INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

Biashara ya kurusha movie nimeifanya tangu mwaka 2011 mpaka 2014, baada ya hapo ikanipa connection ya kazi serikalini JPM alipo ingia madarakai msako wa vyeti feki ukaniondoa huko nikarudi kuifanya ndipo nikapata connectio kwenye kampuni ya wahindi , anay way ni story ndefu, naielewa changa moto zake, maswala ya kuliprishwa memory pale inapotafunwa na wadudu, mara computer kubooma, naona kwa sasa imenoka natamani kurudi tena kwenye biashara hii, ila miaka hiyo tulianza kwa ugumu kweli
ulikuwa unaingiza ngapi kwa siku.
 
Popote mkuu unaweza ifungua DODOMA hapo hapo nina plan yakuja fungua ofisi na ninavyoandika hapa wapo watu wenye movie store wakubwa tu hapo dodoma,tembelea ofisi zao utawaona wanachokifanya.

Kuna hawa wanajiita Cipherdot Series and Movies wapo mtaa wa Uhindini hapo nenda pale utawakuta utaona ofisi utaona uwekezaji uliofanyika.

Kuna huyu mwingine BABALAO mimi namuita hivyo na ndie ROLE MODEL wangu yeye anajiita BOBPAAK MOVIES huyu yupo mtaaa Mtendeni Street pale National Insuarance,Utawakuta hawa B.O.B wanajua biashara ilivyo na ukienda wagusa ukataka stock yao Bei utayotajiwa usipozimia basi unaweza kuzirai maana watu nmewatajia 4M wanahisi ni pesa ya kutishwa,sasa ukienda B.O.B bei zao n za mwana ukome.

Hao BOB PAAK nimewaona pia kinondoni studio na tabata
 
Mkoani ili u enjoy tafuta external za GB 250 au 300GB mbili kisha moja nakua nayo huku nyingine unakua nayo huko,ukimaliza hizo huko unaniambia nakutumia hii nyingine ikiwa na movie pendwa ulizontajia kwahyo external zinapshana hapo njiani, 250 inakuja kwako 300 inakuja kwangu,mchezo wetu unakua ni huo huo,Mpaka pale utakapo staafu kuangalia movie.
Ilinibidi nicheke tu,[emoji1] [emoji1787] [emoji23] [emoji38] [emoji1]

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
4m!!!!!
Nilikuwa nawaza kwa bajeti ya 1m kama mtaji wa soft movies na zile za kwenye CD ukiondoa mashine (CPU) na woofer ya kusikilizia
Hata kwa 500k unaanza inategemea tu unataka kuanza anzaje,Sio lazima 1m hata 50k mtu unaanza depends tu na unavyotaka kuanza.
 
Mkuu mimi ni olevel boy , napendelea hii business,kwa upande wa android video games store,kwa maono yako inawezakana?kivipi? MSAADA 🙏🙏🙏
sijaelewa Mkuu Android Video games Store yani umelenga hasa nini?
 
Yaani ,badala ya kuwa movie store iwe games store (iwe na collection zote za games)
INAWEZEKANA,

Games store huwezi kuwa na Computer pekee,kwasababu si games zote wateja wanaenda chezea kwenye computer,61% wateja wa games wanaenda chezea kwenye PS.

Kwahiyo itakubidi kwenye games store yako unapoifungua uwe na PS humo ndani za kuchezeshea games na kuelekeza wateja mawili matatu kuhusu games wanazochukua kwako.

Mteja anaweza kuja kwako kutaka game ya PES lakini akakuta unaplay Call of DUTY akalipenda ila hajui licheza, hivyo n wajibu wako kumuelekeza chap chap basic step za kulicheza call of duty.

Baada ya hapo atanunua yote mawili PES + Call of Duty,ila mwanzo alikuja na wazo la kufata game 1 tu lkn umemshawishi kwasabbu amekuta PS ndani ina call of duty,akashawishika.

GAMES STORE nadhani ni ya kibabe zaidi na niwachache wenye nazo Nimekagua kagua nikagundua wengi waliopo wanachezesha Games,yani wana PS za kutosha humo ndani ila hawana Games za kuuzia wateja.

Na wakiwa nazo ni zile games ambazo tu wanachezesha wao.ila kwakua wewe unafungua GAMES STORE na lengo lako hasa si kuchezesha bali kuuza GAMES nadhani wale wenye PS wachezesha watu Games wote watakua wateja wako,ki ufupi kufupisha Maelezo GAMES STORE ni ya KIBABE SANA

LAKINI

Games Store si kama Movie Store,movie store unaweza anza hata na 50k ila Games Store mtaji wake BABA acha kazi ufanye kazi,watu nimewatajia 4M wanatafutana,GAMES store mtaji wake N malaika tu wa mbinguni ajuae.

Computer ya MOvie store si sawa na ya Gamer
Computer ya Gamer mpk inakamilika kucheza Games zote (bei yake n moto fire)

Ki ufupi GAMES STORE sio rahisi kama MOVIE STORE but the more the cost the more the Profit.. Games Store n biashara ya ki boss sana Mkuu usi i underestimate hata kidogo,usije ukawa na ka 1M kako ukaanza fikiria kufungua Games Store utasingizia watu wamekuloga. 1M hata mashine tu ya GAMER haitoshi so JIPANGE kabla hujadumbukia eneo hilo.
 
Kuhusu leseni ya biashara, utaratibu unakua kama wa biashara zingine tu?
unakua na leseni na TIN ya biashara kAMA biashara zingine,kama na nyimbo unaingiza unakua na leseni na kibali pia toka TVLA.

Tanzania
Video
Library
Association

Hawa TVLA ndio wanao husika ktk kukamata kamata watu wanaoingiza nyimbo za wasanii bila vibali, wakikuotea hauna Kibali chao kukuchukua 500k ni jambo la kawaida sanaaa maana wanazungukaga na mapolisi na defender na wakija ofisini wanabeba mashine nzima na wewe wanakubeba.

Hawa ni kama (bwana pepsi) usiombwe kukutwa na hawa majamaaa wanatia hasara sanaaaaa, kama hujajipanga halafu ukakutana na hawa majamaa basi ndio mwisho wa hiyo biashara yako maana wako serious kuliko JAJI WA MAHAKAMA KUU.

Kama hutaki kero nao ili uwaepuke

-usiingize nyimbo za wasaniii wowote
-usiingize movie za Bongo
-kuwa serious na wewe,weka ofisi yako kiheshima (hawatokuja watapita kwa mbalii)

Ni hayo TU.
 
Biashara ya kurusha movie nimeifanya tangu mwaka 2011 mpaka 2014, baada ya hapo ikanipa connection ya kazi serikalini JPM alipo ingia madarakai msako wa vyeti feki ukaniondoa huko nikarudi kuifanya ndipo nikapata connectio kwenye kampuni ya wahindi , anay way ni story ndefu, naielewa changa moto zake, maswala ya kuliprishwa memory pale inapotafunwa na wadudu, mara computer kubooma, naona kwa sasa imenoka natamani kurudi tena kwenye biashara hii, ila miaka hiyo tulianza kwa ugumu kweli
We uko wapi njoo tushikiane tuifanye...
 
Back
Top Bottom