Kuwe na mkakati maalumu wa kupunguza idadi ya Wakazi katika mkoa wa Dar es Salaam

Kuwe na mkakati maalumu wa kupunguza idadi ya Wakazi katika mkoa wa Dar es Salaam

Tanga na Mtwara zinasikitisha sana. Zina kila kitu mpaka bandari, lakini ujinga wetu tu ndiyo unazuia maendeleo.

Kuna nchi kama Rwanda hazina bandari zinatamani sana zingekuwa baharini lakini hazina uwezo huo.
Kweli kabisa.
YAani haiingii akilini meli inatoka Asia na Ulaya, inavuka bandari ya Tanga inakuja kushusha mzigo Dar es salaam.
Viwanda vya katani wakua vyote, viwanda vya kusindika Maziwa wakaua vyote, Chungwa linaozea shambani muheza.
Africa na waafrica tunashida kubwa hata shetani asilaumiwe.
 
Dar itaendelea kufurika siku hadi siku mpaka siku tutakayotengeneza balance upande wa Miundombinu, Huduma za kijamii na Shughuli za kiuchumi, Ni juzi tu hapa watu wametenga Billion 500 kwa ajili ya Miundombinu ya Dar Pekee na bado kuna miladi ya uboreshaji majiji nao wamo kitu ambacho sio kibaya, Shida inakuja uwiano na Mikoa Mingine hauna balance sasa hapo ambae hapendi kutembea kwenye barabara nzuli ni nani, Huduma bora za afya, Elimu bora kwa maana ya vyuo vikuu, Shughuli za kiuchumi n.k
 
Nilisema population Tanzania ni ticking timebomb.

Tanzania ina average annual population increase ya 3%.

Na hapa hujaona kitu, population ya Dar inaenda ku double in the next 10 years.

Ila kuna watu ukiwaambia habari za uzazi wa mpango unagombana nao.

Wanasema Tanzania ni nchi kubwa inahitaji watu.
Mji wa Tokyo una watu milioni 36, sawa na mara 9 ya population ya wakazi wa daresalaam
 
Mikoa kama Tanga, Tabora , Lindi na Mtwara , ina ardhi kubwa lkn serikali imeitelekeza, wenyeji wake wote wamejazana Dar.
Mkoa wa Tanga ukiangalia yale magofu ya viwanda unaweza ukalia.
Unaijua dhana inaitwa survive of the fittest?.. variable ya kugawa maendeleo ni viwanda sana. Maeneo ya viwanda yanakua kwa kasi sana asikudanganye mtu yoyote. Pwani ukiiingalia kibaha, chanika, kisemvule zinakuwa si mchezo
 
Jenga angalau Hekta 2000 ya Kilimo cha Umwagiliaji kwa kila Kata (inayolimika) ya nchi hii na kulimwe Mazao kutokana na Mazingira na Mahitaji husika then watu watapungua Dar...
Dar inavutia watu lwa vitu vingi, kuna sehem huko hata lifti hupati mpaka unakufa. Kila mtu anapenda kuonekana wa kisasa
 
Serikali kupitia mamlaka husika hasa mipango miji, ingepunguza au kuweka idadi kamili ya wakazi katika mkoa wa Dar es Salaam.

Dar es Salaam watu wamerundikana sehemu moja kuanzia makazi hadi vyombo vya usafiri.

Sasa kwa nia njema kwanini kusiwe na mpango wa ku zuwia ongezeko la idadi ya watu kuhamia Dar na badala yake wapelekwe maeneo mengine kwani nchi yetu ni kubwa kijografia.

Hii itasaidia hata wakati wa majanga iwe rahisi maeneo mengi kufikika kwaajili ya kutoa msaada kwa haraka na kuokoa maisha ya watu na mali zao.

Watu waende kama ni kwaajili ya shughuli za biashara na kuondoka na si kujenga makazi.

Wakazi wa Dar karibuni Tandaimba, Handeni, Kasulu, Biharamulo, Nachingwea, Newala, Same na maeneo mengine.

Maisha bila kukimbilia na kujazana Dar es Salaam yanawezekana.
Mkuu kuwa serious basi... Yaani mtu atoke Dar ahamie Tandahimba au Nachingwea? au Nangurukuru?
Sasa huko kuna biashara gani wakati hata biashara za makanisa zinalipa zaidi miji mikubwa hasa Dar!
Wanahamishiwa Dodoma taratibu...


Cc: Mahondaw
 
Miji hii inakufa sababu ya rural-urban migration. Dar inakua kubwa kwa kuuwa miji mingi sana tanzania
Na hiyo ingekuwa si tatizo kama watu wanaokuja Dar wangekuwa productive, kama kungekuwa kuna viwanda wanafanyia kazi, kama wangekuwa wamejiingiza katika digital/information economy wanafanya kazi kwenye mitandao na kuingiza fedha nchini.

Lakini, hata hao wanaokija Dar wengi wao ni Wamachinga na wabangaizaji tu.

Yani hata mtu akitaka kujiingiza kwenye uchumi wa mitandaoni, serikali imedhibiti hata njia za kumlipa ni tatizo. Watanzania inawabidi wawalipe Wakenya ili kutumia Paypal accounts za Kenya, wengine wanalipa as much as 30% ili kuweza kulipwa Paypal. Hii ni kodi inawafanya Wakenya wafaidi bila kufanya lolote.

Yani serikali si tu haisaidii wananchi kujijenga kiuchumi, hata pale wananchi wanapojiongeza wenyewe bila kusaidiwa na serikali, serikali inawazibia wasiendelee.
 
Nilisema population Tanzania ni ticking timebomb.

Tanzania ina average annual population increase ya 3%.

Na hapa hujaona kitu, population ya Dar inaenda ku double in the next 10 years.

Ila kuna watu ukiwaambia habari za uzazi wa mpango unagombana nao.

Wanasema Tanzania ni nchi kubwa inahitaji watu.
Serikali itengeneze mazingira rafiki mkoa wa pwani ili mji utanuke... kwa kiasi flani wamefanikiwa kwa kata ya mapinga.. ipo bagamoyo lakini ina vibe ya dar.. hata hivyo dar bado sana kuna miji kama kinshassa au cairo ina population za mil 20 huko
 
Back
Top Bottom