya ujenzi kwa kusomamiwa na mhandisi wa Halmashauri ambaye amesoma hivyo vyuo ulivyotaja.

Sasa kwanini wengi wanaojiita wakandarasi huwa hawaombi kazi ya ufundi? Kwani wamekatazwa? Waombe wakiwa na reasonable price watachukuliwa.

Tuache kulalamika. Specifications za ujenzi ni zile zile hata utumie contractor au fundi mchundo bado ratio za cement, specifications za bati, mbao, Mchanga, kokoto, misumari, rangi etc ni zile zile kwa kutumia ramani husika.

Mfumo wa force account aliuhamasisha sana JPM kwa kuona unaokoa gharama na majengo yanakuwa kwenye standards. Lakini pia yapo majengo mengi tu yaliyojengwa na makandarasi na ni mabovu mno.
 
Mpwa umeongea kwa uchungu sana sana sana. Siku hizi unaongea points tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…