KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ulaya ya wapi nyumba zinajifunga?
Screenshot_20240724-102815.png
 
Kwamba hizo Smart Lock zitajifunga kama hujalipa kodi, maswali ni mengi kuliko majibu.

Hivi likijifunga na watoto wako ndani inakuaje majanga yakitojea mfano ya moto?

Network ikizingua control namba ikawa inasumbua itakuaje?

Hata kama zitakupa alarm kodi ikikaribia kuisha ila huu ni ukatili, chama cha kumlinda mlaji kinatakiwa kuingilia kati.

Nawasilisha.👇👇

View attachment 3050649
Hameni wakose wateja
 
Sio Ukatili tu hawajafikiri swala la Moto pia si unajua Watanzania tunaongoza kwa Udumavu wa kufikiri..
Tatizo exposure
Hujaishi ulaya na marekani wewe
Hizo smart lock kule kiboko .Ukipanga nyumba kodi unayolipa imeunganishwa na maji,umeme na gesi na milango yenyewe
Ikifika muda wa kulipa kodi hujalipa milangi inajifunga yote,umeme,maji na gesi vyote vinakatika uwe ndani ya nyumba au nje na ripoti zinapelekwa kwenye database ya wenye nyumba za kupangisha kuwa wewe ni mpangaji mkorofi na taarifa zingine zinaenda kwa madalali wa kuja kukutoa kwa nguvu.Na toka hapo jiandae kuwa Homeless hakuna mwenye nyumba yeyote atakayekuja kukupangisha wewe chumba au nyumba

Ndio maana waweza kuta homeless wengine wanalala kwenye magari au viambaza wengine sababu ni hiyo
Nchi za wenzetu kodi ya nyumba ni kitu cha kwanza ambacho hawezi cheza nacho

Watanzania tubadilike Uswahili swahili una mwisho wake
Tunaingia ulimwengu wa kidigitali ambapo sio kila wakati mwenye nyumba anakuja kupiga hodi kwako kikudai kodi .Unafungiwa huko .
 
Wewe huna akili kichwani, kuna watu wamezaliwa hapo kabla ya vile vinyumba kubomolewa kujengwa maghorofa.

Hapa ndio kuna watu kweli watamkumbuka Magufuli.
Kuzaliwa na Kuzeekea nyumba ya kupanga hakumfanyi mpangaji mzee kuwa ndie mumiliki wa hiyo nyumba ya kupanga
Mpangaji hubaki mpangaji hata hiyo nyumba mtu apange miaka 80
 
Kuna mtu asiyependa kujenga? Majitu wengine mnavyoiba pesa makazini kwenu basi mnaona kila mtu ana access ya wizi.
Wapo kibao wenye pesa ambao hawataki kujenga hupenda kupanga tu mfano mmojawapo ni wahindi.Wanapenda sana kupanga kuliko kujenga hata awe na pesa vipi
 
Tatizo exposure
Hujaishi ulaya na marekani wewe
Hizo smart lock kule kiboko .Ukipanga nyumba kodi unayolipa imeunganishwa na maji,umeme na genius na milango yenyewe
Ikifika muda wa kulipa kodi hujalipa milangi inajifunga yote,umeme,maji na genius vyote vinakatika uwe ndani ya nyumba au nje na ripoti zinapelekwa kwenye database ya wenye nyumba za kupangisha kuwa wewe ni mpangaji mkorofi na taarifa zingine zinaenda kwa madalali wa kuja kukutoa kwa nguvu.Na toka hapo jiandae kuwa Homeless hakuna mwenye nyumba yeyete atakayekuja kukupangisha wewe chumba au nyumba
Ndio maana waweza kuta homeless wengine wanalala kwenye magari au viambaza wengine sababu ni hiyo
Nchi za wenzetu kodi ya nyumba ni kitu cha kwanza ambacho hawezi cheza nacho

Watanzania tubadilike Uswahili swahili una mwisho wake
Tunaingia ulimwengu wa kidigitali ambapo sio kila wakati mwenye nyumba anakuja kupiga hodi kwako kikudai kodi .Unafungiwa huko .
Yani wewe unataka kumlinganisha Messi na Kibu Denis akili za kijinga hizi.

Unskills job mtu analipwa dolla 20 kwa saa, akipiga masaa 10 ana dolla 200 per day, mambo ya bill yatamsumbuwa vipi?

Turudi Bongo sasa, unaelewa vizuri vipato vya Watanzania?

Kuna watu mpaka tarehe 9 ya mwezi mpya hajalipwa mshahara unalifahamu hilo?

Halafu kama ulikuwa hujui Watanzania wengi hawana kazi wana shughuri tu kwa kifupi watu wengi hawana ajira rasmi wanaungaunga tu halafu unaleta huu upuuzi wa smart lock?

Nina Anko wangu amestaafu kazi mwezi wa pili huu hata pesa za mizigo hajalipwa, calculation za award yake bado, security fund yake bado halafu mnaleta huu upuuzi wenu wa smartlock mnajifanya mmesoma kumbe wapuuzi watupu hakuna mlichoelimika wezi wakubwa.
 
Wapo kibao wenye pesa ambao hawataki kujenga hupenda kupanga tu mfano mmojawapo ni wahindi.Wanapenda sana kupanga kuliko kujenga hata awe na pesa vipi
Unachanganya mambo tu mimi naongelea Watanzania wa kawaida hakuna asiyetamani kumiliki nyumba yake.

Watu waliojipata wengine hata kupanga hawataki wanaishi hotelini maisha yao yote
 
Wabongo hatuwezi kuendana na teknolojia hata kidogo , hapo awali kulikuwa na huduma za maji kwa kuweka sarafu tu unapata maji kulingana na pesa yako ...Sijui ilikuwaje mkaondoa ule mfumo ili mkope .

Hizo mita nilisikia zipo Iringa kwa sasa ..Lazima upate utakacho kila siku zile mashine za ATM mnaharibu pia .
 
Yani wewe unataka kumlinganisha Messi na Kibu Denis akili za kijinga hizi.

Unskills job mtu analipwa dolla 20 kwa saa, akipiga masaa 10 ana dolla 200 per day, mambo ya bill yatamsumbuwa vipi?

Turudi Bongo sasa, unaelewa vizuri vipato vya Watanzania?

Kuna watu mpaka tarehe 9 ya mwezi mpya hajalipwa mshahara unalifahamu hilo?

Halafu kama ulikuwa hujui Watanzania wengi hawana kazi wana shughuri tu kwa kifupi watu wengi hawana ajira rasmi wanaungaunga tu halafu unaleta huu upuuzi wa smart lock?

Nina Anko wangu amestaafu kazi mwezi wa pili huu hata pesa za mizigo hajalipwa, calculation za award yake bado, security fund yake bado halafu mnaleta huu upuuzi wenu wa smartlock mnajifanya mmesoma kumbe wapuuzi watupu hakuna mlichoelimika wezi wakubwa.
Kifupi mtu aishi mahali kipato chake kinaendaba na mtiririko wa hicho kipato chake

Kuna msemo mtu asiige kunya kwa tembo.Nyumba kama hizo za smart lock watu hao wa kawaida wao wenyewe wajitahmini bila kufanyiwa tatami na mtu kama wanastaili kuishi eneo kama hilo kwa vipato vyao vya kuunga unga
 
Wabongo hatuwezi kuendana na teknolojia hata kidogo , hapo awali kulikuwa na huduma za maji kwa kuweka sarafu tu unapata maji kulingana na pesa yako ...Sijui ilikuwaje mkaondoa ule mfumo ili mkope .

Hizo mita nilisikia zipo Iringa kwa sasa ..Lazima uapte utakacho kila siku zile mashine za ATM mnaharibu pia .
Kwa nini mnapenda kutetea ujinga? Mbona Luku watu wanalipa bill shida?

Siyo kila mifumo ya wazungu ni ya kuiga, kama tunakubali mifumo ya wazungu mbona ccm wanang'ang'ania hawataki kupisha chama kingine?
 
Kodi ikikaribia kuisha nweka kimbao mlango usijifunge
System inaona huko ofisini kuwa kuna mtu anavunja mlango nyumba namba fulani sababu sensor zake zinasoma ukijifunga na kujifungua
Utaikuta defender hii hapa
Na kwenye mkataba hutakiwi kuharibu mali ya nyumba
 
Back
Top Bottom