Acha ujinga weka hoja, kwa nini mlalamike Islamic knowledge wakati huo huo kuna divinity?
Muamzisha uzi na wachangiaji ikiwemo wewe mmekurupuka na chuki zenu zilizopitiliza.
Mnajadili why Islamic knowledge??
na mnajifanya hamjui kuwa divinity ipo
Huna hoja bali kuleta kwa screen shot hii ya divinity katika combination kunadhihirisha utahira wenu
• Hoja gani sasa unayotaka, Toka thread hii imeaza hujaona hoja humu,? Hoja zimejitosheleza mkuu..., Ndo maana nasema kama hujaona hoja yoyote humu.. Ujue uwezo wako wa kufikiri ni mdogo.
------------------------
Minong'ono na maneno ya kujigamba kuwa mimi ni nani na wewe ni nani, yaliaza kutokea pale bandari ilipotakiwa kusimamiwa na kampuni isiyoeleweka ya
D. P. W, machawa kila pande ya Tanzania waliibuka na kuisifia
D. P. W, machawa wengine walifika mbali Zaidi nakufikia hatua ya kutukana viongozi wa dini kule Upande wa pili.
INASIKITISHA SANA KUWA NA BINADAMU WA AINA HII HAPA TANZANIA walio kosa weledi wakuchanganua mambo kwa manufaa ya baadae.
TAHASUSI/COMBINATION zina udini ndani yake,
• Mambo haya yanayo husiana na udini, hupandikizwa taratibu taratibu lakini mwisho wa siku hugeuka kuwa bomu lisilozimika hata kwakulimwagia damu.
• Udini, au upendeleo usiofaa kwa dini moja dhidi ya nyingine, unaweza kuleta athari mbaya kwa jamii na nchi kwa ujumla.
Tunaweza tusiyaone haya kwa sasa lakini siku za baadae mambo yatakuwa hatari sana:-
|• Mgawanyiko wa Kijamii, Udini husababisha watu kutengana kulingana na imani zao za kidini, hivyo kuvuruga umoja na mshikamano miongoni mwao
||• Mzozo na Vurugu, udini unachochea migogoro na vurugu, hasa ikiwa makundi ya kidini yanahisi kutengwa au kubaguliwa katika nchi husika.
|||• Ubaya katika Utoaji Haki, unasababisha upendeleo katika nafasi za ajira, elimu, na huduma za serikali, ambapo watu wanapendelewa au kunyimwa fursa kulingana na dini zao.
|V• Kupungua kwa Uaminifu kwa Taasisi, Udini unapokithiri katika serikali na taasisi nyingine, kuna uwezekano wa kupungua imani ya wananchi kwa uadilifu wa taasisi hizo, hivyo kudhoofisha utawala wa sheria na demokrasia.
V• Ukosefu wa Ustawi wa Kiuchumi, Udini uleta kutengwa kwa makundi fulani ya kidini kutoka kwenye shughuli za kiuchumi, kusababisha ukosefu wa usawa na kuzuia maendeleo ya kiuchumi kwenye jamii.
V|• Kupunguza Utalii na Uwekezaji, Migogoro ya kidini inaweza kuathiri taswira ya nchi kimataifa, hivyo kupunguza idadi ya watalii na kuwatia hofu wawekezaji.
V||• Uharibifu wa Mali na Maisha, Migogoro ya kidini inaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na hata kupoteza maisha, kugharimu jamii na nchi kwa ujumla.
• Kupambana na udini na kujenga jamii inayovumiliana na kuheshimu tofauti za kidini ni muhimu kuwa na amani, ustawi, usawa kimajukumu na maendeleo endelevu ya jamii.