Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Kuweka au Kutokuweka WhatsApp status: Kuna uhusiano na mtu kuwa smart, msomi au tajiri?

Sijajua mtoa mada amezungmzia usmart katika nyanja zipi. Wapo watu wanapost status hata 5 kwa siku lakini wakiwa kazini wanachapa kazi vizuri sana na wanaendesha maisha yao vizuri mnoo.

Wengine hawana cha kuweka status kwa hiyo wanaonekana "machuadi".
 
Tumefanana akili

Tofauti yetu ni moja tu mimi nime hide view kwahyo nikiziangalia hawajui kama nimeangalia halafu siangalii zote naangalia zile za wapenda kupost meme
Hawa watu wana mashabiki wengi akina meme lords mimi nishawajua wa kwangu naenda kuchek memes chap,

kuna binadamu wengine wanaweka boring status kichizi
 
Kuna wale daily wanaweka status kama mataruma ya reli… sifungui unless uwe unawekaga memes.
Ku views status ya mtu hadi nitake mwenyewe[emoji16]
IMG_20220929_231200.jpg
 
Akili ya mtu haipimwi kwa clip ya sekunde thelathini
Mkuu ujinga kwenye akili ya mtu ni sehemu ya burudani ukiwa fatilia watu kama hao huwa wengi ni wabinafsi sana halafu wahuni wa chini chini
Furaha ni kuwa na marafiki but whatsapp sio wajinga kuweka privacy option

Narudia akili haipimwi kwa clip ya sekunde thelathini
 
Zamani nilikua naweka ila toka mwaka 2021 December niliamua kuacha hata birthday yangu sikujipost kokote kwa mara ya kwanza. Nilijiuliza why naweka status yani kwanini najipost kila mara then unabaki kuhangaika kila saa kuangalia nani kaview unawaza mbona flani hajaview nikaona kama ni kaujinga flani hivi ka kitumwa.

Nimegundua sio lazima wala haina umuhimu ni kutafuta validation tu za watu waseme umependeza mara sijui hiyo nguo nzuri wtf nikaacha nika archive picha zote insta kifupi nimetoka ulimwengu wa kuweka mapicha yangu mtandaoni nimeona haina maana wala haina faida.

Ambao wanaweka biashara ni sawa lakini wanaboa mtu anaweka picha 50 ni ukosefu wa akili hamna mtu wa kuview mapicha yote hayo labda kama hana cha kufanya weka picha tatu na bei hata kila siku. Ndo mana wengi hawauzi sababu mtu akiona mnyororo hafungui.

Siku ya mwisho kila mtu anafanya anachoona sawa[emoji3578]
 
Suala la kuweka status inategemeana na mtu mwenyewe, ila kwa mtazamo wangu naona kama mtu anaweka zile status zinazoelimisha jamii sio mbaya.

asilimia kubwa ya comments zimeonesha kama kuweka status ni ujinga, kitu ambacho kama watu wote watakuwa na mtazamo huo basi ile maana ya upashanaji, uhabarishaji, kuelimishana na kuburudishana kutakuwa hakuna maana.
 
Mimi sio mwekaji status, hadi marafiki zangu hua wananiulizaga kwamba "wewe vp aisee, jaribu kueka status hata mara moja moja ili tujue kwamba bado upo hujafa kuliko kukaa kimya hatujui unaendeleaje".

Basi nkawa naweka atleast kwa mwezi mara moja moja pia If it was upto me ningestick na ile old version ya WhatsApp kwamba just kutuma na kupokea text, voicenote and videocalls.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wale daily wanaweka status kama mataruma ya reli… sifungui unless uwe unawekaga memes.
Nifungue macho jmn,hakyanani hili neno memes nalisikia kula Mara lkn cjui nini maana yake,msicheke jamaa
 
Kama wewe unapost kila jambo unalokutana nalo mtandaoni au lako binafsi Mimi huwa naona huyo mtu sio smart na rough Sana kwenye maisha yake. Mtu mzima na akili zake kila siku kupost vichekesho na mapicha anayokutana nayo mitandaoni .... Mtu anayepost biashara kutwa nzima huyo Yuko smart maana it's opportunity kuonyesha wateja wake vitu alivyonavyo
 
Kuna mtu humu nina namba zake huu mwaka unaenda wa pili, ila hata siku moja sijawahi muona akiweka status ama akiview zangu.

Siku nyingine naweka naset aone yeye mwenyewe lakini zitamaliza masaa 24 sioni akiview

Watu wa hivyo wana shida gani? Ni utu uzima au ndio wako busy hawana muda na status??

Bado nawashangaaa aisee
Ila depal jamanii kah[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kuna kasumba naona imezidi kushamili kuwa mtu aliweka status kwenye simu ni mtu ambaye sio smart maana mwanaume au mwanamke mwenye heshima zake humkuti na mambo ayo ya status kwenye simu au kuwa online mara kwa mara au pia kuwepo kwenye magroup. Je, hili lina uhalisia wowote?
Ni tabia tu ya mtu tu mimi sina michongo ya kuniweka bize na wala sina stimu ya kuweka status au kupost post mitandaoni ndani ya mwaka naweza kupost mara mbili au tatu tu
 
Back
Top Bottom