Na hiyo ingekuwa si tatizo kama watu wanaokuja Dar wangekuwa productive, kama kungekuwa kuna viwanda wanafanyia kazi, kama wangekuwa wamejiingiza katika digital/information economy wanafanya kazi kwenye mitandao na kuingiza fedha nchini.
Lakini, hata hao wanaokija Dar wengi wao ni Wamachinga na wabangaizaji tu.
Yani hata mtu akitaka kujiingiza kwenye uchumi wa mitandaoni, serikali imedhibiti hata njia za kumlipa ni tatizo. Watanzania inawabidi wawalipe Wakenya ili kutumia Paypal accounts za Kenya, wengine wanalipa as much as 30% ili kuweza kulipwa Paypal. Hii ni kodi inawafanya Wakenya wafaidi bila kufanya lolote.
Yani serikali si tu haisaidii wananchi kujijenga kiuchumi, hata pale wananchi wanapojiongeza wenyewe bila kusaidiwa na serikali, serikali inawazibia wasiendelee.