Brother,
Hapa ni rahisi tu. Kwenye gharama mbalimbali za mafuta kuna vitu ni constant/fixed, na kuna vitu ni variable.
Mfano wauzaji mbalimbali wanaweza kua na bei tofauti, au pia wasafirishaji nao wanaweza kua na bei tofauti pia kwa kila ujazo fulani. Lakini yakifika hapa Tanzania gharama za hapa ni constant kwa kila lita. Yaan TBS, TRA, Ewura, TPA, etc hatutaokoa chochote.
Sasa kama Shabiby anaweza kushusha kwa 50% means atacheza kwenye Muuzaji au Msafirishaji au wote wawili. Anaweza kua sahihi kama tu kuna uzembe unafanyika kwenye ku bargain bei ya hivi vitu viwili. Yaani Inawezekana hawa wanaoagiza mzigo mkubwa (Say 100mil litres kwenye mfano wangu wa awali) wanashindwa ku negotiate bei nzuri then akienda yeye na 10mil litres zake wamsikilize.
Au tuje pale pale kua yeye anaweza kupata ya bei rahisi zaidi bila kujali ubora wake tofauti na Wale wa Bulk ambao wanaweza kua too much selective kwenye ubora.
Ubora weka pembeni hilo kama ulivyoweka fixed costs kama zilivyo hapa:
Issue ni CIF bargaining, usafiri na wapi yananunuliwa.
Umesahau kuwa yawezekana tunapigwa.
Timu kuagiza yaweza kuwa imesheheni wahuni mtupu!