SAGAI,
Nadhani tuangalie mienendo ya wanamuziki wetu na jinsi wanavyojipatia kipato kupitia umaarufu na umaarufu huo wanaupataje?
Mara nyingi umaarufu wa wanamuziki wa nchi hii unapatikana kutokana na mabifu.
Hadija Kopa Vs Nasma Khamis.
Msondo Vs Sikinde
Vijana Jazz Vs Bima Lee
TOT Plus Vs Twanga Pepeta
Ali Kiba Vs Diamond
Nk nk nk.
Ukiangalia vizuri ni kama Diamond kafuata upepo wa mafanikio ya Yanga ya miaka 2 hii ili kutengeneza fedha, lakini akaegemea kwenye bifu la Manara na Barbara (Simba) ili apate mapokezi Makubwa toka Yanga akijua baada ya tukio lile atazoa subscribers wengi toka mashabiki wa Yanga na akaunti itatuna. Yaani mashabiki wake wa siku zote ukiunganisha na wapya wa kutoka Yanga watakaofuata mkubwa, kipato hakitakuwa haba. Na naamini alifanikiwa.
Baada ya kuona hivyo Kiba naye akatafuta Nitoke vipi ili apokelewe Simba. Kama zali tamasha la Simba ambalo miaka ya nyuma lilifana Kwa kutumia mafanikio ya uwanjani ya msimu husika mwaka huu kigezo hicho kikakosekana kikabaki kigezo cha Utambulisho wa Wachezaji pekee. Ndipo Kwa ubunifu mkubwa Ahmed Ally akaibuka na Kibegi. Kibegi kikawa Kibegi na tena kikatengenezewa Version. Kikawa na version I, II na III ambayo Kiba aliibuliwa from no where. Kwa vile ni Msanii akaibuka na Wimbo àmbao ulipambwa Sana na Wanasimba ili kunogesha tukio wengine wakidiriki kusema ndio wimbo Bora wa Simba hivyo ufanywe wimbo rasmi wa timu (Team anthem). Lakini ukisikiliza wimbo wenyewe na rithym ya kawaida ya Simba Simba vinakwenda tofauti. Hata baadhi ya maneno yaliyomo kama vile Simba ndiyo timu No.1 Afrika hayaakisi uhalisia.
Kwa maoni yangu nakubaliana na wewe kwamba kuhamisha muziki bila tahadhari na kuupeleka kwenye soka letu kutakuwa na athari chanya na hasi na ni dhahiri hasi itazidi chanya.
Ukiangalia kwenye siasa kama uwanja wa kufanya siasa Tanzania ungekuwa level, hawa wanamuziki usinhewaona wote wakiwa CCM. Huko wamekwenda kulinda vitumbua vyao wakihofiwa kupigwa rungu na serikali wakionekana upande wa pili au kuwa neutral. Utakumbuka Diamond alitaka kulinda hadhi yake Kwa kubaki neutral kisiasa akapelekewa TRA na akaangushiwa bill ya Kodi bil.4?
Nimalizie Kwa kusema viongozi wenyewe wa timu wanapaswa kuchukua tahadhari za makusudi kulinda Kwa wivu hadhi ya soka isitekwe na kitu kitakachofubaza radha yake.