KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

KERO Kuweka Smart Lock kwenye Magorofa ya TBA Magomeni Kota ili kufunga milango kodi inapoisha ni ukatili kwa wapangaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kifupi mtu aishi mahali kipato chake kibaendaba na na mtiririko wa hicho kipato chake

Kuna msemo mtu asiige kunya kwa tembo.Nyumba kama hizo za smart lock watu hao wa kawaida wao wenyewe wajitahmini bila kufanyiwa tatami na mtu kama wanastaili kuishi eneo kama hilo kwa vipato vyao vya kuunga unga
Nenda South Africa ukapate elimu Mandela alianzisha sera gani ya makazi.

Hao wapangaji wapo hapo miaka yote ndio maisha yao, hizo nyumba hazipaswi kuwa za kibiashara pasee, hizo nyumba ni huduma za makazi, serikali inahudumia raia wake kwa low cost rent.

National housing na hao TBA hayo mashirika hayapaswi kuendeshwa kama real estate agents.
 
Kwa nini mnapenda kutetea ujinga? Mbona Luku watu wanalipa bill shida?

Siyo kila mifumo ya wazungu ni ya kuiga, kama tunakubali mifumo ya wazungu mbona ccm wanang'ang'ania hawataki kupisha chama kingine?
Hizo smartlock mtazoea tu bado ushamba ni mwingi .
 
Kwamba hizo Smart Lock zitajifunga kama hujalipa kodi, maswali ni mengi kuliko majibu.

Hivi likijifunga na watoto wako ndani inakuaje majanga yakitojea mfano ya moto?

Network ikizingua control namba ikawa inasumbua itakuaje?

Hata kama zitakupa alarm kodi ikikaribia kuisha ila huu ni ukatili, chama cha kumlinda mlaji kinatakiwa kuingilia kati.

Nawasilisha.👇👇

View attachment 3050649
Ili kuepuka usumbufu, lipa Kodi mapema.
 
ukiwa ndani unaweza toka ila huwezi kuingia, nadhani ndo mechanism yake ilivo, sasa cha kufanya mmoja asitoke awe anawafungulia wanaotoka wakirudi mpaka mtakapopata kodi.
Ulaya na Marekani walichofanya kodi na maji,umeme na gesi ya kupikia vyote viko pamoja Kodi usipolipa vyote vinakatika kwa mpigo
Kodi ikikatika hujalipa umeme kwa heri maji kwa heri na gesi kwa heri
 
Kwa nini mnapenda kutetea ujinga? Mbona Luku watu wanalipa bill shida?
Hata Luku ilipoanza watu walipiga kelele sababu mita zilipokuwa zikitumika unalipa umeme ukijisikia mfano waweza tumia umeme miezi sita bili hujaletewa ikija inakuja imechelewa na inadai mwezi mmoja tu nao waweza kwenda kulipa unasema napunguza kidogo wanakubali

Luku ikaja kuwa unanua utakaotumia ukiisha badi watu wakapiga yowe ohh sass kama sina hela huku ni kuonea wanyonge ambao vipato vyao sio vya uhakika

Leo hii hakuna mwenye kelele na Luku
Hata hilo la Smart Lock litazoewa tu kama ilivyo Luku

Ushamba kumtoka mtu hutakiwa apewe muda
 
Ulaya na Marekani walichofanya kodi na maji,umeme na gesi ya kupikia vyote viko pamoja Kodi usipolipa vyote vinakatika kwa mpigo
Kodi ikikatika hujalipa umeme kwa heri maji kwa heri na gesi kwa heri
du hyo kali, nadhani waliogopa watu kufanya kama nilivowashauri wa magomeni hapo,
 
Kwamba hizo Smart Lock zitajifunga kama hujalipa kodi, maswali ni mengi kuliko majibu.

Hivi likijifunga na watoto wako ndani inakuaje majanga yakitojea mfano ya moto?

Network ikizingua control namba ikawa inasumbua itakuaje?

Hata kama zitakupa alarm kodi ikikaribia kuisha ila huu ni ukatili, chama cha kumlinda mlaji kinatakiwa kuingilia kati.

Nawasilisha.👇👇

View attachment 3050649
Kuishi kwenye nyumba ni tukio baada ya makubaliano ya mwenyenyumba na mpangaji, ikiwa hukubaliani na taratibu za mwenye nyumba, basi mwache na nyumba yake. Akikosa wateja atafikiria kubadili taratibu.

Ukianza kupiga kelele, utaonekana ulipanga kuishi kwenye hizo nyumba bila ya kulipa pango. Kwani, kama huna shida ya kulipa pango kwa wakati, wala hutajua kama vitasa hujifunga ikiwa unadaiwa pango.

Ova
 
Hata Luku ilipoanza watu walipiga kelele sababu mita zilipokuwa zikitumika unalipa umeme ukijisikia mfano waweza tumia umeme miezi sita bili hujaletewa ikija inakuja imechelewa na inadai mwezi mmoja tu nao waweza kwenda kulipa unasema napunguza kidogo wanakubali

Luku ikaja kuwa unanua utakaotumia ukiisha badi watu wakapiga yowe ohh sass kama sina hela huku ni kuonea wanyonge ambao vipato vyao sio vya uhakika

Leo hii hakuna mwenye kelele na Luku
Hata hilo la Smart Lock litazoewa tu kama ilivyo Luku

Ushamba kumtoka mtu hutakiwa apewe muda
Unachanganya sana mamboz nina exposure ya kutosha na ninajuwa vizuri ninachokiandika.

Kufananisha maisha ya first world na Tanzania ni kujitowa akili tu.

Nchi inayoweza kujifananisha life style na first world ni South Africa peke yake.

Wacha nikuache vijana wa sasa ukimaliza chuo, una kibarua cha kuingiza million 2 una Subaru na bank una million 5 huwa mnamuona kila mtu ni mjinga na hajui kutafuta pesa.

Subiri uwe na familia ndio utajuwa kuna maisha unaamka hata buku hauna mfukoni.
 
Watanzania bila kuwasukuma ni ngumu Sana na utafeli Mimi namkubali Sana chalamila huwa anaongea makavu bila kusita ni Bora uende vingunguti Huko ukapange kuliko kuishi magomeni.
Kama unashindwa kulipa Kodi za TBA hamia kwenye size yako, maisha ya ujanja hayapo sikuhizi
 
Ulaya na Marekani walichofanya kodi na maji,umeme na gesi ya kupikia vyote viko pamoja Kodi usipolipa vyote vinakatika kwa mpigo
Kodi ikikatika hujalipa umeme kwa heri maji kwa heri na gesi kwa heri
Ulaya marufuku kukata Maji hata kama hujalipa miaka
Usisikilize hayo
Maji ni uhai hawakati hata siku moja

Na Umeme na gesi kama ulikuwa unalipa kwa mwezi bila luku basi usipolipa kwa muafaka wenu wanakubadilishia mfumo na kuweka kama wa luku
Ila maji hayakatwi sio Africa huku
 
Tatizo exposure
Hujaishi ulaya na marekani wewe
Hizo smart lock kule kiboko .Ukipanga nyumba kodi unayolipa imeunganishwa na maji,umeme na gesi na milango yenyewe
Ikifika muda wa kulipa kodi hujalipa milangi inajifunga yote,umeme,maji na gesi vyote vinakatika uwe ndani ya nyumba au nje na ripoti zinapelekwa kwenye database ya wenye nyumba za kupangisha kuwa wewe ni mpangaji mkorofi na taarifa zingine zinaenda kwa madalali wa kuja kukutoa kwa nguvu.Na toka hapo jiandae kuwa Homeless hakuna mwenye nyumba yeyote atakayekuja kukupangisha wewe chumba au nyumba

Ndio maana waweza kuta homeless wengine wanalala kwenye magari au viambaza wengine sababu ni hiyo
Nchi za wenzetu kodi ya nyumba ni kitu cha kwanza ambacho hawezi cheza nacho

Watanzania tubadilike Uswahili swahili una mwisho wake
Tunaingia ulimwengu wa kidigitali ambapo sio kila wakati mwenye nyumba anakuja kupiga hodi kwako kikudai kodi .Unafungiwa huko .
Ninaishi Nje shida yangu huku nje ukiita fire au ambulance ni dakika tu wamekuja mambo ya kuiga huku nje wakati Tanzania tatizo la kuibiwa watoto wakitoka shule linatusumbua haya majanga ya Moto yakitokea inakua balaa ni vile watu wengi moto wanauchukulia poa ila kwa huu mfumo kwetu bado sana..najua madhara ya Moto ndio maana nimeuzungumzia...
Ila Ulaya watakayokata maji labda ya Garijembe maji kwao ni Uhai kweli..
 
Hi kweli inaweza kufanya kazi kwa mazingira ya tanzania naona kama ni kuwatisha tu hao watumishi kwani watumishi wengi wa umma ni kama hawajielewi wanapenda sana miteremko
 
Kwa nini mnapenda kutetea ujinga? Mbona Luku watu wanalipa bill shida?

Siyo kila mifumo ya wazungu ni ya kuiga, kama tunakubali mifumo ya wazungu mbona ccm wanang'ang'ania hawataki kupisha chama kingine?
Hii mifumo ni ya Hotel au kwenye maduka ya biashara sio kwenye makazi ya watu.
Watanzania wanapenda kuiga vitu vya kijinga na kuacha vitu vya maana mbona matumizi ya Kodi hawaigi Ulaya kwa kutengeneza miundo mbinu bora..
 
Back
Top Bottom