Kuwatumia vibaya Diamond na Ali Kiba kwenye siasa za Simba na Yanga ''kutaua" soka la Tanzania

Kuwatumia vibaya Diamond na Ali Kiba kwenye siasa za Simba na Yanga ''kutaua" soka la Tanzania

SAGAI,
Nadhani tuangalie mienendo ya wanamuziki wetu na jinsi wanavyojipatia kipato kupitia umaarufu na umaarufu huo wanaupataje?
Mara nyingi umaarufu wa wanamuziki wa nchi hii unapatikana kutokana na mabifu.

Hadija Kopa Vs Nasma Khamis.
Msondo Vs Sikinde
Vijana Jazz Vs Bima Lee
TOT Plus Vs Twanga Pepeta
Ali Kiba Vs Diamond
Nk nk nk.

Ukiangalia vizuri ni kama Diamond kafuata upepo wa mafanikio ya Yanga ya miaka 2 hii ili kutengeneza fedha, lakini akaegemea kwenye bifu la Manara na Barbara (Simba) ili apate mapokezi Makubwa toka Yanga akijua baada ya tukio lile atazoa subscribers wengi toka mashabiki wa Yanga na akaunti itatuna. Yaani mashabiki wake wa siku zote ukiunganisha na wapya wa kutoka Yanga watakaofuata mkubwa, kipato hakitakuwa haba. Na naamini alifanikiwa.

Baada ya kuona hivyo Kiba naye akatafuta Nitoke vipi ili apokelewe Simba. Kama zali tamasha la Simba ambalo miaka ya nyuma lilifana Kwa kutumia mafanikio ya uwanjani ya msimu husika mwaka huu kigezo hicho kikakosekana kikabaki kigezo cha Utambulisho wa Wachezaji pekee. Ndipo Kwa ubunifu mkubwa Ahmed Ally akaibuka na Kibegi. Kibegi kikawa Kibegi na tena kikatengenezewa Version. Kikawa na version I, II na III ambayo Kiba aliibuliwa from no where. Kwa vile ni Msanii akaibuka na Wimbo àmbao ulipambwa Sana na Wanasimba ili kunogesha tukio wengine wakidiriki kusema ndio wimbo Bora wa Simba hivyo ufanywe wimbo rasmi wa timu (Team anthem). Lakini ukisikiliza wimbo wenyewe na rithym ya kawaida ya Simba Simba vinakwenda tofauti. Hata baadhi ya maneno yaliyomo kama vile Simba ndiyo timu No.1 Afrika hayaakisi uhalisia.

Kwa maoni yangu nakubaliana na wewe kwamba kuhamisha muziki bila tahadhari na kuupeleka kwenye soka letu kutakuwa na athari chanya na hasi na ni dhahiri hasi itazidi chanya.
Ukiangalia kwenye siasa kama uwanja wa kufanya siasa Tanzania ungekuwa level, hawa wanamuziki usinhewaona wote wakiwa CCM. Huko wamekwenda kulinda vitumbua vyao wakihofiwa kupigwa rungu na serikali wakionekana upande wa pili au kuwa neutral. Utakumbuka Diamond alitaka kulinda hadhi yake Kwa kubaki neutral kisiasa akapelekewa TRA na akaangushiwa bill ya Kodi bil.4?

Nimalizie Kwa kusema viongozi wenyewe wa timu wanapaswa kuchukua tahadhari za makusudi kulinda Kwa wivu hadhi ya soka isitekwe na kitu kitakachofubaza radha yake.
Swadakta!!!!!!
 
sasa .ni wadogo hao mkuu?.bila.promo.bila.instagram bila.kiba bila.diamond? Usisahau pia.sasa hivi population ime. Double
Usi.kubalie na vtakwimu vyake vya kihuni. Yaani Kirumba uchukue watazamaji 17k na Nyamagana unachukua wangapi?
 
Unapobisha uwe na takwimu siyo kumpinga Mtu ionekane wewe wa kisasa wakati yeye ni wa zamani na Wa kisasa pia maana nyakati zote mbili alikuwepo. Una Taarifa Mechi ya Simba Vs Pamba ilikuwa inajaza uwanja wa CCM Kirumba bila promo na watu wengi wanabaki nje kama walioko ndani? Je, uwanja wa Kirumba u achukua watu 8000 kama ulivyosema? Unajua mwaka 1990 Tanzania ilikuwa na watu wangapi na Sasa inao wangapi?
Wapi nimeandika Kirumba inachukua watu 8000!? Kirumba kujaza siyo issue maana hata lake Tanganyika Kigoma inajaza kwa mechi ya mashujaa tu na hakuna promo yoyote!
Msimamo wangu ni uleule, Mpira wetu umebadilika sana zama hizi tofauti na zamani.
 
Usi.kubalie na vtakwimu vyake vya kihuni. Yaani Kirumba uchukue watazamaji 17k na Nyamagana unachukua wangapi?
Tafuta taarifa kutoka vyanza unavyoviamini then uje kupinga. Kirumba inachukua watazamani waliokaa 17k tu.
 
Hawa viongozi wa Sasa wa Simba na Tanga wengi wapi Kwa kutafuta umaarufu na kufata maslahi ndio maana wanaweza kujitapa kuchukua mtu Toka Tanga au Simba bila kujali madhara yake baadae.
Kwa diamond ni wazi hakuwa mshabiki ila akienda kufata umaarufu lakini Ali Kina sio tu ni mshabiki lakini amecheza mpira mpaka Kuna kipindi alisajiliwa Coastal ingawa alicheza mechi Moja au mbili kiukweli hawezi kuhamia Simba Bali alifata maslahi.
Kitu kingine wasichoelewa ni wao ndio wanawapromoti wasanii na sio wasanii wanaopromoti vilabu Kwa sababu hakuna ukumbi wanaoweza kupiga wakajaza watu elfu 60
 
Wapi nimeandika Kirumba inachukua watu 8000!? Kirumba kujaza siyo issue maana hata lake Tanganyika Kigoma inajaza kwa mechi ya mashujaa tu na hakuna promo yoyote!
Msimamo wangu ni uleule, Mpira wetu umebadilika sana zama hizi tofauti na zamani.
Tatizo hawataki kukubali, hao ndio utasikia wanakuambia "mpira zamani bwana sio sasa" ila ukimuambia akutajie hiyo zamani tulipata mafanikio gani ataanza blah blah za kina Gagalino sijui matakataka gani huko...
 
Kadri miaka inavyozidi kwenda Tasnia ya Michezo na Burudani hapa Bongo inazidi kukosa wapenzi mashabiki.
Tupe ushahidi, mimi ninachojua kwa sasa mpira wetu umepata wapenzi wengi na umekuwa kuliko kipindi chochote kile tangu dunia imeumbwa.
 
Kwa majukwaa yapi? Labda kdg kwa sasa angalau, tena baada ya kujenga jukwaa kubwa lkn kwa zamani ilikuwa haiingizi hata 20k.
Zamani walikua hawauzi tiketi kwa idadi maalum, mpaka mechi inaendelea huku bado walikua wakiuza.
Kuna mechi moja ya derby nilijuta kupoteza muda wangu na pesa yangu na ukizingatia Chama langu lilifungwa, basi uchungu juu ya uchungu.
Walijaza watu mpaka kwenye tartan (sehemu inayotumiwa na wanariadha), kazi yangu ilikua kuhama kambi tu ili nione mpira lakini wapi unaona nusu kiwanja au pungufu ya hapo.
Na hapo tumewapa njagu kitu kidogo wakatutafutie tiketi, bila hivyo tungepata tiketi wakati mpira umeshaisha, na hilo foleni lake la kuingia uwanjani ni balaa.
 
Nakulikuwa hakuna cha promo wala nini
 
Back
Top Bottom