Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Kwa kifupi Shabiby kasema watu wanapiga dili katika uagizaji, watu wanakula mkwanja wakutosha na ni watu wachache…wasiojali wananchi…

Serikali inauwezo wakudhibiti na kupunguza makali kwa njia mbadala lakini ndio vile…
 
Kwa nini kuandikia mate? Shabiby anaahidi bei kupungua chini ya 50%?

Kwanini asipewe nafasi kama Masudi Kipanya ku prove gari lake la umeme?

brazaj hamna chochote huyu Mh ni mjanja mjanja tu. Huu ushauri wake utaingiza serikali chaka. Yaangaliwe mapungu kwenye bulk procument yarekebishwe na serikali itoe ruzuku kwenye mafuta. Kwani serikali inashindwa nini kufanya bulk procument kutoka kwenye hizo meli zilizo huko deep sea zinazotafuta wateja?
 
Anakuwa je mpigaji kupendekeza msingi wa kupunguza bei kufikia 50%?

Kama huo ni upigaji kwa hakika huo ndiyo tunaoutaka!
Unautaka na nani?
CHADEMA siyo wazalendo kabisa.
 
brazaj hamna chochote huyu Mh ni mjanja mjanja tu. Huu ushauri wake utaingiza serikali chaka. Yaangaliwe mapungu kwenye bulk procument yarekebishwe na serikali itoe ruzuku kwenye mafuta. Kwani serikali inashindwa nini kufanya bulk procument kutoka kwenye hizo meli zilizo huko deep sea zinazotafuta wateja?

Mchawi mpe mwana alee taabu iko wapi?

Mfanye Shabiby kinara akashushe bei hata 40% tu.

Shida iko wapi ndugu?
 
Mchawi mpe mwana alee taabu iko wapi?

Mfanye Shabiby kinara akashushe bei hata 40% tu.

Shida iko wapi ndugu?

Hakuna kitu kama hicho kwa bepari. Akijitahidi atapunguza tushilingi kadhaa basi. Nini ambacho Mh Shabibu anaweza kufanya ambacho serikali haiwezi? Serikali wafanye ambacho Mh Shabibu atakifanya kupunguza bei ya mafuta.
 
Unautaka na nani?
CHADEMA siyo wazalendo kabisa.

Wewe hutaki bei kupungua? Tunataka sisi tunaopinga uhuni na kuhitaji bei kupungua.

Kama bei inapungua na shetani ndiye kafanya hilo nini taabu?

Kama bei zinapanda na mpandishaji ni malaika.

Malaika huyo basi hatumtaki aende kuongoza wenziwe huko.

Hatutaki wahuni hapa. Uhuni ni kutupandishia bei na kukataa juhudi zozote za bei kushuka kwa jina lolote.

Habari ndiyo hiyo.
 
Hakuna kitu kama hicho kwa bepari. Akijitahidi atapunguza tushilingi kadhaa basi. Nini ambacho Mh Shabibu anaweza kufanya ambacho serikali haiwezi? Serikali wafanye ambacho Mh Shabibu atakifanya kupunguza bei ya mafuta.

Kwanini hamtaki kumpa nafasi kufanya hilo?

Kwanini kuandikia mate?
 
Shabiby anaongea point, katika yote watakayoongea mwisho wake sisi tunataka kuona mafuta yamepungua bei ifikie ile wakati magufuri yupo 1600-200/l
kabisa mkuu. Kikubwa wananchi tunataka bei ya mafuta ishuke .
Eti wanasema walifanya hivyo ili kudhibiti standards za mafuta. Watanzania sisi habari za viwango hatunaga. Sisi tunataka vitu bei ishuke .
Kwani serikali hii ya CCM lini imeanza kuwapa wananchi vitu vilivyopo Katika viwango vya ubora ?
Huduma za afya mbovu
Elimu ya hovyo.
Barabara mbovu .
Eti Leo wanajifanya kuwajari wananchi kwenye viwango vya mafuta !!!!!!.😂😂😂😂
 
Wewe hutaki bei kupungua? Tunataka sisi tunaopinga uhuni na kuhitaji bei kupungua.

Kama bei inapungua na shetani ndiye kafanya hilo nini taabu?

Kama bei zinapanda na mpandishaji ni malaika.

Malaika huyo basi hatumtaki aende kuongoza wenziwe huko.

Hatutaki wahuni hapa. Uhuni ni kutupandishia bei na kukataa juhudi zozote za bei kushuka kwa jina lolote.

Habari ndiyo hiyo.
Bei zishuke lakini kwa kufuata sheria na taratibu.

Hatutaki serikali ikose chanzo cha mapato, matokeo yake deni la taifa lina skyrocket.

Tanzania itajengwa na Watanzania, serikali ikusanye kodi na kuzuia ama kupunguza ukwepaji.
 
Mh Shabibu angekuwa mkweli angetoa sababu zilizo ifanya serikali ikaamua kwenda kwenye bulk procument ambazo hazipo sasa. Lakini angeonesha jinsi mapato ya serikali yalivyo pungua baada ya kuhamia bulk procument. Hii blabla za kusema flow meter imekufa mara nyingi hazitusaidii.
 
Bei zishuke lakini kwa kufuata sheria na taratibu.

Hatutaki serikali ikose chanzo cha mapato, matokeo yake deni la taifa lina skyrocket.

Tanzania itajengwa na Watanzania, serikali ikusanye kodi na kuzuia ama kupunguza ukwepaji.

Mapato ya serikali? Kama hata huko nako shida watashauriwa cha kufanya.

Tuungane kukataa wahuni.
 
Mapato ya serikali? Kama hata huko nako shida watashauriwa cha kufanya.

Tuungane kukataa wahuni.
Kwahiyo kama CHADEMA mngekuwa madarakani mngeruhusu waingize kiholela?
 
Kufikisha bei 3,000/- kwa Lita waona halali hata kama linaweza kuepukwa?

Mimi ni muumini wa serikali kutoa ruzuku ili bei ishuke. Ama itafute njia nyengine ambayo si ya uagizaji holela kama atakavyo Mh Shabibu itakayo fanya bei ishuke. Khalafu Mh huyu asivyo na huruma anatishia kuwa serikali itakosa mishahara,sijui madawa hii yote nikupinga ruzuku kwenye mafuta na kuhalalisha uagizaji holela.

Unaitetea kodi isitolewa kama ruzuku ili ukaipige na kujinuafaisha kwenye uagizaji holela.
 
Back
Top Bottom