Kuweni makini: Nyumba za kisasa zisizoonyesha bati juu zinavuja mno, msikimbilie kujenga

wanadai ni contemporary designs ilhali ni fashion za enzi za vasco da gama
 
Hizi nyumba zinajengwa sana huko Uarabuni maeneo ambayo yanafanana na Jangwa kwa sababu hamna mvua za mara kwa mara na kina joto kali kwa hyo wanaepuka joto linalosababishwa na bati..
Lakini huku kwetu bila ufahamu watu wamekurupuka kwa kuiga na wengi wao wanalia
 
Unadhani wanapenda..hali za uchumi hazruhusu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nikweli kabisa
 
Ubahiri wenu ndio unawaponza.

Mm nazijenga Sana na Wala hazivuji
Sikilizeni. Tanzania ukihesabu nyumba ambazo zina ubora i.e. zimejengwa kwa kufuata utaalam sidhani kama utapata hata asilimia 30. Nchi yetu watu wanaunganisha matofali na kupiga bati juu lakini hawajengi nyumba. Wenzetu majuu wakijenga wanajua hata nyuzi joto ndani itakuwa kiasi gani. Wanajua mzunguko wa hewa unaotakiwa... ni mambo mengi. Mtaani mafundi asilimia kubwa ni vilaza.
 
Hizo Ni nyumba Kali Sana ila sio za kujenga maskini na kuokoteza mafundi..

Shida kubwa Ni supply ya mafundi wataalamu Ni wachache.

Ingekuwa hivyo magorofa yangekuwa yanavujq Sana .

Ushauri jengea kwa kutumia kampuni za ujenzi ili iwe rahisi kuwa consult.
 
Pamoja na hayo nyumba za contemporary sio za fundi Michael,tumia kampuni za ujenzi na gharama Ni nafuu..

Kampuni unqchagua kuanzia ramani za chini na Hadi finishing,hii ya kusema naomba ramani yako unampa fundi Michael ita ku cost..

Kwenye Miji mikubwa mafundi wapo ila huku kwingine hata paa za kawaida tuu zikiwa na mitindo wanashindwa kuezeka..

Paa Kama hii hapa chini huwezi pata fundi kwenye miji yetu midogo kiasi kwamba mitindo iliyopo ya uesekaji Ni ya kufanana 👇
 

Attachments

  • ASUKILE CLASSIC 4-FINAL.png
    28 KB · Views: 22
  • North Elevation-1.png
    8.1 KB · Views: 22
Tusidanganyane hapa,hizi nyumba kama fundi ni mzuri hazivuji zikiwa mpya,ila tu baada ya miaka mingi huwezi kukataa kuvuja kwakuwa kuna sehemu bati linakutana na ukuta au tofali direct,baadaye kinachokuja haraka ni kutu na bati kuoza haraka sana.Nimeishi nyumba za wahindi au NHC nyingi tatizo ni kuoza mabati kule mwishoni,na kumbuka miaka ile bati zilikuwa ngumu na nzito sana,sasa kwa haya ya geji 30 tunayoweka kubana matumizi lazima ulie tu...
 
Mkuu ulitumia fundi wa kawaida?

Mimi ni mjenzi profesheno nione nikushauri tu hutojuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…