Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Wakikuuliza hivyo inakuondolea uhai????

Huo ni ushamba wa kiafrika. Utamkuta mtu ambae hana uhakika hata wa mlo kwa familia yake, anamcheka mtu ambae amezaa umri umeenda ila anao uwezo wa kumpa mwanae kilakitu anachohitaji. Sasa nani mjinga hapo?
Kipato kikiruhusu zaa kwa fujo. Eneo letu Africa ni kubwa kuliko idadi ya watu ukilinganisha na China. Ni sahihi kwanza uchumi lakini kuzaa muhimu sana.
 
Vijana mkome kutusimanga na kutuita wazee sisi wenye umri miaka 40+
 
Kama mtu kaoa kwa umri mdogo unaokubalika, si shida labda kama yuko chini ya miaka 18. Faida nyingine kuzaa watoto timamu, kuliko ukiwa umri umeenda unazaa vilema.
Watoto wenu timamu mliowazaa mapema ndio masikini ila hao wanaozaliwa wazazi umri umeenda na wakapata mahitaji yote muhimu maisha yao ni mazuri.
 
Kipato kikiruhusu zaa kwa fujo. Eneo letu Africa ni kubwa kuliko idadi ya watu ukilinganisha na China. Ni sahihi kwanza uchumi lakini kuzaa muhimu sana.
Uzae kwa fujo kwa masirahi ya nani??? Unanufaika nini?? Zaa watu ambao unaweza kumudu mahitaji yao na kuwamonitor makuzi yao, malezi yao, afya yao, elimu, talent n.k. Africa tunafanya mambo ya Msingi kimasihara sana
 
Miaka 40 utazaa wehu tupu Dogo
 
Ukifa kabla ya hio miaka 40+ itakuwaje na huna mtoto acha watu wazae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…