Kuwekwa kwa somo ya Kiislamu kwenye Tahasusi kunaashiria nini?

Suala hapa siyo Kodi,mtoa mada uwe wazi unahofu na Hilo box.Nami nimekuelewa hapo kuwa unahofu na matokeo ya wale watakao fundishwa hasa upande Wa pili.Usipige chenga kusingizia Kodi kwani hao wengine hawalipi Kodi. Masomo ya dini zote yanafundishwa acha watoto wanaotaka wasome.Wengine hawana uwezo Wa hizo shule binafsi.
 
Ndugu zangu Watanzania masuala ya kidini yaendelee kama tulivyokuwa.Taasisi za dini ziwajibike kufundisha masomo ya dini.
Tuna mifano hai ya taharuki ya migongano ya dini nchi hii. Karibuni, miaka ya 2012 hadi 2013 tulikuwa na taharuki ya UCHINJAJI. Geita mauaji yalitokea. Maeneo mengine kulikuwa na bucha za wakristo pekee. Serikali ya wakati huo ikaunda kamari za viongozi wa dini ambazo zipo hadi leo. Mambo yakapoa.

Jamani bandugu tusianze mambo ambayo baadaye yataleta maangamizi kwenye taifa letu.
 
Sijuwi kwanini viongozi wskubwa wameziba masikio kuhisi hili jambo
 
Basi liache hilo box bila kulibighudhi. Shetani akikutafuta kwenye dhambi akikukosa anakufuta kanisani. Ana adili kitu kimoja kimoja kwenye vile ulivyokua unaabudu. Mwishoni unamwabudu bila kujua. Tuache masuala ya dini yanakotakiwa kuwa. Sio Ikulu wala bungeni
 
Wagalatia wanateseka sana na uislmau, Punguzeni chuki wakuu zitakuuweni wenyewe
 
swala la dini najiuliza watafundisha nini maana shida itakuja wakristo wanamadhehebu tofauti tofauti mlokole hawez kumfundisha divinity mroma na mroma hawez mfundisha divinity msabato..msabato nae hawez mfundisha divinity mu AC au mashahidi wa YEHOVA. Tuje upande wa islamic wao piah wana shia suni na makundi mengneyo yamegawanyika ko hawawezi fundishana ata kidogo..... maono yangu ni kuwa labda serikali imepima inataka ifanye kama anachofanya kagame kuwa mbeleni bila degree huwezi kua shekhe au mchungaji...ili kupunguza dini zenye misimamo mikali......!
 
Bila Chuki wala Dhihaka Ubaya uko wapi?

Mbona Bible knowledge ipo na hamsemi?
 
The only challenge I see ni watu kuamini wanasoma ili waajiriwe,

Ki ukweli aliyesoma amesema, hata kama Hana ajira, anakuwa na uwezo wa kuziongeza kwenye mambo yake.

So, kwa vijana wa sasa lazima tuongee wigo ili wakujiongeza waje kuziongeza.
 
Hongera mkuu

Taifa linahitaji watu weledi mfano wako

# We must separate religion and state
 
Kwani sasa hivi hayo masomo ya dini yanafundishwaje?.Maana wanafunzi wanafanya mitihani na wanaofaulu wanafaulu na wanaofeli wanafeli. Kwakuwa hakuna atakaye lazimishwa kusoma tahasusi yenye Somo la dini wanaotaka wasome wapewe nafasi.
Hakuna shida,

lakini hayo masomo ya dini kwanini yafundishwe kwa kodi za watu wote!?

Unaelewa mambo ya imani ni ya kibinafsi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…