Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Brother,Kwanini Shabiby asipewe rungu bei zianguke 50%. Kwanini kukaa kubishana badala ya kumpa mtu nafasi akafanya mambo?
Brother,
Hapa ni rahisi tu. Kwenye gharama mbalimbali za mafuta kuna vitu ni constant/fixed, na kuna vitu ni variable.
Mfano wauzaji mbalimbali wanaweza kua na bei tofauti, au pia wasafirishaji nao wanaweza kua na bei tofauti pia kwa kila ujazo fulani. Lakini yakifika hapa Tanzania gharama za hapa ni constant kwa kila lita. Yaan TBS, TRA, Ewura, TPA, etc hatutaokoa chochote.
Sasa kama Shabiby anaweza kushusha kwa 50% means atacheza kwenye Muuzaji au Msafirishaji au wote wawili. Anaweza kua sahihi kama tu kuna uzembe unafanyika kwenye ku bargain bei ya hivi vitu viwili. Yaani Inawezekana hawa wanaoagiza mzigo mkubwa (Say 100mil litres kwenye mfano wangu wa awali) wanashindwa ku negotiate bei nzuri then akienda yeye na 10mil litres zake wamsikilize.
Au tuje pale pale kua yeye anaweza kupata ya bei rahisi zaidi bila kujali ubora wake tofauti na Wale wa Bulk ambao wanaweza kua too much selective kwenye ubora.
Hapa wanao negotiate bei ndo wanatupiwa lawama,Kwa kifupi Shabiby kasema watu wanapiga dili katika uagizaji, watu wanakula mkwanja wakutosha na ni watu wachache…wasiojali wananchi…
Serikali inauwezo wakudhibiti na kupunguza makali kwa njia mbadala lakini ndio vile…
Mkuu,Mafuta yanauzwa sehemu nyingi duniani,sio lazima wote muende kununua sehemu moja.
Suala la ubora ni la TBS, wafanye kazi yao ya ukaguzi sawasawa.
🤔🤔🤔🤔🤔 kweli bongo tunanyonywa. Sasa kama wanatumia bei average mbona tunashuhudiaga hapa , bei ya soko la mafuta ikipanda duniani huko na sisi huku muda huo huo Ewura wanapandisha bei. Lakini bei ya duniani ikishuka Ewura huwa hawashushi muda huo huo huku wakitoa sababu kuwa mziko ulioko stock ni mkubwa kwa hiyo hawawezi kuuuza kwa bei ya chini . kwanini napo wasitumie bei ya average?Mkuu,
Labda kwa sasa ni kweli tuna mafuta ya kutumia siku hizo 27, lakini huko nje yamepanda bei tumeagiza kwa bei kubwa. Yaani kwenye costing ya mafuta hua wanatumia average pricing na sio kila mzigo na cost yake. Average means bei ya yaliyoko na bei ya yanayokuja.
Usipofanya hivyo utajikuta yaliyoko umeuza sawa kwa bei "nafuu" lakini ulichopata hakikuwezeshi wewe kulipia mzigo mpya uliopanda bei.
Mkuu,
TBS ikague yakifika hapa au yakiwa huko kabla ya kununua? TBS ina utendaji fulani usioeleweka kidogo, hata juzi Mama kashauri iache kukagua magari yanayokuja kutokea nje yapimiwe huko huko yalikotoka.
Pengine Kwa bulk purchase ni rahisi TBS ku monitor mzigo mmoja kuliko kua na wauzaji wengi
Hakuna bidhaa unaweza kuicontrol price yake kama huizalishi na wewe kwa kiasi kikubwa consumer tu.... Dunia haitutegemei kwa chochote il kwa kiasi kikubwa mpaka sasa tunaitegemea sana dunia watu wetu waweze kuishi..... Tuache ubwanyenye na kulialia, tuhimizane kuchapa kazi na kuweza kujifanyia mambo mengi either kwa kuwa na mitaji au technolojia..
Leo hii tunalialia bei ya mafuta wakati huko baharini tuna gas yakutosha, yapo maeneo kibao yameonyesha dalili za kuwa na mafuta, pale Songea kuna Uranium, kule Mbeya kuna helium...Ziwa Nyasa kuna mafuta pale live..Tuna mabwawa na mito kila mahala..
Tuache kulialia, Kizazi hiki na kingine kijitoa mhanga kuleta heshima, watu wafanye kazi na wafie huko kwenye kazi kuijenga Tanzania, Taifa halijengwi kwa watu kulialia na comedians, Taifa linajengwa kwa ushupavu na kujitolea kwa muda mrefu..
Leo hii mnataka mafuta ya bei rahisi wakati yanachimbwa na wengine huko vidume, mnataka urahisi wa maisha wakati nyie ni consumers tu, Mnajivunia rasilimari wakati hamuonyeshi dalili zozote za kuichakata zaidi ya kutegemea watu walete mitaji na akili zao...
Shida ya Africa na Tanzania ni watu wake wengi kuwa legelege na kuwaza maisha mazuri huku hakuna aliyeyaandaa zaidi ya siasa na ujinga ujinga tu..
Mnataka mafuta yashuke bei?, hata serikali leo hii ikitoa kodi zote kwenye mafuta bado tutaona ni gharama tu na tutataka wanaotuletea watupe bure maana tunapenda burebure.....Ukiwa masikini duniani utaonewa, utadharaulika, utadhulumiwa na kila aina ya uhuni utafanyiwa..... Russia yule asingekuwa strong leo angeshapotea, lakini babu zao akina Stalin na Lenin walipiga kazi kwelikweli na kulifia Taifa na hatimaye wakaleta vizazi strong kama akina Putin, Lavrov, Abrahamovic nk..
mbona utaratibu simple tu . kila mtu anapeleka makadilio ya mzigo anaotaka kuuagiza kwa Ewura.Hapa wanao negotiate bei ndo wanatupiwa lawama,
Kwamba sababu mafuta yote yanapitia kwao basi watakachokubali wao ndio "final". Shabiby anasema kila mtu akienda ku negotiate bei akaagiza kivyake bei zitashuka.
Yaani kama Mnunuzi wa reja reja anapewa bei nzuri kuliko Mnunuzi wa jumla basi liko tatizo mahali.
😂😂😂😂 jamaa kaandika ugoro . anasema huwezi kuicontrol bei ya vitu usiyoizalisha . tumuulize mbona Tanzania hapa viwanda vya mafuta ya kula ni vingi , lakini bei ya mafuta serikali imeshindwa kuimudu? ,vifaa vya ujenzi je,.Umeandika pumba tupu, umekurupuka au uwezo wako wa akili ni duni sana.
Bei ya Bidhaa ni hesabu za numbers au figures. Kwamba unaweka mchanganuo wa gharama mbalimbali kuanzia Manunuzi na usafirishaji (CIF) kisha zile tozo mbalimbali za hapa nchini.
Kama tunakubaliana kua mahali pekee ambapo Shabiby anaweza kucheza napo kupunguza bei ni kwenye CIF basi angalau angeweka hata mfano CIF iliyopo sasa na labda yeye angeweza kuyapata kwa kiasi gani.
Yaani angetuwekea mfano wa numbers tunapoweza kuja mpaka kwenye 50% price tungeweza kumuelewa zaidi.
Mfano bei ya sasa ni Approx. TZS 2,800/Ltr minimum (Bei ya Dar), 50% yake ni TZS 1,400/Ltr. Tozo na Kodi zote tu ni labda TZS 1,000/Ltr, je wapi tunaweza kupata kwa CIF TZS 400/Ltr?
Shabiby anatakiwa atuaminishe hiyo 50% anayoisemea. Otherwise labda awe hakufanya utafiti wa hiyo number. Yanawezekana kushuka kweli, ila kwenye 50% kunahitaji ufafanuzi wa numbers.Shabiby hana haja ya kufanya hivyo, ni kupotezeana muda tu. Serikali haijui kufanya biashara wala haina uwezo huo, iache sekta binafsi ifanye biashara kwa uhuru wote.
Shabiby anatakiwa atuaminishe hiyo 50% anayoisemea. Otherwise labda awe hakufanya utafiti wa hiyo number. Yanawezekana kushuka kweli, ila kwenye 50% kunahitaji ufafanuzi wa numbers.
Pia Shabiby ni Mwanasiasa na Mfanyabiashara hivyo Inawezekana kwenye kauli zake Kuna Lugha za ki biashara na kisiasa pia.
kwanza utambue kuwa kuanzia Ewura , TRA, TBS, nk . wote hao kamwe hawapendi na hawafurahii bei ya Lita ya mafuta ishuke . kwa sababu wao wanapata chao kwa kutumia % . sasa mfanyabiashara A akapeleka bei ya chini aliyonunulia , ambayo kwa kawaida ataenda kuuza chini pia . linganisha na mfanyabiashara B yeye akaagiza kwa bei kubwa ambapo pia atakwenda kuuza kwa bei kubwa pia. Tusidanganyane hapa hizo taasisi na mamlaka zitampenda huyu wa bei kubwa course wanapata% kubwa na wao.Bei ya Bidhaa ni hesabu za numbers au figures. Kwamba unaweka mchanganuo wa gharama mbalimbali kuanzia Manunuzi na usafirishaji (CIF) kisha zile tozo mbalimbali za hapa nchini.
Kama tunakubaliana kua mahali pekee ambapo Shabiby anaweza kucheza napo kupunguza bei ni kwenye CIF basi angalau angeweka hata mfano CIF iliyopo sasa na labda yeye angeweza kuyapata kwa kiasi gani.
Yaani angetuwekea mfano wa numbers tunapoweza kuja mpaka kwenye 50% price tungeweza kumuelewa zaidi.
Mfano bei ya sasa ni Approx. TZS 2,800/Ltr minimum (Bei ya Dar), 50% yake ni TZS 1,400/Ltr. Tozo na Kodi zote tu ni labda TZS 1,000/Ltr, je wapi tunaweza kupata kwa CIF TZS 400/Ltr?
we na huyo magufuli wako, kamfufueni aisee, kwani wakati wake mafuta hayajawai kupanda?? Au alikuwa na visima vya mafuta huyo mungu wenu, wenzio wanaongelea mambo ya msingi, we na huyo kiumbe wenuShabiby anaongea point, katika yote watakayoongea mwisho wake sisi tunataka kuona mafuta yamepungua bei ifikie ile wakati magufuri yupo 1600-200/l
Kwaiyo waziri wa fedha ulitaka hawe kutoka kanda ya ziwa ,sindio?sasa kama serikali ya tozo inategemea kuvuna hela humo humo kwenye mafuta unategemea waruhusu watu binafsi kujiagizia wenyewe? haya mambo hayahitaji digirii kujua tatizo lilipo, nilishawahi kusema mtu kama mwigulu anakuaje waziri w fedha, for God sake how?
Bei inaweza kuwa za chini na himilivu lakini ametoa tahadhari hapo kuwa mfumo anaopendekeza shabbiby ,kuna kampuni zinaweza agiza mafuta ya ubora wa kiwango cha chini .Hujasema BEI zilikuaje kabla na baada ya huo utaratibu wa BPS.
Jambo la muhimu kwa watumiaji mafuta ni bei na ubora tu, hizo nyingine zote ni mbwembwe tu.