Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Haya mambo YA status waachieni wanawake.
Wanawake huwa wanatumia status kuchambana na show offf za kijinga

Mimi binafsi status sijawahi kuweka na sina muda wa kuangalia status ya mtu

Watu wamekuwa watumwa kwenye mitandao. Vitu wanvyovitafuta kwenye hizo posts au status ni likes, followers, views, comments kutoka kwa watu.

Wengine wanapokosa hivyo vitu wanaanza kujiona hawana thamani au hawapendwi (inferiority) na depression inaanza. Huu ni utumwa ambao umejificha

Mtu anapost halafu kila wakati anatembelea post yake kuona kuna likes ngapi au je watu wanacomment? Au anapost kutafuta attention ili aongeze followers. Huu ni utumwa
 
Si utu uzima ,Wala ushamba au chochote!Ni maamuzi tu. Mfano Mimi siweki kabisa status,kwa sababu naziona irrelevant,hazina maana.Hivyo tu.
 
We sema tu kuwa hupendi kuweka status..!! Sasa usichokipenda usitutake tukusaidie kukichukia..!!
 
Sio kuweka ila kuna wale wanaoweka kama mipasho na kuchamba watu, so hapo akili ndogo utaijua tu
 
Mimi siweki sana status, naweza kukaa hata miezi sita sijaweka, sio nataka kuonekana matured huwa naona tu uvivu, halafu huwa nahisi kama nikiweka najichoresha tu lakini za watu naangalia na kuzifurahia.
 
Kwamba mtu smart ni yule anaeweka mistari ya bibilia na picha za Yesu?
 
Kwangu status ni sehemu ya kuwachanganya watu wasiyajue maisha yangu halisi japo sivimbi wala kufanya showoffs ila ninachopost kwa mtu anaetarajia kujua maisha yangu basi ataniona ni mtu wa hali ya chini sana mda mwingine post zangu zinatoa fundisho kwakua hata akionyesha ulicho nacho haibadili kitu chochote zaidi utajiletea marafiki wasio na tija maishani. status zangu zimenifanya niwe na marafiki wachache wasio thamini vitu ambao ni wakweli na wako makini[emoji41]
 
Kuna wale daily wanaweka status kama mataruma ya reli… sifungui unless uwe unawekaga memes.
Naomba nieleweshe nitajuaje mtu akiangalia status yangu
 
Sio anatumia gb watsup ana view lakini wewe huoni
 
Mimi siweki sana status, naweza kukaa hata miezi sita sijaweka, sio nataka kuonekana matured huwa naona tu uvivu, halafu huwa nahisi kama nikiweka najichoresha tu lakini za watu naangalia na kuzifurahia.
Tumefanana akili

Tofauti yetu ni moja tu mimi nime hide view kwahyo nikiziangalia hawajui kama nimeangalia halafu siangalii zote naangalia zile za wapenda kupost meme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…