Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Airtel hao wamevurugwaYaan hapo naitaman ya mwenye pik pik huyo
Sema picha hazifunguku
amini usiamini, hata mtoto wake wa kumzaa alifunga ndoa namna hiyohiyo mwezi huu wa pili, na ilifungwa ndoa moja tu siku hiyo. huo ndio umekuwa msimamo wa kakobe tangu naanza kumjua. sisali pale, ila huwa namfuatilia, na msimamo huo ni wa kweli, ya kwamba, mke anakuwa ashakuwa mkeo pale tu wazazi wa pande mbili wakikubaliana kuwa muoane, cha kwanza au any of them kinaweza kuanza ni ninyi kukubaliana, halafu wazazi wenu pia wakubaliana, na wewe ukatoe mahali, kwisha habari. hizo mbwembwe zingine ni mapambo tu. alikuwa anatofautiana na wenzake wwenye msimamo kwamba, mfano, mimi nimetoa posa, nimetoa mahali, ninaishi na mwanamke tumeshazaa watoto lakini hatujabarikiwa kanisani, yapo makanisa hadi leo yanasema hapo ndoa hakuna. lakini kwenye Bible yeye anasema hizo kubariki hazikuwepo, wazazi wakukubaliana kukupatia mke mkayamaliza kule home tayari amekuwa mkeo. huku church mnakuja tu kubarikiwa. ndio maana hata serikali inatambua ndoa zote kuwa ni sawa, ziwe za kikristo, za kiislam, za boman mbele ya serikali ni sawa tu, huko kubarikiwa au kutobarikiwa serikalii haitambui, kwasababu hata wale wa bomani huwa hawabarikiwi kiislam wala kikristo. yapo makanisa yametengenisha familia nyingie tu, mtu ameishi na mwanamke miaka kadhaa wamezaa watoto rundo, wameamua kwenda kwenye hilo kanisa, wanaambiwa mnaishi bila ndoa mnazini, achaneni.Mkuu unajaribu kupotosha uma!,hii inaitwa kubariki ndoa na wala sio ndio,hii ni kwa wale wanaoishi uchumba sugu na wanapika na kupakua,utakuwa hauelewi vizuri ndoa ni nini na kubariki ndoa ni nini !
Basi watu weusi wenye uchumi hoehae ndo wazee wa show off, wenzetu weupe walishatoka kwenye utumwa huo.Umasikini wako isiwe hoja kwa wenzako, kufa na shida zako wenzako wanatumia hela zao kufurahi dunini..
Shughuli ya wazazi inaishia kwenye posa.Inatia huruma nilichokiona hapo ni kuwa maharusi wanajioza hawaozwi na wazazi wala ndugu tofauti na makanisa mengine
Hiyo si nzuri kwa mahusiano ya wazazi na ndugu .Yaani kweli watu wanaoana hawana hata mzazi au ndugu wa kuwasindikiza wakishaoana wanaondoka kama wakiwa au yatima.Hivi kwa mtindo huo kuna hata mkwe au mzazi au ndugu atakwenda kukanyaga nyumbani kwa maharusi?
Huo mfumo unaua kabisa undugu.Wanatakiwa kuozwa sio kujioza ndio maana hata michango huwa haiitishwi na wanaooana huitishwa na wazazi au ndugu
Hata kipindi cha Yesu harusi zilikuwa sherehe mfano harusi ya kana
Hilo la watu kujiondokea tu utafikiri vibaka na kukimbilia daladala na bodaboda ni kudhalilisha ndoa
Mzee hayo madubwasha ya kukariri ndo madeni yenyewe.issue sio kuwepo kuhudhuria ibada ya kufunga harusi ila huo uondokaji una walakini na umeficha mengi ! Walitakiwa kusidikizwa na ndugu hata kama wanaenda kwao
Wamekaa kikiwa mno sio sawa mtu mwenye wazazi na ndugu na majirani na marafiki kuondoka hivyo kuna walakini!!!
Mbali ni kwamba imepunguza gharama, kwanza naona wamependeza sana kwa mavazi waliyovaa.Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Sana wamependeza sana,siyo makitu yasiyo na ulazima.Mbali ni kwamba imepunguza gharama, kwanza naona wamependeza sana kwa mavazi waliyovaa.
Pia kila anayeonekana kwenye picha ni mwenye furaha usoni. Kikubwa ni amani ya moyo na upendo wa dhati, haya mengine ni matokeo tu.
Sio siku moja ni masaa 60 tu. Haina haha ya kuhama pale unaposali unaweza kufunga watu wanne tu.Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Wabongo wanafik jinsi wanavyopenda msosi na bia afu uwaambie ndo kanisan tu !!!mmmhIlikuwa siku ya Ijumaa 19.2.2021, ni siku nyingine ya kukumbukwa, katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam, lililoko Barabara ya Sam Nujoma; pale ambapo jumla ya wahusika 84 waliposhiriki katika kufungwa kwa Ndoa 21, zilizofungwa kwa pamoja katika Ibada ya Ndoa iliyoanza saa 5 asubuhi. Wahusika hao 84, walikuwa ni Mabwana Arusi 21, na Mabibi Arusi 21, ambao hawajawahi kuishi pamoja; na jumla ya Mashahidi 42 (waume 21 na wake zao 21).
Kama ilivyo ada, katika Arusi hizo, viwango vya mavazi ya Mabwana na Mabibi Arusi, vilikuwa ni vilevile ambavyo vimekuwa vikizingatiwa, katika Ndoa mamia kwa mamia, zilizofungwa katika Kanisa la FGBF, kwa miaka zaidi ya 30; hususan tangu Askofu Mkuu Zachary Kakobe alipoliasisi Kanisa hili, tarehe 30.4.1989.
Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe alihubiri kwanza ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII" (WARUMI 12:2); kisha ndipo alipofungisha Ndoa hizo 21 kwa pamoja.
Suala lililowavutia sana wageni, waliohudhuria kwa mara ya kwanza, katika Ibada za Ndoa za Kanisa la FGBF, ni jinsi walivyowashuhudia Maarusi hao, wakitumia usafiri uleule wa kawaida ambao wamekuwa wakiutumia, wanapokwenda Kanisani, katika Ibada nyingine za kawaida. Baada ya kufunga Ndoa zao, Bwana Arusi mmoja mwenye gari lake, alikwenda na mkewe, nyumbani kwake, na gari lake hilohilo, huku akiliendesha mwenyewe.
Baadhi ya Maarusi, walikwenda kwao, kwa kutembea tu kwa miguu, huku wameshikana mikono kwa upendo na furaha isiyoelezeka; na kuwasisimua watu wengi. Siyo hilo tu, Maarusi wengine wengi walitembea kwa miguu, huku wamejaa bashasha, mpaka kwenye kituo cha daladala kilichoko jirani na Kanisa hilo, na kupanda daladala hizo zilizowapeleka majumbani kwao. Taarifa zilizopatikana baadaye, zinaeleza jinsi baadhi yao walivyokuwa wakihubiri Injili ndani ya daladala hizo walizozipanda.
Bwana Arusi mmoja, ambaye hutumia pikipiki (bodaboda) yake kuja Kanisani, alimvisha helmet (kofia ngumu) mkewe, kisha akampakia mkewe (Bibi Arusi), kwenye bodaboda hiyo, na kuondoka naye kwenda nyumbani, huku watu wengi walioshuhudia tukio hilo, wakishangilia kwa nderemo, vifijo na vigelegele !
"Basi atukuzwe Yeye (Mungu) awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina" (WAEFESO 3:20-21). MARANATHA !!!
Tazama picha zao
View attachment 1708770
View attachment 1708771View attachment 1708772View attachment 1708773View attachment 1708774View attachment 1708775View attachment 1708776View attachment 1708777View attachment 1708778View attachment 1708779View attachment 1708780View attachment 1708781View attachment 1708782View attachment 1708783View attachment 1708785View attachment 1708786View attachment 1708787View attachment 1708788View attachment 1708789View attachment 1708791View attachment 1708792View attachment 1708793View attachment 1708794View attachment 1708795View attachment 1708796View attachment 1708797View attachment 1708798View attachment 1708800View attachment 1708801View attachment 1708802
Watu wa aina yako tunawajua shida zao unawanyima watu sherehe ya harusi yako hakafu huyo nkeo akifariki huko ndani kelele unapiga mtaa nzima kuwa umefiwa na mjeo waje msibani wakati kwrnye harusi hukuwaalika unajifanya mtu wa principle usiyetaka kuingiliwa personal affairs zako na mkeo!!!