Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Unakuta kijana amezaa akiwa na umri mdogo, na kuanza kubeba majukumu mazito ndani ya umri mdogo, ata maisha anakuwa hajayafurahia.

Mbaya zaidi anazaa watoto wengi, inayopelekea katika maisha yake yote ya ujanani mpaka uzeeni anaishi kwa kuteseka, kwa kugharamia familia kwenye mahitaji na elimu.

Ukitaka kushuhudia hili, mtazame mwenzako au ata jirani yako hapo mtaani, hawana furaha kabisa, wote wanawaza mwezi januari watavukaje.

Ile ya kusema kila mtoto anakuja na bahati yake hiyo haipo siku hizi, we zaa angalau ukiwa na miaka 40+, ndio maana wenzetu nje wanazaa watoto 2 au 1.​
Hatufanani na hivyo mifumo ya maisha yetu pia hatofanana kamwe!
 
Wewe unamjua mtoto mkubwa wa P funk unamjua mtoto wa lowasa, unamjua mtoto wa amani karume yule shangazi, unamjua mtoto Gardner, unamjua mtoto mkubwa wa ruge, unamjua mtoto mkubwa wa dudu baya wewe kuza before 26 kuna raha yake😬lakini sishauri
Raha ipi??? Tunajaribu kuziishi falsafa za kizazi Cha tatu kilichopita wakati mazingira hayaruhusu.

Utafutaji umekuwa mgumu na gharama za kutunza familia ni kubwa sana, ukienda na huo ushamba wa kuzaa kwa kufata mkumbo unazeeka na hauna chochote unabaki kusubiri bahati watoto wakusaidie.
 
Hizo ni theory tu mkuu mda wowote tu kina happen nilitamani kuzaa under 25🥶Ila huo umri ukapita
Sio theory mkuu ndio maana kwenye practical wewe ulishindwa. Ndio maana wataalamu wakaja na hitimisho kwamba umri ambao mwanaume anakua yuko kikamilifu kua na familia ni kuanzia miaka 30.

Ila kuzaa tu unazaa baada ya kubalehe miaka 12 hadi 15 unazaa tu.
 
Unakuta kijana amezaa akiwa na umri mdogo, na kuanza kubeba majukumu mazito ndani ya umri mdogo, ata maisha anakuwa hajayafurahia.

Mbaya zaidi anazaa watoto wengi, inayopelekea katika maisha yake yote ya ujanani mpaka uzeeni anaishi kwa kuteseka, kwa kugharamia familia kwenye mahitaji na elimu.

Ukitaka kushuhudia hili, mtazame mwenzako au ata jirani yako hapo mtaani, hawana furaha kabisa, wote wanawaza mwezi januari watavukaje.

Ile ya kusema kila mtoto anakuja na bahati yake hiyo haipo siku hizi, we zaa angalau ukiwa na miaka 40+, ndio maana wenzetu nje wanazaa watoto 2 au 1.​
Mkuu kila jambo lina faida na hasara, shuhuda akiwa ni mimi.

Nimeoa na hiyo 40 unayotaka wewe, nimestaafu nikiwa na kachanga ka kustaafia na watoto 3 wakiwa Sekondari.

Walio oa mapema na kubeba majukumu mapema wapo vizuri kuliko sisi tulochelewa.

Ntaendelea kuwa mlishi hadi nazikwa.
 
Faida ya kuzaa mapema ni kuhangaikia watoto ukiwa bado na nguvu na pesa. Umri ukienda ni vigumu kutafuta pesa na wakati huo watoto wanahitaji karo na mahitaji mengine.
Huu mfumo umeshashindwa sio mfumo sahihi tena wa maisha.

Huu mfumo umezalisha watoto wa mtaani wengi, masikini wengi, wajinga wengi n.k kwasababu watu wanazaa kutimiza wajibu tu nayeye aonekane anae mtoto ila kiuhalisia hakupaswa kabisa kuwa na mtoto kwasababu hawezi kumpa mahitaji muhimu kama malezi Bora, afya, makazi bora, elimu bora n.k
 
Miaka 40 unapiz nini kama sio upepo
Mnachekesha vijana wadogo, mimi am 44yrs, na nipo fire vibaya sana, siri kubwa nafanya mazoezi makali,nakunywa tangawizi,mdalasini,karafuu, na kingine karanga kwa sana,na vyakula vya proten,

Maji ndio starehe yangu pia, kwa mwanaume miaka 40 bado sana, labda nyie kwakuwa hamtafikia umri huu tulionanao,siwezi ongea sana maana hutoelewa, Mungu ajalie mfe mkuwa wadogo ivyo ivyo,maana mnatusimanga sana wapuuzi nyie(joking)
 
Back
Top Bottom