Kuzaa watoto wengi bila mpango mkakati wa kuwalea utahukumiwa

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Hakuna idadi ya watoto utakaozaa useme umezaa wengi. Kwa Mwingine watoto wengi kwao ni mmoja. Mwingine kama yule mzee mjaluo wa shirati, watoto wengi ni 38 na mwingine watoto wengi ni 0.

Kipimo cha wingi sio idadi bali uwezo wa kuwahudumia na kuwapa malezi yaliyonyumbuka pote kwa usawa bila upendeleo.

Kama unaona huna muda wa malezi au huna uwezo wa kuhudumia ni afadhali msizae.

Ukizaa watoto ambao hauna utayari wa kuhudumia kimalezi na kimahitaji Mwenyezi Mungu atakuhukumu
kwa kosa la kuijaza dunia na Majambazi, makahaba, watu waliopinda wasio na maadili, ombaomba na utatakiwa kujieleza.

Fikiria au kubalianeni kabla ya kuoana. Kama hamuwezi na mko bize msizae, Mle maisha wenyewe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…