Kuweka Records Sawa: Utaratibu alioupendekeza Shabiby ndio uliokuwepo kabla, Haufai

Sababu zilikuwa na mashiko kipindi hicho ila kwa sasa hakuna maana kwa sababu kama ni Kodi kuna valuation systems mpya,kila taarifa unaipata kwenye mtandao kwa hiyo janja janja inakuwa imepunguzwa..

Pili swala la quality kuna TBS,ishu ya kuficha mafuta Ili bei zipande halina msingi kwa sababu mafuta yanayoingia yanajulikana na yanayotumika yanajulikana.. kampuni zikiwa nyingi hiyo cartels ni ngumu Sana..

Hili la mafuta ya magendo inawezekana ila yakiingia hayawezi kuuzwa Kwa bei ya Juu,lakini pia hayawezi kuwa mengi kwa kiasi hicho maana utayasafitishaje bila kugundulika?..

All in all kinachotakiwa ni mafuta yauzwe Kwa bei ya chini ambapo chini ya bulk procurement imeshindikana kupata huo unafuu na in fact bei inakua moja..

Mwisho hivi kampuni za biashara ya mafuta zitakua vipi kwa staili hii ya bulk procurement ikiwa mnalazimishwa kununua kwa wauzaji wakubwa wachache na Kwa bei ambayo wamepanga wao na Serikali?..

Huu utaratibu licha ya kutotoa nafuu ya bei kwa wananchi unawanufaisha makampuni makubwa wachache na maofisa wa serikali, wengine nyie mtaishia kama kuwa mawaka wao..

Duniani kote mafuta yanaagizwa na kampuni binafsi tofauti tofauti,suala la kuwa na mafuta ya akiba ni la serikali kupitia tpdc/puma hao ndio wawe na reserves za kuja ku offset in case kuna scenarios kama ya kuficha mafuta au upungufu wa kawaida...

Mwaka juzi somewhere around 2018 mafuta yaliadimika na bulk procurement ilikuwepo so hii sio sababu ya msingi Ili mafuta yasiadikike.
 
Shabiby anasema mafuta yauzwe 1,400 lakini kodi za Serikali takriban TZS 1,000 au zaidi zisiguswe sababu ndizo zinazolipa au kununua madawa. Means kuna uwezekano wa kupata mafuta ya mpaka TZS 300/Litre CIF.

"Burden of Proof" hapa ni iko kwa Shabiby kutuambia wapi tutapata kwa hii Bei. Amesema Deep See unaweza kupata kwa mpaka 1/4 price ya world market price, Serikali umuombe awasaidie details za huko wakayachukue wakishajiridhisha ubora na Usalama wake .
 
K
Shabiby mpigaji tu!
Kumbe ! Mafuta ni Kila kitu,mazao shambani,uzalishaji viwandani,usafiri na usafirishaji, tunataka bei nafuu ya mafuta.hiyo Bulk imeundwa na kina nani?isije kuwa wanaofanya biashara ya mafuta ndio wanaajaza kwa pamoja na sisi tunasema ni Bulk kumbe ni cartel.hatutaki 'monopoly' kama si kwa ushindani,basi serikali iunde kampuni ya kununua na kusambaxza mafuta ,si. TIPPER !,kwa nini hapo TU bei ili hali kwani wap eaweze na sisi tushindwe_why !
 
Nimeiskiliza kwa umakini mkubwa clip ya Shabiby. Kwa wakati huu wa vita ya urusi bulk procurement sio njia sahihi ya kuagiza mafuta nje! Kwa sababu kampuni inayotumika inachukua mafuta iliyowagonga vikwazo Russia. Hii ina maana wamebadili soko na hivyo hili likampuni ni la EU.
Hii ni fursa kwa kampuni kuagiza nje mafuta kwa bei nafuu...kwani huyo Mrusi tu kwa sababu ya vikwazo ameshusha bei ya mafuta yake up to 600 per litre.
Sasa 600 tukaweka na vikodi uchwara vyao hapo. Yakauzwa 1200 siye wananchi tutakuwa na shida gani?
Shabiby kasema wazi kuwa hako kakamati kanakosiamamia bulk procurement na kenyewe kanapiga cha juu vizuri tu kwenye hizo bei za kuagiza.

Faida ulizozielezea hapo kwa bulk procurement ni nzuri lakini haziondoi ukweli kuwa bulk procurement kwa kipindi cha vita inaumiza wananchi.
 
Watanzania mnapenda sana magendo!
 
Good analysis. Inaonekana ni sekta yako unayoielewa vizuri.

JF ndivyo ilivyostahili kuwa. Kuna mambo kama member wa JF umatakiwa kuwasikiliza wataalam au wenye uelewa wa kutodha kwenye eneo hilo, japo haizuiwi kuuliza.

Bahati mbaya, siku hizi, JF kuna virukia njia, kila wakiona kitu, hata kama hawajui, wanarukia tu, tena kwa jeuri, jeuri ya kijinga.
 
Shabiby anasema mafuta yauzwe 1,400 lakini kodi za Deep See unaweza kupata kwa mpaka 1/4 price ya world market price, Serikali umuombe awasaidie details za huko wakayachukue wakishajiridhisha ubora na Usalama wake .
Serikali haiwezi kwenda deep sea

Kifupi kuna machinga wauza mafuta mengine ya wizi 'magendo nk huko deep sea.Mengine yanatoka nchi zilizowekewa vikwazo hivyo wenye business vya mafuta huamua kuyauza kwa magendo .Serikali na magendo wapi ns wapi

Shabby alichoshauri watu binafsi waachie hiyo shughuli Serikali isubiri Meli bandarini kachukue kodi zao mafuta bei rahisi waingie

Hizo meli zinaitwa Ro Ro kama sikosei ziko nyingi deep ni machinga waliochangamka ambao huuza bidhaa nyingi tu ikiwemo.mafuta

Huu no wakati muafaka Serikali iruhusu sekta binafsi waingize mafuta itashangaa. Mafuta ya bei chee yataingia
 
Safi sana. Nchi hii haija hawahi pungukiwa wazalendo. Mh Shabibu hakutaka kuweka wazi kitu kilicho sababisha serikali kuamua bulk procurement. Uzuri wenyewe alikiri Watanzania wa leo si wale wa mwaka 47.
hili aliliweka wazi kinaga ubaga

Shabiby kasema sababu ya kuletwa Bulk Procument System ni Wazungu wa TOTAL kulalamika ku loby serikalini kwamba Wahindi wa JAMNAGAR (walionunua GapOil na GapCo) wameshusha bei ya mafuta kupindukia walipokuja Tanzania.

BPS ilipoanzishwa JAMNAGAR akaona hakuna ushindani, business plan yake ya kuja Tanzania ilikuwa kushusha bei kuteka soko, akaondoka zake.

Bei zikafumuka tena.
 
Shabiby anataka fursa atupige. Ule utaratibu uliondolewa sababu ulileta shida sana kwenye controls. Naona wanataka kuanza kumdanganya spika wapenyeze upigaji wao
 
Unaona. Sasa!!!
Mafuta ya deep see yanayouzwa rahisi ni mafuta ya magendo na hayana constant flow, kwamba utayapata kila siku,
Ni sawa tu na kununua simu ya dili kinondoni
 
Muhindi anapata wapi mafuta ya bei nafuu ilhali source ya mafuta ni moja na bei zinajulikana?
Nyanya sokoni zina bei tofauti sababu zinatoka sehemu mbali mbali na gharama za kuzilima zinatofautina , mafuta yana source moja mtu anaposema ana ya bei tofauti kabisa na ya soko , ni either ameyachakachua au ni ya deal.
 
Mafuta kufikia 3000 lazima itafutwe njia mbadala.
Ndio sababu ulaya zamani sanq walianza na hybrid car , electric nk. Ilikuwa ni swala la muda tu kabla hayajalipuka bei
 
Mkuu umepotoka kidogo , you may want to edit your post .
Roro sio meli za mafuta , ni meli ya kubeba mizigo hasa magari yanayotembea
Terminology Roro ina maana ya' Roll on and roll off' kwa maana gari litaingia na kutoka kwenye meli hiyo likiwa linatembea
Swaum njema
 
Ok mfano meli kwa meli yenye mafuta na ingine haina mafuta zikisogeleana meli yenye mafuta ikipump mafuta kuingiza meli ingine inayopokea mafuta deep sea na kuondoka nayo kwenda nchi husika hiyo meli ina pump mafuta sio Roro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…