Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Arabi ni kwamba wenye uwezo mkubwa kiuchumi hawana utitiri wa Watoto....!!
 
Hua sipanic mkuu,
Nimekuelekeza kazi ya uumbaji ni ya mungu, na kazi ya kuendeleza kizazi ni ya mungu, wewe na wengine tunetunikiwa tu nafasi ya kushiriki katika uumbaji huo,

Haimaanishi wote tukikataa kuzaa basi kizazi kitakufa, mungu anaweza tafuta namna nyingine ya kukiendeleza kizazi kama tukiwa wajeuri kama ulivo wewe,

So uzae au usizae, mungu hapungukiwi na kitu wala hauongezekiwi na kitu

So kuendeleza kizazi sio choice, kitaendelea tu hata usipozaa.

Ila faida za watoto zipo nyingi, wewe endelea kukataa kuzaa halafu rudi kwenye huu uzi 20-30 yrs uone umemiss nn kwa kutokuzaa
 
Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Nature. Ni ecosystem, ukienda darasani ukajifunza utaelewa. Kila kilichomo hapa duniani, mchwa, konokono, Simba, jongoo, tembo, panzi, chura, binadamu, miti, maua, majani vimo kwenye mfumo huo.
 
Kuzaa ni njia mpya ya kuhamisha genes kuendelea kubaki duniani. Viumbe wote ni watumwa wa genes. Ningeelezea mengi ila niishie hapo kwa leo.

Viumbe huzaa pale wanapokuwa wana resource za kutosha mfano chakula. Na viumbe huzaa watoto wengi pale inapokuwa chance of survival is low to compasate vifo ila population ipo at equilibrium. Mfano Sasa hivi hatuzai sana maana hatufi sana hence resources zipo chache na population is stable tukizidisha tuu vifo vitatokea vingi sana
 
Kuzaliana ni njia ya kuzifanya "genes" na viumbe kuendelea kuwepo duniani. Genes zako automatically zinataka kuendelea kuwepo duniani hivyo zinakusukuma wewe chombo uliyezibeba au kiumbe kingine chochote pia ambacho ni chombo cha genes kufanya uzazi.
Umejibu kwa mhemuko, swali ni kiumbe yyoyote yule anapata faida gani akizaa mtoto. Achana na kujikita kwa binadamu tu.

Yaani kwa mfano, ule mwembe unazaa maembe ambayo ndani yana mbegu ambazo zikiota zinakuwa mwembe mwingine. Sasa ule mwembe uliozaa maembe unapata faida gani endapo lile tunda la embe litaota na kuwa mwembe?

Mnyoo jnapata faida gani ukizaa kimnyoo kingine kidogo?


Mjusi anapata faida gani akizaa kamjusi kengine kadogo? Nk
 
Kwa sababu ni "copy" yake ilyobeba sehemu kubwa ya "genes" zake na hivyo ni chombo kitakachohakikisha genes zake zinaendelea kuwepo duniani. Hivyo ndivyo upendo kwa ndugu wengine wa karibu unavyotokea pia.

Kadri undugu wa damu unavyokuwa wa karibu ndivyo kujali huyo mtu kunavyoongezeka kwa sababu anakuwa na genes asilimia kubwa zinazofanana.
Upo sahihi coz ni kama betting unaweza zaa mtoto na akaja kuwa liability.

But why kunakiwa na upendo kati ya mzazi na mtoto.?
 
Nimekuwa najiuliza sana hili swali. Nakumbuka mara ya kwanza kuwaza hivi nilimuuliza mama. Nikasema sisi lengo letu nini? Bibi kamzaa mama, bibi anazeeka anakufa. Na mama anatuzaa sisi, nae atazeeka na atakufa vile vile. Na mimi naanza kupambana na mihangaiko ya maisha kisha nazaa watoto. Then what?


Kama mleta maada alivyosema, labda kama tungekuwa hatufi ingeleta maana.
Kama watu wa BC hakuna wanachofaidika na kizazi hiki ya nini kuzaana? Si tustop biashara kichaa iishie hapa?

au sisi tumefungwa na kitu fulani ambacho lengo lake ni kitoweo. Kama vile sisi tunavyofuga kuku.

Inafikilisha kwa kweli forget wandugu.
Kama unaona hamna faida, usizae na wala usihangaike na mambo ya utelezi. Kwa ufupi kizazi chenu kikomee kwako
 
Back
Top Bottom