Ilinitokea hiyo, Nilitoa kwa card NMB Wakala hapo Kariakoo yule wakala mpaka leo namkumbuka, baada ya kutoa fedha kiasi cha 300,000 nikaondoka baada ya kuona message imeingia kwenye simu kwamba umetoa kiasi cha sh 300,000 kutoka kwa wakala ABC... sasa kumbe message zimeingia mbili za miamala ya 300k, ila kwasababu ya haraka utaona ile message moja tu, au hata ukiona mbili utasema labda ni mtandao tu, Sasa kumbe yule wakala amefanya miamala miwili ya laki tatu jumla 600k ila cash aliyonipa mkononi ni 300k. Sikuhangaika kuwaza au kuangalia salio. Baada ya siku kadhaa kupita nikasema ngoja niangalio salio, Lahaula! Nakuta 300k haipo na sielewi imeenda wapi! Chap nikaenda NMB Bank nikaomba statement, kuangalia nakuta ile siku niliyotoa 300k kumbe ilikuwa 600k! Yaani miamala inaonekana miwili imefuatana.Wakanipa barua nikafuate hiyo 300k iliyobaki kwa yule wakala, wakaniambia au kama nimepasahau wao wanaweza kuwasiliana naye, bahati nzuri nikapakumbuka, nikarudi nikamuonyesha vielelezo vyote, wala hakua mbishi, chap akanivutia 300k yangu nikatembea.
Fikiria wangapi wanaofanya miamala midogo wala hawaangalii salio au bank statement wanaibiwa kiasi gani? Ina maana nisingeshtuka ndiyo ingekuwa basi tena😀