Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Ivi mnawezaje kuzuia wakati mna mikataba na wawekezaji???.. Acacia wanalalamika wamepata hasara ya 40b kwa 2 wks toka order imetolewa...
Kesho wakienda mahakamani tunawalipa hela nyingi kwa kuvunja mikataba.
Kwa nini kama serikali wasikae hao wawekezaji waone wanachaweza kupata na mwisho kuboresha maslahi ya wa Tanzania kwenye kupata ajira...
Hii awamu italeta kesi nyingi saana na tutashindwa wote kwenye mahakama za kimataifa!.
Kikwete alipoingia alikuta mrahaba wa madini ni 3%..ila mbona hakufunga migodi zaid walikaa na kuangalia kuwa tunapunjwa.
Kufunga/kuzuia bado hujatoa suluhisho maana watu wamewekeza saana kwenye hizi shughuli!..
Sheria za kimataifa zinaruhusu kupitia upya mikataba.hiyo ndo best way.
Maana kama kuzuia ilishawahi kuzuiliwa
Tuwe na sera na sio kukulupuka kufanya maamuzi bila kuangalia athari zake!.
Kumbe ww mwezetu unaujua huo mkataba?
 
Ndio maana magu kasema atayafungua Yale makontena baada ya taratibu kukamilika ili Tanzania , Africa na dunia ione..hajakurupuka faiza
Mule ndan huenda kuna dhahabu asilimia kubwa zaid ya mchanga[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Yafunguliwe
 
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu huku gesi tunaibiwa, Tanzanite tunaibiwa, kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.
To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo kwa Watanzania kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
Kati ya vitu ulivotudanganya ni nchi zenye hzo smelters. Waandshi wetu mmezd kukurupuka. Tulien fanyen utafit,hamna haja ya kuwa na haraka. Nenda ufanye utafiti urudi tena na list ya nchi zenye smelter.

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
 
Anybody with basic knowledge of chemistry utafiti wa dakika chache kwenye mtandao angefahamu sababu msingi mchanga kusafirishwa nje - surely Phd chemistry with a difference.
 
Mule ndan huenda kuna dhahabu asilimia kubwa zaid ya mchanga[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Yafunguliwe
Sio huenda, wanachimba na ku semi process kwa kusaga tuu na sio mchanga bali ni makinikia ya dhahabu.

Paskali
 
Lengo ni zuri tatizo ni ukurupukaji. Hili zoezi lilihitaji majadiliano baina ya pande 2. Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa zuio hili chini ya JPM. Mara ya kwanza lilifeli.

Kuchenjua madini kunahitaji uwekezaji mkubwa wa mitambo. Hivyo wawekezaji walipaswa kupewa muda mf miezi6 au mwaka kwa makubaliano ya pande zote 2. Huku kukurupuka ni sawa na zoezi la Viroba. Hakuna muda wa mpito kwa Mwekezaji.

Naskia migodi imesitisha mikataba na kampuni zote, wafanya kazi wote wamesimamishwa kazi, mafunzo yote yamesitishwa, nk. Kodi tunapoteza, ajira kwa watu wetu zinapotea, biashara za jirani zina athirika, nk.
 
Tukumbuke kuwa kuna sheria na kanuni za mikataba, hazitubani?

Pia tukumbuke kisa cha Tiny Rowlands na Nyerere.
Dhahabu ni yetu na mchanga hautoki, hakuna cha sheria ya mikakataba wala mikakataba ya uwekezaji, tumesema wajenge smelter hapa na wauchambulie hapa hapa, kama hawataki wafungashe wakwende zao, tutaichimba dhahabu yetu wenyewe tukiisha jenga uwezo. ICCD tunajitoa na hatusikilizi kesi yoyote wala hatutaki usuluhisho wowote kwenye rasilimali zetu! .
Nimemshauri tukifanikisha hili la dhahabu tuje na kwenye gesi maana nako tunaibiwa! .
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Paskali
 
Dhahabu ni yetu na mchanga hautoki, hakuna cha sheria ya mikakataba wala mikakataba ya uwekezaji, tumesema wajenge smelter hapa na wauchambulie hapa hapa, kama hawataki wafengashe wakwende zao, tutaichimba dhahabu yetu wenyewe tukiisha jenga uwezo. ICCD tunajitoa na hatusikilizi kesi yoyote wala hatutaki usuluhisho wowote kwenye rasilimali zetu! .
Nimemshauri tukifanikisha hili la dhahabu tuje na kwenye gesi maana nako tunaibiwa! .
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Paskali

Safi sana, tukumbuke tu ya Nyerere na Tiny Rowlands. Ilitunyeeshea.
 
Lengo ni zuri tatizo ni ukurupukaji. Hili zoezi lilihitaji majadiliano baina ya pande 2. Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa zuio hili chini ya JPM. Mara ya kwanza lilifeli.

Kuchenjua madini kunahitaji uwekezaji mkubwa wa mitambo. Hivyo wawekezaji walipaswa kupewa muda mf miezi6 au mwaka kwa makubaliano ya pande zote 2. Huku kukurupuka ni sawa na zoezi la Viroba. Hakuna muda wa mpito kwa Mwekezaji.

Naskia migodi imesitisha mikataba na kampuni zote, wafanya kazi wote wamesimamishwa kazi, mafunzo yote yamesitishwa, nk. Kodi tunapoteza, ajira kwa watu wetu zinapotea, biashara za jirani zina athirika, nk.
It's so sad, hizi papara na maamuzi ya kukurupuka is not very good at all kwenye investment climate.

Tuliwahi kushauri humu
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ukifanya jambo kwa papara with a negative preconceived ideas, then atakapokuja kuambiwa ukweli kuwa Tanzania hatuna umeme wa kuendesha hizo smelter za ku separate gold, silver and copper, sura itamshuka!.

Watu wana mikataba ya uwekezaji, sheria, taratibu na kanuni zipo, papara za nini? .

Paskali
 
Tukumbuke kuwa kuna sheria na kanuni za mikataba, hazitubani?

Pia tukumbuke kisa cha Tiny Rowlands na Nyerere.
Umenena kibibi gagula, kuzuia kisiasa kutaitumbukiza nchi hii kwenye madeni makubwa sana . hekima inafaa itumike maana hao watu kama mliingia nao mikataba mnafaa muelewe ni sheria na itatumaliza
 
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu huku gesi tunaibiwa, Tanzanite tunaibiwa, kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.
To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo kwa Watanzania kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
Kwasasa hivi wananchi wengi wanamuona Magufuli ni shujaa na wanampongeza kwa maamuzi yake ya kuzuia huo mchanga.. Lakini amini usiamini, soon Tanzania itasuffer na ikiwezekana kabisa kufunguliwa mashtaka kwenye mahakama za kimataifa kwa sakata hili.... Na hapo ndipo watu watakapomgeuka Rais na kuanza kujiuliza maswali yasiyo na majibu...
 
Kati ya vitu ulivotudanganya ni nchi zenye hzo smelters. Waandshi wetu mmezd kukurupuka. Tulien fanyen utafit,hamna haja ya kuwa na haraka. Nenda ufanye utafiti urudi tena na list ya nchi zenye smelter.

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
Usichanganye madawa, nimesema Tanzania haipo kwenye top ten gold producers, kwenye bara la África, South Africa na Ghana ziko kwenye top ten na hazina smelter of such magnitude, nikasema kwenye top ten, nchi 4 ndizo zenye hizo smelter, sasa what are the chances kwa Tanzania to have such a smelter, kwa dhahabu gani na kwa umeme gani? .

Ili Tanzania tuweze kuendelea ni lazima mkuu wetu apewe expert opinion kabla ya kutoa maamuzi ya kukurupuka ambayo mwisho wa siku yatakuja kuli cost taifa.

Mimi nimependekeza asaidiwe https://www.jamiiforums.com/threads...a-kitu-peke-yake.1224084/page-6#post-20343364

Umetaja nchi zenye smelters hata ulaya hamna ukataja china,urusi,japan na ukasema afrika hamna nchi yenye smelter.

Hili ndo naomba ulifanyie utafiti boss maana nyie waandsh tunawategemea sana.
 
Back
Top Bottom