Kwa CHADEMA kuwa Rafiki na Chama cha Kikiristo cha UJERUMANI, Wanafuata Mrengo wa chama hicho?

Kwa CHADEMA kuwa Rafiki na Chama cha Kikiristo cha UJERUMANI, Wanafuata Mrengo wa chama hicho?

Status
Not open for further replies.
mkuu, kwanza lazima utambue kuwa ushirikiano wa mtu na mtu ni tofauti na chama au taasisi. vyama hushirikiana vile ambavyo vina sera zinazolingana. bibafsi naona kuna hoja hapo imejificha hasa kutokana na hulka za viongozi wa chadema kuwa na upendeleo wa wazi wa kidini

WATANZANIA wengine wanafiki sana, yaani hapa wanainanga CDU lakini kila mwaka tunapokea misaada kibao kutoka Ujerumani inayoongozwa na CDU. Sasa si tungesema hatutaki hiyo misaada maana CDU ni chama cha Kikristo??

Hivi unajua serikali ya CDU imewapa hifadhi Waislamu kutoka Somalia,Uturuki n.k kiasi gani?? mbona hatusemi msiende huko kwenye nchi inayoongozwa na chama cha CDU??
Bajeti yetu ina upungufu wa karibu 40% na wanaojalizia hiyo 40% ndio hao CDU, twapokea tena tukitabasamu sana na tunaomba zaidi, ila leo hatutaki kushirikana nao hata kwa ushauri eti kwa kua ni Ukristo.

Hivi chama cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP) wanapinga uwepo wa MUNGU, na ukiwa unaamini MUNGU uwe Mkristo au Muislam ukijulikana unafukuzwa uanachama wa CCP. Wao CCP ni marafiki wa CCM sasa unataka kutuaminisha kuwa CCM nao ni watu wanaopinga uwepo wa MUNGU ndio mana wanatajwa kulipua watu kwa mambomu na risasi?? CCP kinatajwa kukiuka haki za binadamu sasa je na CCM ni hivyo ndio mana Waalimu wakidai nyongeza wanatishwa?? au ndio mana wazee wa East Africa hawajalipwa hadi leo??

Acga ushabiki na tulia jiulize ushirika wa CDU na CHADEMA ni kwenye maeneo gani?? au CCM na CCP ni kwenye maeneo gani???
 
Tungewekewa katiba au ilani ya uchaguzi ya CDM tungepata majibu ya udini, ukabila wa CDM
 
Hoja ni balozi anayewakikisha nchi kujihusisha na ukada wa chama ndani ya nchi anayowakilisha. Na hapa CCM mtueleze CHINA inahusikaje na kulipua mabomu kule Arusha. Je lengo lilikuwa kubomoa CHADEMA kwakuwa wanapinga mikataba ile mingi ya siri, ya kifisadi lakini yenye maslahi kwao?
HOJA HAPA URAFIKI WA CHINA NA CCM UNAMANUFAA KWA WA TZ Wote AU ni kwa ajili tu ya WACHINA NA MAFISADI wanaokihodhi CCM? including kuokoa mtoto asinyongwe. Na je URAFIKI WA CHADEMA NA CDU AU CSU UMELETA MADHARA GANI KWA WA TZ?
 
Wadau,


Wakati wa Kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani zikiwa zimepamba moto, tumeshuhudia muungano wa vyama kwa misingi ya itikadi za vyama hivyo. CDU cha Angel Merkel ambacho ni cha Kikristo, kinashirikiana na vyama vingine vyenye mrengo wa kikristo kikipambana na vyama vingine vya mrengo wa kati. Ikumbukwe kuwa CDU ndo chama rafiki cha CHADEMA na wamekuwa wakiitumia taasisi ya KAS kutengeneza vyama vibaraka ulimwenguni kote ambavyo vinafuata mrengo wa Kikristo. Kutokana na Katiba ya hapa Tanzania kutoruhusu vyama vya mrengo huo, tumeshuhudia CHADEMA wakitekeleza sera za CDU kwa kificho. kwa CHADEMA kuwa rafiki na chama cha kikristo na kutokana na chama hicho kuwa na mwelekeo wa kupendelea watu wa dini ya kikristo hasa katika kupanga safu ya uongozi na uteuzi wa nafazi za wagombea, je si wakati muafaka sasa wa kukifuta chama hiki? Tujiridhishe jinsi wajerumani wenyewe wanavyoelezea muungano wa vyama hivyo;


Neck-And-Neck Race Ups Grand Coalition Chances

A neck-and-neck race between Chancellor Angela Merkel’s center-right coalition and the center-left opposition parties increases the likelihood of a grand coalition in Germany, according to a poll published Tuesday.

Ahead of Sunday elections, the findings of Forsa institute indicate only two coalitions would have a workable majority.
First, a grand coalition between Ms. Merkel’s Christian Democrats, the Bavarian Christian Social Union sister party and the opposition Social Democrats would get a solid majority to run the next government.
A second possibility would be a coalition between the Christian Democrats and their Christian Social Union partner with the opposition Greens, but this is unlikely due to disagreement on issues like national security and the environment.
In Tuesday’s poll, Ms. Merkel’s present coalition with the pro-business Free Democrats secured 44% in combined support, based on 39% for the Christian Democrats and Christian Social Union, and 5% for the Free Democrats.
The Social Democrats of chancellor candidate Peer Steinbrueck, the Greens and Left party also had 44% in combined support. Of that, the Social Democrats had 25%, the Left party 10% and the Greens 9%.
The apparent stalemate comes as support slipped for Ms. Merkel’s coalition partner, the Free Democrats. At 5%, the party was one percentage point lower than last week, casting doubt on whether election day would see it meet the 5% threshold needed to enter parliament.
The euro-skeptic party Alternative for Germany remained at 3%, but Forsa said it is hard to predict turnout because voters aren’t openly expressing support for the new party.

Hoja dhaifu, nani kakuambia kuwa CDM na CDU wanashirikiana katika ukristo? Kwani ni vimesajiliwa kama vyama vya kidini au kisiasa? Je wajerumani wamekulalamikia kuwa wanabaguliwa kutokana na dini zao na chama tawala hivyo uwasaidie watanzania kuachana na chama chochote rafiki na CDU? Kama ndo hivyo; vip ccm ni chama cha kikomunist? Mbona kimeazima mpaka balozi kuwasaideni kupiga kampeni? Fikira zangu ni kwamba kwenye siasa kuna maslahi mapana zaidi ya dini!
 
Wacha ushamba wa siasa za kimataifa chama cha CD si cha kidini ni jina tuu. Pia angalia CCM ina urafiki na chama cha kikomonist cha China ambacho hakiamini uwepo wa MUNGU, je utasema nacho kinafuata imani hiyo ya Wachina?
 
Chadema ni chama killicho waz bila maficho kutekeleza sera za kanisa alichokisema mheshimiwa kina ukweli sema tu ubishi na ushabiki tu hamna kingine.......
 
Ponda kapigwa na serikali ya ccm ambaye mw\kit wake tunajua ni din gan je ccm ni wakristo wote kwa kumpiga ponda simama jitambue muache propaganda
 
WATANZANIA wengine
wanafiki sana, yaani hapa wanainanga CDU lakini kila mwaka tunapokea
misaada kibao kutoka Ujerumani inayoongozwa na CDU. Sasa si tungesema
hatutaki hiyo misaada maana CDU ni chama cha Kikristo??

Hivi unajua serikali ya CDU imewapa hifadhi Waislamu kutoka
Somalia,Uturuki n.k kiasi gani?? mbona hatusemi msiende huko kwenye nchi
inayoongozwa na chama cha CDU??
Bajeti yetu ina upungufu wa karibu 40% na wanaojalizia hiyo 40% ndio hao
CDU, twapokea tena tukitabasamu sana na tunaomba zaidi, ila leo
hatutaki kushirikana nao hata kwa ushauri eti kwa kua ni Ukristo.

Hivi chama cha Kikomunisti Cha Uchina (CCP) wanapinga uwepo wa MUNGU, na
ukiwa unaamini MUNGU uwe Mkristo au Muislam ukijulikana unafukuzwa
uanachama wa CCP. Wao CCP ni marafiki wa CCM sasa unataka kutuaminisha
kuwa CCM nao ni watu wanaopinga uwepo wa MUNGU ndio mana wanatajwa
kulipua watu kwa mambomu na risasi?? CCP kinatajwa kukiuka haki za
binadamu sasa je na CCM ni hivyo ndio mana Waalimu wakidai nyongeza
wanatishwa?? au ndio mana wazee wa East Africa hawajalipwa hadi leo??

Acga ushabiki na tulia jiulize ushirika wa CDU na CHADEMA ni kwenye
maeneo gani?? au CCM na CCP ni kwenye maeneo gani???

toa uongo wako hapa. ujerumani wanatoa misaada gani kwa serikali zaidi ya kusaidia CHADEMA tu?
 
Hoja dhaifu, nani kakuambia
kuwa CDM na CDU wanashirikiana katika ukristo? Kwani ni vimesajiliwa
kama vyama vya kidini au kisiasa? Je wajerumani wamekulalamikia kuwa
wanabaguliwa kutokana na dini zao na chama tawala hivyo uwasaidie
watanzania kuachana na chama chochote rafiki na CDU? Kama ndo hivyo; vip
ccm ni chama cha kikomunist? Mbona kimeazima mpaka balozi kuwasaideni
kupiga kampeni? Fikira zangu ni kwamba kwenye siasa kuna maslahi mapana
zaidi ya dini!

haya ndo madhara ya kulewa viroba. umesoma lakini hujaelewa. CDU maana yake ni Christian Democratic Union. chadema kwa tafsiri ya uswazi ili wafanane nao ni Christian Democratic Movement (CDM)
 
Chadema ni chama makini.Suala la kushirikiana na chama chenye itikadi tofauti siyo tatizo,dunia hii ya sasa huwezi ukaishi kama kisiwa.Au umesahau kwamba Nyerere alikuwa ni rafiki wa Soviet Union,Cuba na North Korea ambazo zilikuwa zinafuata itikadi ya UJAMAA na wakati huo huo akiwa ni rafiki wa Raisi John F kennedy wa USA ambayo inafuata itikadi ya UPEPARI.Leo CCM bado inashirikiana na China ya kisoshalist wakati Tz ujamaa umebaki kwenye makaratasi tu ya CCM.Mbona huhoji Raisi wako kikwete kwenda nchi za kiislamu kuomba misaada wakati TZ si nchi ya kiislamu?Jambo la msingi ndugu yangu hata kama unashirikina na yeyote la msingi ni kuhakikisha maslahi ya taifa hayawekwi rehani.Kumbuka CHADEMA ni chama cha mlengo wa kati(LIBERALS)hivyo wanaweza kushirikiana na yeyote pasipo kuhatarisha maslahi ya nchi.
 
hebu ainisha hzo sera za CDU zinazopandikizwa nchini otherwz kajpange..omba wanalumumba wakuelekezee namna ya kutunga uongo uonekane ukweli..
 
Hoja yako nini?!!chama kuwa na chama rafiki ktk nchi nyingine tatzo ni nini! Bac tufunge baloz zet katka nchi za zinazotawaliwa na sharia i mean nchi za uarabuni kama katib yetu hairuhusu. Ila njaa bana!!
 
Umeuliza swali zuri Elton John Ritz...nadhani ungemwambia huyu Elton John mwenzio mleta thread atuambie CHADEMA wanashirikiana na chama hicho kwenye maeneo gani?
Akili za Bavicha utazijua tu kwa michango yao haya nenda mtaa wa Ufipa ukachukue viroba vyako.
 
Nchi hii sikuzote ukisema ukweli sio unaonekana hufai,mchochezi ktk jamii lakini mm siachi kusema ukweli,kwasababu ndivyo nilivyo umbwa namutanichukia kweli,kama ponda anavyoonewa na serikali hii dhalimu kwa sababu kasimama kwenye ukweli
 
toa uongo wako hapa. ujerumani wanatoa misaada gani kwa serikali zaidi ya kusaidia CHADEMA tu?

Wewe jamaa wa ajabu sana yaani hujui kua bajeti ya nchi yetu inachangiwa na Ujerumani??? Hii ni aibu sana

Sasa naanza kujua ni mtu wa namna gani asiyejua hata abc za Nchi yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom