Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Tofautisha kati ya NDOA na SHEREHE.

NDOA haijawahi kuwa na GHARAMA kubwa hata siku moja.

Narudia tena NDOA haijawahi kuwa na GHARAMA.

Fungeni ndoa kama mnataka kuoana, achaneni na SHEREHE.
Ki
Unless useme labda kikwazo ni MAHARI, kitu ambacho kanisa halihusiki bali ni makubaliano ya wazazi.
Kwa Watanzania hii kitu kueleweka ni ngumu sana watu wanataka mpka sherehe ndiyo kuanza kusumbuana na kadi za michango
 
Huku kwetu hata kwa baiskeli au kwa mguu watu wanatembea na sio big issue. Ndoa ni sakrament, sio show off
Nakubali lakini husindikizwa na ndugu wakishafunga ndoa na sherehe hufanyika nyumbani wakila vyakula vilivyoko hapohapo kijijini.Wakishatoka Kanisani huenda kwa miguu au baiskeli umati wa wanakijiji ndugu majirani nk wakiwasindikiza hawawi wapweke kama hao wa Kakobe
 
Uislam dini nzuri sana kwenye upande wa kuoa 😂😂😂,,, pisi 4 za kwenda ruksa kuzimiliki kwa gharama ya chupa za chai na mandazi tu.
Hatari mpka nafikilia ning'oe pisi ya hijabu hizi za vitenge vya santini ni cost sana mara ununue vitu upeleke kwa mashangazi zake wote ndiyo ubebe mke kwa hili hawataniona ,😆😆🤸🤸
 
Mbona hamkuwasindikiza kupanda daladala na bodaboda mlijificha wapi?
Kwa mfano sisi ndugu yetu kuna vikao kabla ya ndoa yao tulifanya juu ya maandalizi ya siku hiyo lakina alikataa kufanya sherehe Wala kuwachangisha watu.
Tulialikwa kuhudhuria ndoa yao kanisani lakini pia walitukaribisha jioni tukabariki nyumbani kwao.

Ndugu yangu aliondoka kwa usafiri wa uba na mkewe. Na sisi tukatawanyika kila mtu kwake.
 
Uislam dini nzuri sana kwenye upande wa kuoa 😂😂😂,,, pisi 4 za kwenda ruksa kuzimiliki kwa gharama ya chupa za chai na mandazi tu.
Ndoa za kiislamu zimerahisishwa kulingana na zenyewe zilivyo.

Kwanza ukishatoa barua tu ( Probably Tsh 30,000 ) tayari unaruhusiwa kupiga mashine hata kuzalisha au kwenda kulala kabisa kwao. Wakizingua unarudishiwa chako.

Hata ukishaoa unaweza kutoa talaka 1, ukaendekeza ubabe, ya pili tena then ujamrudia ukikumbuka goma mpaka 3 ndio mwisho.

Unaweza kuoa wengine vile vile mpaka 4.

Note: Hatpa inategemeana na hadhi ya familia unakooa.


Sasa Sisi kwetu ( siyo kidini ) ukishatoa mahari ndio kwanza demu anamibdwa kama mboni ya jicho 🤣🤣.

Na hata kishika uchumba ukishatoa ( siyo pungufu ya Tsh 100,000 ) huwa hakirudishwi hicho ukighairi.
 
Hatari mpka nafikilia ning'oe pisi ya hijabu hizi za vitenge vya santini ni cost sana mara ununue vitu upeleke kwa mashangazi zake wote ndiyo ubebe mke kwa hili hawataniona ,😆😆🤸🤸
Chukua mtoto wa hijab tu mzee. Muhimu sana huko kwenye WAX mambo ni mengi.
 
Zamani walokole tulifikiri umasikini ni sifa njema na ni ishara ya uaminifu, wakati hata kwenye biblia Abraham baba wa imani alikuwa tajiri, kufunga ndoa na kumpakia mke kwenye daladala sio sifa njema wakuu tusake pesa.
 
Kwa mfano sisi ndugu yetu kuna vikao kabla ya ndoa yao tulifanya juu ya maandalizi ya siku hiyo lakina alikataa kufanya sherehe Wala kuwachangisha watu.
Tulialikwa kuhudhuria ndoa yao kanisani lakini pia walitukaribisha jioni tukabariki nyumbani kwao.

Ndugu yangu aliondoka kwa usafiri wa uba na mkewe. Na sisi tukatawanyika kila mtu kwake.
Kukiri kuwa kuna tatizo hakugharimu kitu.Huo uondokaji wa bila kuwasindikiza maharusi hauko sawa .Hizi picha na maelezo ya mleta mada yanajitosheleza kabisa ba yanaonyesha hali halisi ya ndoa zote 21 kuwa hakuna hata moja iliyosindikizwa kuondoka iwe na waumini iwe na ndugu iwe na marafiki au majirani

Baada ya kufunga walijiondokea kama wakiwa au yatima kwenda nakwao kuanza maisha ya upweke ya ndoa
 
Nakubali lakini husindikizwa na ndugu wakishafunga ndoa na sherehe hufanyika nyumbani wakila vyakula vilivyoko hapohapo kijijini.Wakishatoka Kanisani huenda kwa miguu au baiskeli umati wa wanakijiji ndugu majirani nk wakiwasindikiza hawawi wapweke kama hao wa Kakobe
Yeah, binafsi napendaga ndugu, majirani, na hata wapita njia wale ubweche mpk wabebe kwa nguo. Ni vzr ndugu washiriki furaha ya wanandoa. Kupunguza gharama huku kwetu watu huja wamefungasha vijizawadi, vyakula nk na huwa inapendeza. Hao wa Kakobe sijui watakuwa wana shida gani kama hawakupata kampani
 
ISSUE HAPA NI KUTAKA KUUFANYA UMASIKINI FASHION ZA KUJISIFIA. HICHO NDICHO NINACHOKIKATAA! SEMA SINA PESA NAPANDA DALADALA! NITAKUSIFU
Mkuu swala sio umaskini, kubwa ni mtu akubaliane na Hali yake , shida kubwa watu wanafanya shughuli kubwa kutegemea michango ya majirani na ndugu inakuwa Vita sio furaha. Ifike mahali kila mmoja afanye Jambo kulingana na kipato chake. Tusiforce vitu Kama viko nje ya uwezo.
 
Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Huwa mnahangaika sana!

Wanaojitambua siku hizi wanafunga ndoa serikalini. The process is very CLEAN and simple.

Huna haja ya kubebelea mapipa ya pilau na kualika kijiji kizima.

Funga ndoa, rudi nyumbani. Haina makelele.
 
Ni Jambo jema lakini kwa Karne hii mtihani mkubwa ni kumpata mwanamke atakayekubali kufunga ndoa bila sherehe kubwa. Wengi wanataka sherehe ya kifahari, msafara wa magari na miosho mingi ili mji mzima wajue kuwa ameolewa. Ukigusia swala la ndoa bila sherehe wanakukimbia
Hawajitambui.

Na ukiona hivyo, ujue hiyo ni dalili ya kwanza ya mwanamke mpuuzi.

Atakusumbua sana!
 
Mkija kuambiwa hao ni watu waliokodiwa toka sehemu mbali mbali msije mkashtuka tu 🤣🤣
 
Ilikuwa siku ya Ijumaa 19.2.2021, ni siku nyingine ya kukumbukwa, katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam, lililoko Barabara ya Sam Nujoma; pale ambapo jumla ya wahusika 84 waliposhiriki katika kufungwa kwa Ndoa 21, zilizofungwa kwa pamoja katika Ibada ya Ndoa iliyoanza saa 5 asubuhi. Wahusika hao 84, walikuwa ni Mabwana Arusi 21, na Mabibi Arusi 21, ambao hawajawahi kuishi pamoja; na jumla ya Mashahidi 42 (waume 21 na wake zao 21).

Kama ilivyo ada, katika Arusi hizo, viwango vya mavazi ya Mabwana na Mabibi Arusi, vilikuwa ni vilevile ambavyo vimekuwa vikizingatiwa, katika Ndoa mamia kwa mamia, zilizofungwa katika Kanisa la FGBF, kwa miaka zaidi ya 30; hususan tangu Askofu Mkuu Zachary Kakobe alipoliasisi Kanisa hili, tarehe 30.4.1989.

Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe alihubiri kwanza ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII" (WARUMI 12:2); kisha ndipo alipofungisha Ndoa hizo 21 kwa pamoja.

Suala lililowavutia sana wageni, waliohudhuria kwa mara ya kwanza, katika Ibada za Ndoa za Kanisa la FGBF, ni jinsi walivyowashuhudia Maarusi hao, wakitumia usafiri uleule wa kawaida ambao wamekuwa wakiutumia, wanapokwenda Kanisani, katika Ibada nyingine za kawaida. Baada ya kufunga Ndoa zao, Bwana Arusi mmoja mwenye gari lake, alikwenda na mkewe, nyumbani kwake, na gari lake hilohilo, huku akiliendesha mwenyewe. Baadhi ya Maarusi, walikwenda kwao, kwa kutembea tu kwa miguu, huku wameshikana mikono kwa upendo na furaha isiyoelezeka; na kuwasisimua watu wengi. Siyo hilo tu, Maarusi wengine wengi walitembea kwa miguu, huku wamejaa bashasha, mpaka kwenye kituo cha daladala kilichoko jirani na Kanisa hilo, na kupanda daladala hizo zilizowapeleka majumbani kwao. Taarifa zilizopatikana baadaye, zinaeleza jinsi baadhi yao walivyokuwa wakihubiri Injili ndani ya daladala hizo walizozipanda.

Bwana Arusi mmoja, ambaye hutumia pikipiki (bodaboda) yake kuja Kanisani, alimvisha helmet (kofia ngumu) mkewe, kisha akampakia mkewe (Bibi Arusi), kwenye bodaboda hiyo, na kuondoka naye kwenda nyumbani, huku watu wengi walioshuhudia tukio hilo, wakishangilia kwa nderemo, vifijo na vigelegele !

"Basi atukuzwe Yeye (Mungu) awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina" (WAEFESO 3:20-21). MARANATHA !!!

Tazama picha zao

View attachment 1708770

View attachment 1708771View attachment 1708772View attachment 1708773View attachment 1708774View attachment 1708775View attachment 1708776View attachment 1708777View attachment 1708778View attachment 1708779View attachment 1708780View attachment 1708781View attachment 1708782View attachment 1708783View attachment 1708785View attachment 1708786View attachment 1708787View attachment 1708788View attachment 1708789View attachment 1708791View attachment 1708792View attachment 1708793View attachment 1708794View attachment 1708795View attachment 1708796View attachment 1708797View attachment 1708798View attachment 1708800View attachment 1708801View attachment 1708802
Ilikuwa kabla ya ujio wa barakoa!?
 
Huwa mnahangaika sana!

Wanaojitambua siku hizi wanafunga ndoa serikalini. The process is very CLEAN and simple.

Huna haja ya kubebelea mapipa ya pilau na kualika kijiji kizima.

Funga ndoa, rudi nyumbani. Haina makelele.
Watu wa aina yako tunawajua shida zao unawanyima watu sherehe ya harusi yako hakafu huyo nkeo akifariki huko ndani kelele unapiga mtaa nzima kuwa umefiwa na mjeo waje msibani wakati kwrnye harusi hukuwaalika unajifanya mtu wa principle usiyetaka kuingiliwa personal affairs zako na mkeo!!!
 
Back
Top Bottom