Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Haha mkuu
Miaka 16 iliyopita nilifanya harusi na ilikuwa by far more cheaper than this , sikosoi bali nashangaa hiyo staging , haileti maana.

Uwe na asubuhi njema
Barikiwa sana, uwe na amani na mafanikio kwa kila ufanyalo kikubwa tu liwe la halali
 
ndoa shirikisha ndugu , marafiki na majirani ili hata siku mmojawapo wa wanandia akifa isiwe taabu ushirikisha ndugu , marafiki na majirani

Hapo hao wanandoa wa Kakobe wanewabania ndugu , majirani na marafiki wanajifanya ndoa inawahusu wenyewe wawili tu !!! Akifa mmojawapo hapo wanaanza kusumbua mitangazo kila kona ohhh ndugu,jirani na marafiki nasikitika kutangaza kifo cha mwenza wangu karibuni tushirikiane maombolezo na mazishi .Msiba ni watu na watu ndio nyie ndugu zangu , majirani na marafiki.Unafiki mtupu

Ndoa ni kitu cha community hiyo staili selfish ya hao wanandoa wa Kakobe haiko sahihi
 
Yeah, binafsi napendaga ndugu, majirani, na hata wapita njia wale ubweche mpk wabebe kwa nguo. Ni vzr ndugu washiriki furaha ya wanandoa. Kupunguza gharama huku kwetu watu huja wamefungasha vijizawadi, vyakula nk na huwa inapendeza. Hao wa Kakobe sijui watakuwa wana shida gani kama hawakupata kampani
Masihi mwenyewe alikuwepo kwenye harusi moja huko kana, divai ikaisha akafanya mambo yake watu wakaendelea kunywa kwa furaha.
 
Kwa hakika kuna funzo hapo kwa vijana wengine.

Mambo ya vikao vya harusi kwa miezi minne kutafuta michango kwa nguvu, kutumbua mamilioni lukuki kwa siku moja tu, na kisha kuanza maisha kukiwa na madeni ni shida.

Hongera Askofu Kakobe!
Hili swala la michango ya harusi na gharama zake kama wanajamii hebu tulitazamie upya especially nyakati hizi za ugumu wa maisha......
 
Kwahio hao ni wanaume kwa wanaume au ni malaika?? Acha upotoshaji
Amesemea kuhusu kupata mwanamke ambae atakuwa tayari kufanya ndoa ya gharama nafuu ni nadra. Hajasema kuwa hakuna mwanamke wa kufanya nae ndoa nafuu.
 
Inatia huruma nilichokiona hapo ni kuwa maharusi wanajioza hawaozwi na wazazi wala ndugu tofauti na makanisa mengine

Hiyo si nzuri kwa mahusiano ya wazazi na ndugu .Yaani kweli watu wanaoana hawana hata mzazi au ndugu wa kuwasindikiza wakishaoana wanaondoka kama wakiwa au yatima.Hivi kwa mtindo huo kuna hata mkwe au mzazi au ndugu atakwenda kukanyaga nyumbani kwa maharusi?

Huo mfumo unaua kabisa undugu.Wanatakiwa kuozwa sio kujioza ndio maana hata michango huwa haiitishwi na wanaooana huitishwa na wazazi au ndugu

Hata kipindi cha Yesu harusi zilikuwa sherehe mfano harusi ya kana

Hilo la watu kujiondokea tu utafikiri vibaka na kukimbilia daladala na bodaboda ni kudhalilisha ndoa
Unaweza kuta ndugu zao hawasali kanisa hilo, au walikuwapo ila hawajapiga picha tu.
 
issue sio kuwepo kuhudhuria ibada ya kufunga harusi ila huo uondokaji una walakini na umeficha mengi ! Walitakiwa kusidikizwa na ndugu hata kama wanaenda kwao

Wamekaa kikiwa mno sio sawa mtu mwenye wazazi na ndugu na majirani na marafiki kuondoka hivyo kuna walakini!!!
Nadhani walikuwa wanapiga picha tu kuonyesha kuwa ndoa yao haikuwa na mambo mengi kama misafara na kadhalika. Ila ndugu wanakosekanaje katika tukio kama hilo.
 
Vikao miezi 4, michango niyakuifukuzia, bajeti haiwiani na pesa mliyo ikusanya mnaingia madeni, kisa sherehe kubwaaa kama ya fulani mburaaaa, nikufunga ndoa halafu fyuuu jumbani kula kilichopo kesho yake kibaruani, wamependeza na kufanya lililojema.
Tatizo tunaishi jamii ya watu wanafiki sana. Wanaojifanya hawaoni kinachoendelea kwasababu ya unafiki tu. Gharama za ndoa ni unnecessary kwa maisha ya kijana wa sasa. Na hii ndio inafanya vijana kujizungusha zungusha inapokuja swala la ndoa wanakosa maamuzi ya wakati.

Ndio maana wale wanaoamua kufunga ndoa za fasta huwa hawapotezi muda....
 
Je majizo na lulu ni maskini.. mbona nao hawajafanya sherehe
... walipiga picha wakiwa wamepanda daladala na kuzirusha kwenye mitandao? Tunazungumzia ujumbe uliotumwa kwa jamii; hoja sio kufanya au kutofanya sherehe.
 
Hivi kwa nn wale mabibi harusi wengine uvaa mashera yale meupe tena yanameremeta kweli kwli lakini hawa maharusi wa kakobe mbona wamevaa magauni kama wanaenda kwenye send-off au kitchen part ila ongera zao
 
ISSUE HAPA NI KUTAKA KUUFANYA UMASIKINI FASHION ZA KUJISIFIA/KUJIVUNIA. HICHO NDICHO NINACHOKIKATAA! SEMA SINA PESA NAPANDA DALADALA! NITAKUSIFU
Hapana mkuu ishu hapa ni kuonyesha tofauti ya ndoa na harusi na pia kuonyesha sio kila ndoa ifuatiwe na harusi, pia haiitaji uwe na pesa ndio ufunge ndoa
 
Maisha tunatofautiana...kila MTU afanye kwa uwezo wake...masuala yakufanya harusi babkubwa huku maisha yako una unga unga ili kisa tu nawe uonekane ni ujinga.
 
Hahahahahah daaah Safi Sana very simple hakuna mbwembwe Wala majotroo[emoji1]
 
Kuna wadada mjini watasugua sana benchi na watarundikana makanisani wapate waume kumbe sometimes vitu huwa simple......kuna mdada alimpa MTU condition eti anataka Pete ya Tanzanite plus harusi yake ifunike ya wenzie...saiv yule mwanamke anazidi kufubaa tu mwaka wa tano yuko sokoni wateja hamna
 
Ilikuwa siku ya Ijumaa 19.2.2021, ni siku nyingine ya kukumbukwa, katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam, lililoko Barabara ya Sam Nujoma; pale ambapo jumla ya wahusika 84 waliposhiriki katika kufungwa kwa Ndoa 21, zilizofungwa kwa pamoja katika Ibada ya Ndoa iliyoanza saa 5 asubuhi. Wahusika hao 84, walikuwa ni Mabwana Arusi 21, na Mabibi Arusi 21, ambao hawajawahi kuishi pamoja; na jumla ya Mashahidi 42 (waume 21 na wake zao 21).

Kama ilivyo ada, katika Arusi hizo, viwango vya mavazi ya Mabwana na Mabibi Arusi, vilikuwa ni vilevile ambavyo vimekuwa vikizingatiwa, katika Ndoa mamia kwa mamia, zilizofungwa katika Kanisa la FGBF, kwa miaka zaidi ya 30; hususan tangu Askofu Mkuu Zachary Kakobe alipoliasisi Kanisa hili, tarehe 30.4.1989.

Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe alihubiri kwanza ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII" (WARUMI 12:2); kisha ndipo alipofungisha Ndoa hizo 21 kwa pamoja.

Suala lililowavutia sana wageni, waliohudhuria kwa mara ya kwanza, katika Ibada za Ndoa za Kanisa la FGBF, ni jinsi walivyowashuhudia Maarusi hao, wakitumia usafiri uleule wa kawaida ambao wamekuwa wakiutumia, wanapokwenda Kanisani, katika Ibada nyingine za kawaida. Baada ya kufunga Ndoa zao, Bwana Arusi mmoja mwenye gari lake, alikwenda na mkewe, nyumbani kwake, na gari lake hilohilo, huku akiliendesha mwenyewe.

Baadhi ya Maarusi, walikwenda kwao, kwa kutembea tu kwa miguu, huku wameshikana mikono kwa upendo na furaha isiyoelezeka; na kuwasisimua watu wengi. Siyo hilo tu, Maarusi wengine wengi walitembea kwa miguu, huku wamejaa bashasha, mpaka kwenye kituo cha daladala kilichoko jirani na Kanisa hilo, na kupanda daladala hizo zilizowapeleka majumbani kwao. Taarifa zilizopatikana baadaye, zinaeleza jinsi baadhi yao walivyokuwa wakihubiri Injili ndani ya daladala hizo walizozipanda.


Bwana Arusi mmoja, ambaye hutumia pikipiki (bodaboda) yake kuja Kanisani, alimvisha helmet (kofia ngumu) mkewe, kisha akampakia mkewe (Bibi Arusi), kwenye bodaboda hiyo, na kuondoka naye kwenda nyumbani, huku watu wengi walioshuhudia tukio hilo, wakishangilia kwa nderemo, vifijo na vigelegele !

"Basi atukuzwe Yeye (Mungu) awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina" (WAEFESO 3:20-21). MARANATHA !!!

Tazama picha zao

View attachment 1708770

View attachment 1708771View attachment 1708772View attachment 1708773View attachment 1708774View attachment 1708775View attachment 1708776View attachment 1708777View attachment 1708778View attachment 1708779View attachment 1708780View attachment 1708781View attachment 1708782View attachment 1708783View attachment 1708785View attachment 1708786View attachment 1708787View attachment 1708788View attachment 1708789View attachment 1708791View attachment 1708792View attachment 1708793View attachment 1708794View attachment 1708795View attachment 1708796View attachment 1708797View attachment 1708798View attachment 1708800View attachment 1708801View attachment 1708802

Mkuu unajaribu kupotosha uma!,hii inaitwa kubariki ndoa na wala sio ndio,hii ni kwa wale wanaoishi uchumba sugu na wanapika na kupakua,utakuwa hauelewi vizuri ndoa ni nini na kubariki ndoa ni nini !
 
Back
Top Bottom