Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Kwahiyo kama CHADEMA mngekuwa madarakani mngeruhusu waingize kiholela?

Kuingiza kiholela maana yake nini?

Shabiby kasema wazi mafuta yote yanaingia kupitia kwenye flow meter.

Achana na ukereketwa wa kivyama. Maendeleo hayana chama!

Tuungane kukataa wahuni!

Mzizi wa fitina uko hapo.
 
Mimi ni muumini wa serikali kutoa ruzuku ili bei ishuke. Ama itafute njia nyengine ambayo si ya uagizaji holela kama atakavyo Mh Shabibu itakayo fanya bei ishuke.

Serikali ipi itoe ruzuku ipi wapi ikiwa hata 100/- ya tozo inataka?

Holela ipi unayomnukuu nayo Shabiby out of context, wakati mwenyewe anasema mafuta yote yatapita kwenye flow meters ambazo kwa sasa wahuni wako busy kuzihujumu?
 
Mbona hiyo simu yako unayoitumia kuingia nayo JF iliingizwa kiholela kutoka China na ukainunua huku unakenua meno.
Mimi ni muumini wa serikali kutoa ruzuku ili bei ishuke. Ama itafute njia nyengine ambayo si ya uagizaji holela kama atakavyo Mh Shabibu itakayo fanya bei ishuke.
 
Metre si wana-temper nayo tu.

Kama nchi tumekosa wa kuhakikisha flow meters haziko tempered?

Kwamba kote kumesheheni wahuni?

Hata wewe tukikuweka pale bado tutakuwa tumeuvaa mkenge?
 
Serikali ipi itoe ruzuku ipi wapi ikiwa hata 100/- ya tozo inataka?

Holela ipi unayomnukuu nayo Shabiby out of context, wakati mwenyewe anasema mafuta yote yatapita kwenye flow meters ambazo kwa sasa wahuni wako busy kuzihujumu?

Flow meter ni tarakimu haziwezi kusindikizwa na maneno matupu ya kisiasa bila Takwimu. Atoe takwimu za kodi kabla ya bulk procument na baada ya bulk procument kutetea hoja yake.

Hujui kwa nini 100/-imerudishwa. Haikufuta taratibu kutolewa kwake. Kwa maana nyingine taratibu zikifuatwa ruzuku inaweza kutolewa.
 
Watumiaji mafuta wanachojali ni bei ya mafuta, sio brah brah nyingine
Flow meter ni tarakimu haziwezi kusindikizwa na maneno matupu ya kisiasa bila Takwimu. Atoe takwimu za kodi kabla ya bulk procument na baada ya bulk procument kutetea hoja yake.
 
Flow meter ni tarakimu haziwezi kusindikizwa na maneno ya kisiasa bila Takwimu. Atoe takwimu za kodi kabla ya bulk procument na baada ya bulk ptocument kutetea hoja yake.

Zote katoa hizo.

Basis yake ya argument ni kuwa mafuta yaletwe kwa ushindani. Atakayetoa Ukraine, uarabuni, Venezuela, urusi nk wote waje kuuza kwa bei zao.

Huoni juu ya makodi yaliyopo, bei ya kuagizia pia inachangia katika bei kwa mlaji?

Au wahuni wenyewe ndiyo ninyi nini ndugu?
 
Watumiaji mafuta wanachojali ni bei ya mafuta, sio brah brah nyingine

Hata bei si brahbrah ni shule kamili watu wanayoipata wakati mwengine kwa kuweka miguu kwenye makarai ya maji wakisoma usiku wa manane
 
Hana
Zote katoa hizo.

Basis yake ya argument ni kuwa mafuta yaletwe kwa ushindani. Atakayetoa Ukraine, uarabuni, Venezuela, urusi nk wote waje kuuza kwa bei yao.

Huoni juu makodi yaliyopo bei ya kuagizia pia inachangia bei kwa mlaji?

Wahuni wenyewe ndiyo ninyi nini ndugu?

Hana arguement yeyote ya maana zaidi ya kuitisha serikali isitoe ruzuku na kutaka waruhusuwe kwenda kuizungukia na kuipiga kodi kwa uagizaji mafuta holela.
 
Si kweli. Anataka bei ya kuagizia cif iwe ya ushindani. Mengine wahuni kama tulivyo wazowea hamtakosa vikwazo.

Hiyo cfi ya kuagiza kiholela haikuwepo kabla ya serikali kuona shida yake na kuamua kuhamia utaratibu mpya wa bulk procurement? F = Freight.
 
Hakuna mtu mhinga hapa nchini kama kumuamini mfanya biashara wa Tanzania.

Daima atatafuta faida zaidi ya kinyonyaji basi atakwepa kodi.
Sijaona mfanyabiashara mwaminifu.
Bado
 
Hiyo cfi ya kuagiza kiholela haikuwepo kabla ya serikali kuona shida yake na kuamua kuhamia utaratibu mpya wa bulk procurement? F = Freight.

Wahuni zao huwa ni hujuma.

Suluhu yetu ni kuungana kuwakataa wahuni.
 
Wahuni zao huwa ni hujuma.

Suluhu yetu ni kuungana kukataa wahuni.

Hamna cha uhuni hapa brazaj kwanza sijui hata kama huyu Mh anasense of security precautions. Hivi kweli Tanzania tunataka tukajiingize kwenye vita ya Rubble na Dollar tutaiweza? Tusidanganyane hatuna misuli waliyo nayo China na India. Serikali iruhusu wafanyabiashara Wakitanzania wawe sehemu ya kuhujumu vikwazo kwa Urusi vilivyowekwa na NATO. Kwenda kununua mafuta kiholela ya kwenye hizo meli za Urusi anazozitaja huyu Mh zilizoko deep sea ni kuhatarisha Ulinzi na Usalama wa nchi.
 
Sasa ndugu mdau hebu tueleze . juzi tumeambiwa mafuta yapo ya kutufikisha siku 27. Lakini juzi ewura wametangaza bei mpya na zimeanza kutumika hapohapo , kwanini isingesubiriwa hizo siku 27 ziishe Ndo bei zibadilike?
Mkuu,
Labda kwa sasa ni kweli tuna mafuta ya kutumia siku hizo 27, lakini huko nje yamepanda bei tumeagiza kwa bei kubwa. Yaani kwenye costing ya mafuta hua wanatumia average pricing na sio kila mzigo na cost yake. Average means bei ya yaliyoko na bei ya yanayokuja.

Usipofanya hivyo utajikuta yaliyoko umeuza sawa kwa bei "nafuu" lakini ulichopata hakikuwezeshi wewe kulipia mzigo mpya uliopanda bei.
 
Hatutaki mambo ya ujamaa, yalishindwa vibaya enzi za Mwalimu. Huu ni wakati wa soko huria na soko linapaswa lituongozo sio serikali ilipangie na kuliongoza soko.
Mjadala wake bahati mbaya haukufika hapa jF.
 
Urusi haijawekwa vikwazo kwenye mafuta na gesi, hata Ulaya bado inanua mafuta na gesi kutoka Urusi. Hujui unachosema, akili yako imedumazwa na kufungwa na mawazo ya kijamaa yaliyopitwa na wakati na ambayo hayajawa na tija kwa nchi yetu kwa muda mrefu sana tangu kuwepo kwake.

Back
Top Bottom