Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Naamini bado kuna wanawake wengi, walio tayari kufunga ndoa bila hata sherehe kama hawa waliofunga ndoa kwa askofu Zachary Kakobe.

Wanawake wanachotaka ni kupata mme wa kuishi; na ndio maana wengi wanaishi bila kufunga ndoa katika jamii.
 
Halafu wewe jamaa siyo muelewa kabisa,watu wameshaamua kufanya hivyo wewe unakomaa siyo sawa,wewe kama nani? Acha kupangia watu maisha
Muulize kama anazifahamu ndoa za mkeka zina gharama kubwa ⁉️
 
Uliza uambiwe kabla ya kuandika upotoshaji mbele ya umma kama huu. Nenda YEHODAYA kanisa la Full Gospel Bible Fellowship utafundishwa kweli ya neno la Mungu kwa usahihi.
 
Askofu Kakobe aliwahi kufungisha ndoa 50 kwa wakati mmoja miaka mingi iliyopita.
Wewe Mkaruka unashangaa hizi 21 ⁉️ Nina mashaka umri wako.
 
Hakuna mzazi au ndugu mwendawazimu wa kutofurahia mtoto wake kufunga ndoa labda mjumbe mpigaji fedha wasiokosa kila kamati za harusi atalalamika kukosa dili la pesa.
 
Mkuu unajaribu kupotosha uma!,hii inaitwa kubariki ndoa na wala sio ndio,hii ni kwa wale wanaoishi uchumba sugu na wanapika na kupakua,utakuwa hauelewi vizuri ndoa ni nini na kubariki ndoa ni nini !
Wewe Muuza simu used ndiye unayepotosha umma si MIMI.

Tukio hili si kubariki ndoa bali kufunga Ndoa Takatifu kwa watu ambao hawajawahi kukutana kimwili wala kuishi pamoja hata siku moja.
 

TUJIKUMBUSHE KUHUSU BINTI WA ASKOFU MKUU ZACHARY KAKOBE ALIPOFUNGA NDOA - JUMATANO 23.12.2020


Ni Praise Sifa Zachary Kakobe (34), ambaye ni binti wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe; aliyefunga ndoa na Joseph Hamisi Mkose (36), siku ya Jumatano 23.12.2020.





















Ndugu Joseph Mkose, amekuwa mshirika wa Kanisa la FGBF, kwa miaka 24, hususan, tangu akiwa na umri mdogo wa miaka 12. Mashahidi wa Ndoa hiyo, walikuwa ni, Mchungaji REUBEN MLAY na mkewe Mchungaji Msaidizi PAULINA MLAY, wa Kanisa la FGBF, kijiji cha KABUKU, wilaya ya Handeni.

Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe, alihubiri ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "MSIENENDE KAMA MATAIFA WAENENDAVYO" (WAEFESO 4:17)


Unaweza kutazama picha zaidi kupitia link >>> Album ya tukio la ndoa ya binti wa askofu Zachary Kakobe
 
Mkuu na wale walioamua kuishi bila kuoana, je mke akifa washawahi kosa majirani wa kuja msibani?? Maana hawajawahi kuwa na ubwabwa ni sogea tukae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…