Pesanyingi
JF-Expert Member
- Apr 15, 2023
- 1,157
- 1,983
Serikali kupitia mamlaka husika hasa mipango miji, ingepunguza au kuweka idadi kamili ya wakazi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Dar es Salaam watu wamerundikana sehemu moja kuanzia makazi hadi vyombo vya usafiri.
Sasa kwa nia njema kwanini kusiwe na mpango wa ku zuwia ongezeko la idadi ya watu kuhamia Dar na badala yake wapelekwe maeneo mengine kwani nchi yetu ni kubwa kijografia.
Hii itasaidia hata wakati wa majanga iwe rahisi maeneo mengi kufikika kwaajili ya kutoa msaada kwa haraka na kuokoa maisha ya watu na mali zao.
Watu waende kama ni kwaajili ya shughuli za biashara na kuondoka na si kujenga makazi.
Wakazi wa Dar karibuni Tandaimba, Handeni, Kasulu, Biharamulo, Nachingwea, Newala, Same na maeneo mengine.
Maisha bila kukimbilia na kujazana Dar es Salaam yanawezekana.