Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.
Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.
Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.
Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .
Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .
Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.
Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3
Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu huku gesi tunaibiwa, Tanzanite tunaibiwa, kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.
To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo kwa Watanzania kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .
Paskali