Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Twende sawa uislamu ulianza lini?na ukristo nauyahudi ulianza lini?mwenye akili timamu atajua tu uislamu ni falsafa mfu ya kukopi na paste kati ya ukristo na uyahudi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja kidogo nichangie hapa,,story ilianza Abrahamu anahamia caanan,akitokea Ur ya mesopotamia,today iraq,
Huko caanan anakutana na mfalme,Melikizedek,ambayo actually ni title yenye maana mfalme mtukufu,
Huyo mfalme ni kuhani wa Mungu mkuu alieabudiwa na jamii yote ya caanan,Mungu huyo aliitwa El..
Kiufupi Abraham,ambae nae kiukweli hakupata kuwepo,anakua introduced katika imani ya kumuabudu El,
Abrahama anazaa mtoto wa kwanza anampa jina, Ishmael.
Ishma-kusikia.
El-Mungu
Maana yake "Mungu kasikia"
Mpaka hapo hakuna uyahudi,Abraham anaabudi mungu wa caanan aitwae El,
Pia twaona ,Abraham akikutana na mfalme wa filstian,maeneo ya gaza,king Abimelech.
Ambayo nayo ni title.
Abi-Abu=mwana.
Melech-malik=mfalme,
Yaani, Mwana wa mfalme
Kimombo tuite Prince.
Abrahamu anataka kumuuza mkewe sara kijanja alalwe na mwana wa mfalme,
Mungu,yaani El akamwotesha Abimelech kuwa yule si dada wa abraham bali mkewe,
Automatically hapa Abimelech haongei na yahwew,ameoteshwa na mungu aliemuabudu yaani El,
Hii inaonyesha Abraham amekuta jamii ya caanan inaabudu mungu El.
Jina israEl linabeba Mungu wa caanan,,yaani El ambae ndo alikua Mungu mkuu,the most high.
Utafiti wangu sasa,to cut the story short,
El ndoo huyohuyo Allah.
Katika maandiko ya kiyahudi utakutana na jina,,,ABDIEL lenye maana sawa na jina ABDALLAH.
Maana yake ni moja,"Mtumishi wa mungu"
Hivyo El na Allah kitu kimoja ila matamshi yakatofautiana kufuatana na jamii,sawa na jina,
Abimelech=Abumalik=Mwanamfalme,
Mungu wa israel ndo huyo huyo mungu wa waarabu.
Kiufupi mungu ni mmoja tu,,dini zinazengua tu.🏃🏃🏃🏃🏃🏃
 
Twende sawa uislamu ulianza lini?na ukristo nauyahudi ulianza lini?mwenye akili timamu atajua tu uislamu ni falsafa mfu ya kukopi na paste kati ya ukristo na uyahudi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mitume wote ni Waislamu.

Uyahudi haijulikani hasa ulianza lini wapo wanao sema baada ya nabii Suleyman,wapo wanao sema baada Musa,lakini kipindi cha nabii Musa Uyahudi haukuwepo.

Ukristo umeanza baada ya kuondoka nabii Issa kuondoka.
 
Nazidi kucheka sababu unaonekana hujui kusoma Qur'aan.

Nionyesha hiyo sehemu katika aya hakuna hiyo sehemu. Tena ukisoma matini ya aya kuna tamko "Aslaam".

Nimekupa kazi kwanini umeweka kipande cha matini ya aya ukaacha matini ya mwanzo ambayo imeongelea Taurati na Kiislamu ?

Ukimuita mwenzako anayejua kusoma atakucheka. Yaani kijana una vituko balaa. Someni aisee.
Kujadili jambo na watu kama nyinyi ambao mmeishalishwa uislamu na ukristo ni kupoteza muda. Dini ni ujinga.
 
Kujadili jambo na watu kama nyinyi ambao mmeishalishwa uislamu na ukristo ni kupoteza muda. Dini ni ujinga.
Highlight hiyo matini.

Hatulei ujinga,najua hujui kusoma Qur'aan achilia mbali Kiarabu. Sasa onyesha toka kwenye aya.

Hii tabia ya uongo na uzushi nataka kuikomesha,na nyinyi hamsoni hili limethbitika wazi kabisa.

Sasa ukitaka kuujadili Uislamu unatakiwa uusome hasa. Kinyume chake utaonekana kituko kama ulivyo onekana hii leo.
 
wayahudi wanatumika na ma aliens...ukisoma kitabu cha ezekiel kimeelezea mpaka ndege zao (UFO) pay attention to details.
 
UTANGULIZI
Masiku yamepita huku nikitamani sana kuandika chochote kuhusu Uyahudi na Wayahudi. Kuandika kuhusu chimbuko lao, kuandika kuhusu uhusiano wao na wana wa Israeli,kuandika kuhusu itikadi zao, kuandika kuhusu madai yao kwa nabii wa Mola muumba Musa mwana wa Imraan mwana wa Quhaata mwana wa Lawi mwana wa Yaqoub mwana wa Is'haak mwana wa Ibrahiim.

Lakini kalamu zimeshanyanyuka na wino umeshakauka na historia iliandikwa kitambo sana na wakubwa zetu kwa ubora, wakubwa zetu kwa maarifa na wakubwa zetu kwa umri, na nachokifanya mimi ni kurejea kwao na wala sitaandika jipya ambalo wao hawakuliandika,yaani kwa ufupi sitazua.

Maneno nitakayo yahudhurisha kwenu katika mfululizo wa anuani hii "KUYAFUNUA YALIYO FUNIKWA" ni natija au zao la utafiti wangu wa muda mrefu juu ya historia ya watu hawa. Lakini marejeo yangu hasa hasa yamemili katika vitabu viwili, ambavyo nitavitaja mwishoni mwa mada hii, yaani nikiwa nahitimisha somo hili.

Nini maana ya Uyahudi?
Katika kudurusu tamko hili la "Uyahudi" nitapita katika mapito mawili tofauti, pito la kilugha na pito la kiistilahi.

Maana ya Uyahudi kilugha
Wametofautiana wanazuoni juu ya tamko hili, wapo wanaosema tamko hili limetokana na lugha ya kiarabu katika tamko "al Huud" lenye maana ya toba (kutubia) na kurejea katika utiifu (kutokana na maovu aliyo yafanya mtu).

Wengine wakakataa na kusema hakika tamko hili si lenye asili ya Kiarabu, bali limetokana na mmoja wa watu kutoka katika ukoo (uzao) wa wana wa Israeli naye si mwingine bali ni "YAHUUDHA" (Huyu tutamuelezea kwa undani huko mbeleni) au tamko "Uyahuud/Yahuud" limetokana na ile dola iliyo anzishwa kusini mwa nchi ya Palestina baada kupita nabii Suleyman na hii ndiyo kauli yenye nguvu.

Maana ya Uyahudi kiistilahi
Uyahudi kiistilahi maana yake ni wale watu wanao dai ya kuwa wana mfata nabii Musa.

Sehemu ya pili post #28

Sehemu ya tatu post #113

Tofauti na Mahindu na Mabudha hawa hawajinasibishi na mtume yeyote ila Mayahudi wanajinasibisha na nabii Musa hali ya kuwa hawana uhusiano wowote na nabii Musa,hili nitalithibitisha huko mbeleni panapo majaliwa.
Hapo kwenye red, kwani Musa aliongoza akina nani toka Misri?
 
Mitume wote ni Waislamu.

Uyahudi haijulikani hasa ulianza lini wapo wanao sema baada ya nabii Suleyman,wapo wanao sema baada Musa,lakini kipindi cha nabii Musa Uyahudi haukuwepo.

Ukristo umeanza baada ya kuondoka nabii Issa kuondoka.
Kwani Quran Tukufu inasemaje kuhusu Uyahudi, kwamba ulianza lini?
 
Kwani Quran Tukufu inasemaje kuhusu Uyahudi, kwamba ulianza lini?
Hakuna katika Qur'aan aya inayo wazungumzia Mayahudi ila kwa ubaya.

Haijulikani lini hasa Uyahudi ulianza wapo wanao sema kipindi cha nabii Musa na wapo wanao sema baada ya utawala wa nabii Suleyman.
 
Hakuna katika Qur'aan aya inayo wazungumzia Mayahudi ila kwa ubaya.

Haijulikani lini hasa Uyahudi ulianza wapo wanao sema kipindi cha nabii Musa na wapo wanao sema baada ya utawala wa nabii Suleyman.
Itakuwaje katika Qur"aan hakuna haya ya kuzungumzia Mayahaudi wakati, Qur'aan haijaacha chochote?
 
Itakuwaje katika Qur"aan hakuna haya ya kuzungumzia Mayahaudi wakati, Qur'aan haijaacha chochote?
Qur'aan haijaacha kitu kwa maana ya muongozo,ndiyo maana hukuti katika Qur'aan namna ya kupika ugali,ila katika Qur'aan utakuta namna kuutafuta ukweli,kuishi na watu kwa wema kuepuka maasi na mfano wa hayo.
 
So, Musa (Muislamu) aliongoza Wasiowaislamu (Makafiri) toka Misri kwenda nchi ya Kanaani?
Hii ndiyo maana ya Mtume. Musa alio waongoza ni wafuasi wake na wafuasi wa Musa ni Waislamu. Bali Musa alipelekwa kwa Makafiri,katika hao Makafiri wapo walio muamini na kumfata Musa hawa ndiyo huitwa Wafuasi wa Musa ambao nao ni Waislamu.
 
Hakuna katika Qur'aan aya inayo wazungumzia Mayahudi ila kwa ubaya.

Haijulikani lini hasa Uyahudi ulianza wapo wanao sema kipindi cha nabii Musa na wapo wanao sema baada ya utawala wa nabii Suleyman.
uyahudi ulianza baada ya kifo cha sulemani, na ilikua ni matokeo ya kutengana kwa makabila 12 ya israel ambapo makabila 11 yaliunga na kuendelea na jina la israel na makao yake makuu yakawa Samaria, kabila la yuda likasimama kivyake na makao yake makuu yakabaki yerusalem....

ko utengano ulikuja kimaeneo na wala sio kidini na kiutamaduni na kabila la yuda liliendelea kuishika torati ya musa iliyo kuwa na mambo ambayo mungu aliwaamuru israel, ko yuda na israel waliendelea kuabudu katika dini ile ile ya musa...

Na utengano huo ulitokea kama adhabu kwa suremani baada ya kushirikiana na wake zake katika ibada ya miungu yao
Ila israel ilikuja kufanya machukizo makubwa na kuziacha njia za bwana hali iliyopelekea mungu kuwatia mikononi mwa adui na adui alichokifa ni kuzaliana nao kuharibu asili yao

ko torati ya kweli ikabaki kwa kabila la yuda na muisrael ikawa ni mwiko kuchangamana na kabila la yuda rejea ilivyokuwa ajabu kwa yesu kumuomba maji binti msamaria

kwahiyo huwezi sema kwamba wayahudi ikimaanisha watu wa kabila la yuda hawana uhusiano na israel na haiwezekani kuutenganisha uyahudi na torati ya musa
 
kwahiyo huwezi sema kwamba wayahudi ikimaanisha watu wa kabila la yuda hawana uhusiano na israel na haiwezekani kuutenganisha uyahudi na torati ya musa
Hapa ndipo tatizo lilipo. Uyahudi ni dini na si kabila.

Mayahudi hawaingiliani na Musa,bali Mayahudi wabajinasibisha na nabii Musa tunasema wanajikomba huku wakibadilisha mafundisho ya nabii Musa.
 
Back
Top Bottom