Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Mkuu kwa hali ilivyo Sasa anauwezo wa kubadili katiba na kuongeza term za kuendelea kubaki madarakani.Nani ndani ya CCM atagoma akitaka kuendelea?katiba inabadilishwa na anaendelea kutawala
 
We jifariji tu. Kila mwenye akili timamu aliliona hili mapema tu. Huyu hatakaa achomoke. Labda Mungu mwenyewe aamue kumalizana nae.
 
Nyakati tofauti. Watu tofauti. Mazingira tofauti kabisa.

Hata akina Museveni na Kagame walikuwa wanasema hivyohivyo, lakini hatua walizokuwa wanachukua unaona kabisa wanajitengenezea grounds za kuongeza mihula. Nguvu kubwa anazotumia Jiwe kuonea. kuintimidate. kutoheshimu viapo alivyokula vya kutawala kwa fairness na kuheshimu katiba, Kuua civil socities, kusilence dissent, kuparalyse press,kujaribu kuua vyama vya siasa, kuwaondolea wananchi power ya kuweka viongozi madarakani kwa ridhaa zao (rejea uchaguzi serikali za mitaa, zile za marudio na uchaguzi mkuu wa juzi)kwa kutumia nguvu kubwa mithili ya mapinduzi ya Kijeshi ni dhahiri kuwa hayafanyi haya huku akijua kuwa ana miaka mitano au kumi tu ya utawala, ni dhahiri anaweka ground kwa utawala wa muda mrefu na hivyo lazima ahakikishe ameparalyse any credible resistance ya kumuwekea kikwazo njiani!

Kama kweli alikuwa hataki kuongeza Mhula basi angetumia rungu lake la Uenyekiti wa CCM kumzuia Ndugai asiwe Spika tena mtu aliyeonekana waziwazi kusupport idea ya kuondoa term limits ya miaka 10. Kwa kuwa Spika anakuwa nominated na Chama, na kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti basi ni dhahiri angeweza kuzuia chama kisimpe mtu anayeonekana ana mawazo yasiyo best kwa interest ya nchi. Ila unakumbuka alifanya nini juu ya Spika, Naibu Spika na Waziri mkuu kabla ya uchaguzi?-Aliwatungia sheria ya kuwapa Kinga nao wasishtakiwe kwa makosa watakayotenda kazini, Sasa huyu anawaz nini?

If It looks like a duck, walks like a duck, quack like a duck then it is a duck
Based on his actions (not words) we can infer that the man initends to change terms limits of the current constitution
 
Kugombea ni kitu kingine. Kuchapisha mamilioni ya kura feki kwa kushirikiana na NECCM na kuyaingiza katika vituo kwa mtutu wa bunduki ili ushinde uwe Rais wa kazi ambayo unasem ani mzigo mkubwa... kumewafedhehesha sana CCM na Magufuli. Ndio maana hawana nguvu ya kusherehekea kabisa.
1. Kama Jiwe anaona uraisi ni Mzigo kwa nini amegombea the second term?

2. Kama unadhani hawezi kuturudisha tulipotoka kwa nini anaturudisha tulipotoka in so many ways, repressive laws, moves za kuua upinzani, kuminya uhuru wa habari etc
 
Madicteta usiamini kauli zao. Ref. Hotuba ya kwanza ya Museven baadaya kuapishwa kwa mara ya kwanza Uganda.
 
Until it happens, my opinion will stay put.
 
Kuna vitu kuviona hadi uwe na third eye..
Uweze kuona future..

Binafsi naamini kama hataongeza mda atachagua mtu wake na kumlazimisha awe Rais..na inawezekana akawa worse than him
Au his puppet...

Sioni any bright future ambayo Magufuli atashiriki
 
Kwani akiongeza muda kuna ubaya gani
Acha aongeze tu

Ova
 
Kuna vitu kuviona hadi uwe na third eye..
Uweze kuona future..

Binafsi naamini kama hataongeza mda atachagua mtu wake na kumlazimisha awe Rais..na inawezekana akawa worse than him
Au his puppet...

Sioni any bright future ambayo Magufuli atashiriki
Nakubaliana nawe.

Atajitahidi kuweka ‘puppet’ wake.

At least that’s what I think...
 
Alishasema akiondoka yy hakuna wa kumalizia hyo mirad nadhan itapendeza akiwa hata mfalme
 
Uchaguzi umeisha tutegeme 2025 tanzania kuwa kama ulaya au SA ccm watakamilisha miradi yote
Lami mpk vichochororoni,afya tatizo watalimaliza
Maji hakutakuwa na shida
Uwanja umebaki na wao wenyewe sasa

Ova
Mmeanza kutafuta vijisabb vya kufufukia ile 2025???
 
Mkuu kwa hali ilivyo Sasa anauwezo wa kubadili katiba na kuongeza term za kuendelea kubaki madarakani.Nani ndani ya CCM atagoma akitaka kuendelea?katiba inabadilishwa na anaendelea kutawala
Mwinyi, Mkapa, Kikwete wote wana uwezo huo, hawakufanya hilo.

Tukisema wewe una uwezo wa kumtukana mtu, na tukuhukumu kwa sababu una uwezo huo, kabla hujamtukana mtu, hukumu hiyo itakuwa ya haki?
 
Ni kweli huwa anasimmamia maneno yake..
 
Confirmation bias. You just confirmed your biases.
Wewe ni kichocheo(katalisti) kama magadi yanavyo tumika katika kuivisha maharage yale magumu kuchemka ila nakueleza Mungu ankuona na wenzako wenye tabia hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…