Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Mkuu kila jambo lina faida na hasara, shuhuda akiwa ni mimi.

Nimeoa na hiyo 40 unayotaka wewe, nimestaafu nikiwa na kachanga ka kustaafia na watoto 3 wakiwa Sekondari.

Walio oa mapema na kubeba majukumu mapema wapo vizuri kuliko sisi tulochelewa.

Ntaendelea kuwa mlishi hadi nazikwa.
Hujafikiria tu vizuri, nguvu unayotumia wewe kulea familia yako ni tofauti na kijana wa miaka 30 mwenye watoto watatu.

Wewe unalea watoto ukiwa na umri ambao sio wa mihemko, huna mambo ya ujana focus Yako inakuwa kwenye makuzi ya wanao ni tofauti na hawa watoto wa saivi wanalelewa na mtaa kwasababu wazazi wao wapo bize kutafuta maisha.

Kuzaa uzeeni sio shida kama watoto wanapata mahitaji muhimu kama elimu bora, Afya, makazi bora n.k
 
Mnachekesha vijana wadogo, mimi am 44yrs, na nipo fire vibaya sana, siri kubwa nafanya mazoezi makali,nakunywa tangawizi,mdalasini,karafuu, na kingine karanga kwa sana,na vyakula vya proten,

Maji ndio starehe yangu pia, kwa mwanaume miaka 40 bado sana, labda nyie kwakuwa hamtafikia umri huu tulionanao,siwezi ongea sana maana hutoelewa, Mungu ajalie mfe mkuwa wadogo ivyo ivyo,maana mnatusimanga sana wapuuzi nyie(joking)
Sasa chukua hii mzee wangu kami Pata akiwa 44 of age nilimsumbua sana enz za kusoma, pia kingine incampibility ya kulea watoto at that age tuisijifananishe na wazungu mtu ana hadi daktari wa lishe haya probability ya kupata ajali ni ndogo mwenzetu wana four ways plus fly overs Sasa uwezekano wa kuishi muda mrefu upo haya uwekezaji wao pia,

Kibongo, unastaafu huna Ata hisa, bonds, unategemea biashara mwishowe unakufa kwa stress
 
Unakuta kijana amezaa akiwa na umri mdogo, na kuanza kubeba majukumu mazito ndani ya umri mdogo, ata maisha anakuwa hajayafurahia.

Mbaya zaidi anazaa watoto wengi, inayopelekea katika maisha yake yote ya ujanani mpaka uzeeni anaishi kwa kuteseka, kwa kugharamia familia kwenye mahitaji na elimu.

Ukitaka kushuhudia hili, mtazame mwenzako au ata jirani yako hapo mtaani, hawana furaha kabisa, wote wanawaza mwezi januari watavukaje.

Ile ya kusema kila mtoto anakuja na bahati yake hiyo haipo siku hizi, we zaa angalau ukiwa na miaka 40+, ndio maana wenzetu nje wanazaa watoto 2 au 1.​
Hio 40 kuikamata siku hizi nayo mtiti people are dying at 20s to 30s
Unazaa at 40s unakufa at 50s watoto hawana direction yoyote
 
Unakuta kijana amezaa akiwa na umri mdogo, na kuanza kubeba majukumu mazito ndani ya umri mdogo, ata maisha anakuwa hajayafurahia.

Mbaya zaidi anazaa watoto wengi, inayopelekea katika maisha yake yote ya ujanani mpaka uzeeni anaishi kwa kuteseka, kwa kugharamia familia kwenye mahitaji na elimu.

Ukitaka kushuhudia hili, mtazame mwenzako au ata jirani yako hapo mtaani, hawana furaha kabisa, wote wanawaza mwezi januari watavukaje.

Ile ya kusema kila mtoto anakuja na bahati yake hiyo haipo siku hizi, we zaa angalau ukiwa na miaka 40+, ndio maana wenzetu nje wanazaa watoto 2 au 1.​
Unastaafu au unafikia umri wa kustaafu na mtoto miaka 5. Unaulizwa huyu ni mjukuu au mtoto ? Kibaya zaidi first born anakuwa hajamaliza hata degree.
 
Africa kuzaa ni fashion na kufata mkumbo tu. Usipokua na watoto utachekwa ila hao watoto wakikosa mahitaji muhimu huchekwi inaonekana ni kitu cha kawaida tu.

Kuzaa hakukunufaishi chochote wakati wa malezi zaidi ya kuongeza majukumu, kabla hujazaa tambua unakwenda kujiongezea majukumu na ujiandae kukabiliana nayo.

Unakuta umekaa zako huna hili wala lile mara mshikaji anakucheki anaomba umuazime 30k mke ameenda kujifungua, ukimcheki jamaa ana miaka kama 25-26 hivi. Unajiuliza huyu jamaa anawahi nini? kama hata 30k kakosa hao watoto watapata matunzo kweli?

Kama huwezi kumudu mahitaji na malezi ya watoto usizae watoto waje kuwa ombaomba na kutaabika kwa starehe zako za kijinga.
 
Huu mfumo umeshashindwa sio mfumo sahihi tena wa maisha.

Huu mfumo umezalisha watoto wa mtaani wengi, masikini wengi, wajinga wengi n.k kwasababu watu wanazaa kutimiza wajibu tu nayeye aonekane anae mtoto ila kiuhalisia hakupaswa kabisa kuwa na mtoto kwasababu hawezi kumpa mahitaji muhimu kama malezi Bora, afya, makazi bora, elimu bora n.k
Kama mtu kaoa kwa umri mdogo unaokubalika, si shida labda kama yuko chini ya miaka 18. Faida nyingine kuzaa watoto timamu, kuliko ukiwa umri umeenda unazaa vilema.
 
Mnachekesha vijana wadogo, mimi am 44yrs, na nipo fire vibaya sana, siri kubwa nafanya mazoezi makali,nakunywa tangawizi,mdalasini,karafuu, na kingine karanga kwa sana,na vyakula vya proten,

Maji ndio starehe yangu pia, kwa mwanaume miaka 40 bado sana, labda nyie kwakuwa hamtafikia umri huu tulionanao,siwezi ongea sana maana hutoelewa, Mungu ajalie mfe mkuwa wadogo ivyo ivyo,maana mnatusimanga sana wapuuzi nyie(joking)
Bila hata joking, 44 ni kijana mdogo bado, haujafikia hata kuitwa 'wa makamo'.

Na kwa mwanamke umri huo sasa, wanapendeza sana kuliko wasichana wakiwa kwenye kilele cha kuelekea kuyaaga mambo yetu yaleee, basi wanakuwa ni vipusa kishenz, chaguo la kila mwanaume!
 
Africa kuzaa ni fashion na kufata mkumbo tu. Usipokua na watoto utachekwa ila hao watoto wakikosa mahitaji muhimu huchekwi inaonekana ni kitu cha kawaida tu.

Kuzaa hakukunufaishi chochote wakati wa malezi zaidi ya kuongeza majukumu, kabla hujazaa tambua unakwenda kujiongezea majukumu na ujiandae kukabiliana nayo.

Unakuta umekaa zako huna hili wala lile mara mshikaji anakucheki anaomba umuazime 30k mke ameenda kujifungua, ukimcheki jamaa ana miaka kama 25-26 hivi. Unajiuliza huyu jamaa anawahi nini? kama hata 30k kakosa hao watoto watapata matunzo kweli?
Uchumi ukitengenezwa vizuri kuzaa ni muhimu, hata 10 zaa tu
 
Unastaafu au unafikia umri wa kustaafu na mtoto miaka 5. Unaulizwa huyu ni mjukuu au mtoto ? Kibaya zaidi first born anakuwa hajamaliza hata degree.
Wakikuuliza hivyo inakuondolea uhai????

Huo ni ushamba wa kiafrika. Utamkuta mtu ambae hana uhakika hata wa mlo kwa familia yake, anamcheka mtu ambae amezaa umri umeenda ila anao uwezo wa kumpa mwanae kilakitu anachohitaji. Sasa nani mjinga hapo?
 
Bila hata joking, 44 ni kijana mdogo bado, haujafikia hata kuitwa 'wa makamo'.

Na kwa mwanamke umri huo sasa, wanapendeza sana kuliko wasichana wakiwa kwenye kilele cha kuelekea kuyaaga mambo yetu yaleee, basi wanakuwa ni vipusa kishenz, chaguo la kila mwanaume!
Kujisifu tu ujinga broo 44 Unatakiwa na mtoto s chini ya miaka 18 hyo ndo awe first born
 
Back
Top Bottom